Uncategorized

FEEDBACK YA STORY YA AMINA YULE DADA MWENYE KISASI

By  | 
Nimeona mnaulizia sana kutaka kujua nini kinaendelea kuhusu Amina kwa wale mnaokumbuka kisa chake.Kwanza naomba niseme kisa hiki ni chakweli kabisa hatuna haja ya kutunga chochote ili kuvutia usikilizwaji wa kipindi.Dunia hii ina mambo mengi sana yanayotokea ambayo wakati mwingine ni magumu kuaminika lakini ni kweli.Mnakumbuka story ya house boy  Kigamboni aliyemuua housegirl waliyekuwa wakifanya wote kazi katika nyumba moja?akamzika hapo hapo nyumbani na akatengeneza mazingira ionekane dada alitoroka na watu wote wakaamini dada alitoroka kumbe kafa na kazikwa hapo hapo nyumbani.Baada ya mwaka kupita ndio houseboy anasema ukweli tena baada ya yule dada marehemu kuwa anamtokea mara kwa kwa mara kumtaka aseme ukweli.Aliposema ukweli akaonyesha alipomzika kweli pakafukuliwa na kukutwa mabaki ya mwili yule dada.Mpaka leo yule kaka kesi yake inaendelea maana alikataa sio yeye aliyeua alidai yeye alimkuta dada kafa akaamua kumzika kwa kuogopa ataonekana yeye ndio kaua.
Anyway tuache hili sasa kuhusu Amina wote tulisikia toka amebakwa na kuambukizwa HIV,ujauzito ni miaka 11 iliyopita na hajawahi kumwambia mtu yoyote zaidi ya madaktari waliomuhudumua na mama aliyemuuokota baada ya kubakwa.
Tumesikia kisasi alichonacho na ni mara ngapi amethubutu kutaka kuua.Mtu kama huyu hayupo sawa na wote tumeliona hilo.Japo amekubali kukutanishwa na yule mama aliyemfukuza nyumbani chanzo kilichopelekea yeye kubakwa lazima kuwe na process.
Nimeongea na wanasaikolojia wakanishauri kabla ya kumpeleka kukutana na huyo mama lazima apitie hatua flani za matibabu.Tunaweza kwenda kule akamuona mbaya wake hali ikabadilika isiwe rahisi kama tunavyohisi pengine akajaribu kufanya kitu kibaya tukiwa hapo hapo.
Nimejaribu kumconnect na Aunty Sadaka lakini Sadaka amekuwa busy sana nimeshindwa.Nilichofanya nilimpa nauli arudi kwao akamwangalie mtoto wake aliyekuwa amemuachia kwa mtu.
Mwanasaikolojia Chriss Mauki ameingia jana akitokea shule SA ndio amekubali kushughulikia suala la Amina.
Wiki ijayo nitamtumia nauli Amina aje kwa jambo hilo pia kuna shekhe nimeshaongea nae ili kumsaidia kiimani maana yeye ni muislam kama kuna visomo au dua maalum asaidiwe.
Baada ya hapo ndio tuingie kwenye hatua ya kukutana na mtuhumiwa.Sio kitu rahisi kukitolea majibu ni process maana huyu mama ana kidonda cha miaka 11.Mimi ndio nimekaa nae na kuongea nae ni mwanamke aliyekosa furaha,matumaini ni kama anaishi kusindikiza wengine duniani.Ndani yake ni mweupe hana maisha kabisa. 
Iwapo kutatokea any update nitawataarifu sura yake na picha zake nimevifadhi mpaka muda utakaofika wa kufanya hivyo kwa idhini yake mwenyewe.

12 Comments

 1. zena juma

  November 26, 2013 at 9:18 am

  haya maisha inafikia wakati unakata tamaa kabisa, but ukiamini kuwa Mungu yupo na kila kitu hutokea juu yake basi unamwachia yeye, maana akipanga kuwa kuna stage utapitia huwezi kupinga katu, anatakiwa tu amina ajue hii dunia si ya binadamu ni yake yeye Muumba Mbingu na vyote vilivyomo, so anatakiwa kumkabidhi maisha yake kwa kila kitu, ajiulize iweje yeye mpaka leo u hai tena akiwa ni muathirika wa Ukimwi toka hiyo miaka 11 ilyopita wangapi washapoteza uhai? ni wengi sana still yeye yuko hai, ni kukubaliana na hali halisi ya maisha, maisha yana mitihani mingi sana but ukijua yote ni kwaji ya Mungu basi unamwachia mwenyewe. na huyo mama amsamehe saba mara sabini hata asipolipwa hapa duniani basi hata akhera Mungu atakulipa. afanye ibada ndio nguzo kuu

 2. zena juma

  November 26, 2013 at 9:22 am

  out of topic toka mmerekebisha hiyo studio yenu kuwapata imekuwa shidddddddddd kweli kweli mara leo mnapatikana mara kesho no signal basi tabu tupu, rekebisheni poa basi tuwapate au na mMhz nazo mmebadilisha, twambieni basi, mi niko Morogoro

 3. Anonymous

  November 26, 2013 at 12:09 pm

  ni kweli umefanya mambo kisomi and kiprofessional da dina.we nye subira wasubirie,hii sio udaku unaanza kutoa picha za muhusika,nooo haitakiwi endelea mwaya is agud job na trust me utaona kesi kama hizo zitakavyo fumuka mama angu watu wameumizwaa dina watu wanamajeraha makubwa,na watu wameshindwa kufanikiwa kutokana na laan hza watu na vinyongo hakika huwezi kufanikiwa au kuwa na furaha maishani kama wewe ni mtendwa au mtenda. kikubwa tujifunze kusamehe na kumuomba mungu kila mtu kwa imani yake atuwezeshe kuishi maisha ya kusamehe.

 4. Anonymous

  November 26, 2013 at 1:16 pm

  Thnx for the updates mummy ..unafanya kazi nzuri sana.. Mimi penda we we sana.. Be blessed dina..

 5. Ald

  November 26, 2013 at 2:03 pm

  Out of Topic:
  Happy birthday Dina. Naomba basi uwe unatushirikisha, tusione kwa majirani tu jamani……Tupo wengi tunaokutakia maisha mema na marefu

 6. Saada Hassan

  November 27, 2013 at 5:12 am

  Asante kwa mrejesho wa taarifa ya Amina. Mimi nina shauri kidogo kuhusu afya yake naomba kama akija mumshauri ajiunge na vikundi vya watu wanaoishi na VVU atapata faraja pia msaada wa lishe na mawazo pia. Kama sikosei nilivyomsikiliza yeye huwa anakwenda kwa mtu ambaye ni daktari na si kliniki ya watu wanaoishi na VVU. Pia alielezea kwamba huwa anachanganya vitamin yeye mwenyewe kwa utundu wake kwa ajili ya kupaka mwili. Namuombea kwa M'Mungu ampe moyo wa kusamehe, ataishi kwa amani sana.

 7. Anonymous

  November 27, 2013 at 6:56 am

  mbona siku izi hampatikani hewani?mdau japan

 8. Anonymous

  November 27, 2013 at 11:04 am

  asante kwa usiri ulio nao juu ya huyo mama pia ukweli watu.wengi wana majeraha hatariii sana moyoni mwao mtawapata wengi.sana pia ndipo ninapo kupendea feedback ni muhimu sana pia.ukweli wengi hawafanikiwi kwa ajili ya laaan zawatu huyo mama ana watoto hakika mlipo ya kila.kitu ni hapa duniani mbinguni ni hukumu tuuu.ongera.dina siwezi kusikia redio yenu ila naingoja hapahapa kwa hamu story hii.pia hizo pesa uwapzo una pata wapiiii tengeneza din foundation

 9. Anonymous

  November 27, 2013 at 8:17 pm

  morogoro clouds ni majanga au inaelekea kuded?

 10. Anonymous

  November 28, 2013 at 3:33 pm

  Hi, da Dina. Hongera kwa kazi kubwa unayofanya. Mungu akutie nguvu

 11. RUKY

  November 28, 2013 at 4:33 pm

  THANKX DINA INSHAALAH ITAKUWA KHERI NA MOLA ATAMSAIDA..AMEEN

 12. Anonymous

  December 5, 2013 at 4:26 pm

  Mungu akubariki mnoooo Dina

Leave a Reply