Uncategorized

MUME AMUUA MKEWE KIKATILI NA MWILI KUUFICHA STOO!

By  | 
 Ni kifo cha kusikitisha cha mwanamke huyo pichani Hamida Urembo na muhusika wa mauaji hayo ni mumewe wa ndoa waliyeishi kwa miaka mitatu.Hamida alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu  mwaka watatu na alikuwa anatarajia kugraduate mwezi huu chuoni hapo.
Hamida na mumewe yahaya walibahatika kupata mtoto wa kike mwenye miaka mitatu sasa.Kwa mujibu wa dada wa Hamida ndoa yao ilikuwa ya misuko suko sana.Mume alikuwa sio mwaminifu mara nyingi alikuwa akizini nje.Ukiacha hilo alikuwa akimpiga sana mkewe mpaka kumzimisha.
Matatizo ambayo ndugu walikuwa wakiyajua na walishasuluhisha mara nyingi na Hamida kurudi kwa mume kuendelea na maisha.Hii ya mwisho ndio ilikuwa kubwa zaidi.Mume alikuwa akimtongoza housegirl hapo nyumbani na housegirl akamfahamisha mama.
Akamueleza jinsi gani muwewe amekuwa akimsumbua kumtaka kimapenzi.Hamida akamwambia anataka tu uthibitisho kama ni kweli.Siku ya siku Yahaya akamlazimisha Hamida kwenda kwao na Hamida akakubali akijua kuna jambo.Akasindikizana na mumewe mpaka kituoni mume akijua mkewe hayupo kumbe mke aligeuzia njiani akarudi nyumbani akajificha chini ya uvungu chumbani kwa housegirl wake.Baadae mume akawasilia na housegirl kuwa anarudi nyumbani,aliporudi akaendelea kuomba mambo tena akavua nguo kabisa akabaki na boxer.Wakati huo yupo chumbani kwao na mkewe.Housegirl akamwambia wahamie chumbani kwako hapo sio salama.Basi wakahamia chumbani na akawa ndio anamuinamisha dada ili amfanye Hamida akatoka chini ya uvungu ili kumuokoa dada na kumuonyesha mumewe kuwa alikuwepo na amejua usaliti wake.Na alipokuwa chini ya uvungu alikuwa akirekodi kila kitu kwenye simu na alipotoka na picha akapiga.
Yahaya mume wa Hamida pichani
Hamida alitoka hapo akashitaki kwao na kwao wakamwambia aende kwa mjomba wa mumewe kumueleza matatizo ya mtoto wao.Alipofika kwa mjomba akaambiwa wanaume ndivyo walivyo avumilie tu arudi kwa mumewe.
Hamida akarudii kwao akiwa hana raha lakini uamuzi aliouchukua ni kuachana na mumewe kwani alikuwa kashachoka.
Wakawa wakivutana sana mume akimsihi arudi nyumbani walikokuwa wakiishi Mbagala ila Hamida hakuridhia.
Story ya Hamida ni ndefu sana hapa naipeleka huku nikiruka ruka.
Hamida alishaenda mpaka Bakwata ili mumewe aamriwe kutoa talaka.
Mwisho wa Hamida kuonekana nyumbani ni siku ambayo yeye na ndugu zake walikuwa waende kijijini kwao kwenye viwanja walivyopewa na babu yao.Ila siku hiyo Hamida alitoa udhuru kuwa haendi na akamtaarifu mama yake kuwa Yahaya kamuita akachukue vitu vyake vilivyobakia.Mama akamkatalia kwenda akamwambia kuna kaka zake wakubwa aache wataenda kuvifata kwani huyo mume ni mshenzi anaweza kumfanyia kitu kibaya.Hamida akamwambia mama anataka kwenda mwenyewe kwani kuna vyeti vyake muhimu akavichukue.
Basi mama akamuacha aende kishingo upande lakini mama akamwambia basi nenda hata na mdogo wako.Akaenda na mdogo wake kufika kule mume akamkatalia mdogo mtu kuingia ndani.
Wakabishana sana kwa nini asiingie mdogo mtu kuepusha shari akaenda kukaa kwa jirani asubiri kuitwa.Akakaa na muda kupita kukawa kimya akajua wale wameelewana ndio maana hakuna makelele hivyo akaendelea kusubiri.
Akakaa weee mpaka jioni giza lilipoanza kuingia kidogo Yahaya akampigia simu kwa kutumia simu ya Hamida akimwambia aondoke tu arudi nyumbani wao wameshaondoka na vyombo wamebeba.
Mdogo mtu akaondoka kurudi nyumbani kwao Tabata akijua mke na mume wameelewana kumbe dada yake ameshakufa ndani.
Mdogo mtu akafika nyumbani saa mbili usiku na kumwambia mama jinsi Hamida alivyomuudhi kamuacha yeye kwa jirani na akaondoka na mumewe Yahaya.Mama machale yakamcheza akanyanyua simu akampigia Yahaya kumuuliza mwane yupo wapi.Yahaya akamjibu kuwa ameachana nae kitambo mama akamwambia sio kweli mwanangu hawezi kuchelewa kurudi nyumbani na hana kawaida hiyo.Yahaya akamjibu atarudi tu Hamida mtu mzima.
Mama tayari alishajua kuna jambo akampigia simu baba Hamida aliyekuwa Arusha kumtaarifu kilichotokea.Baba Hamida akampigia Yahaya lakini hakupokea simu.Wasiwasi ukazidi kutanda na ndugu kupeana taarifa zaidi.Asubuhi kulipokucha wakaenda Mbagala kwa Yahaya lakini wakatoa taarifa polisi.Polisi wakawaondoa wasiwasi kwamba hao wanajuana wenyewe labda wameamua kukumbushiana.
Ndugu hawakuridhika wakaenda kwa mjumbe awaruhusu wavunje nyumba waingie ndani pengine kamfungia ndani maana ilikuwa kawaida yake kufanya hivyo kumfungia Hamida ndani.Basi mjumbe akaruhusu mlango uvunjwe walipoingia ndani palikuwa patupu hawakuona kitu wala dalili za mauaji.Kuna chumba ambacho ni stoo hicho walishindwa kufungua na mjumbe akawaambia hiyo ni stoo wanawekaga mavitu yamejazana humo basi wakakiacha wakaondoka.
Hawakuishia hapo bado waliendelea kumsaka Hamida bila mafanikio.
Hamida alipotea toka jumapili iliyopita,jumanne juzi  wakapanga kila mtu akamtafute popote pale anapoona anaweza kumpata.Mama akaenda kwenye maombi kanisani wakati muislam,dada akaenda blue pearl kazini kwa Yahaya na huku majirani Mbagala wakaanza kuona inzi na harufu kali ikitoka nyumbani kwa Yahaya.Ikabidi mjumbe apige simu kwa mama Hamida kumueleza kinachoendelea polisi wakaitwa,nyumba ikavunjwa ili kutafuta harufu inatokea wapi.Wakavunja kile chumba cha stoo na kukuta mwili wa Hamida umeshaanza kuharibika.Kanyongwa na kamba ya katani na kitenge kafungwa puani na mdomoni.Mwili wake ukawekwa kwenye mfuko akajaziwa mito na manguo nguo na tendegu la kitanda kawekewa shingoni.
Ndugu,polisi wakachukuwa mwili kwa ajili ya msiba na mazishi wakati huo Yahaya alishakimbia siku nyingi hajulikani alipo.
Hamida alizikwa jana jumatano kule kwa babu yake Mzenga uzaramuni walipokuwa waende  kwenye mashamba waliyopewa.Msiba upo nyumbani kwao Tabata.Na ameacha mtoto wa kike wa miaka mitatu anaitwa Tayana.
Habari hii tumeianza kusikiliza leo inaendelea tena kesho katika heka heka za leo ndani ya leo tena ya clouds fm.

65 Comments

 1. Anonymous

  November 7, 2013 at 5:59 pm

  Hii stori imenitia hasira mno kupindukia mpk nimemkosea Mungu, nimepata hasiira sana ukizingatia juzi juzi tu wifi yangu alikuwa anafanyiwa vituko kama hivyo vya Yahaya kwa Hamida mpk nkaamua kumuhamisha wifi yangu kwa siri toka kwa huyo mwanaume. Wifi yangu amehamia mkoa mwingne juzi ndo kapata uhamisho kamili ila mumewe hajui, na nimemshauri abadiili namba za simu. WOSIA WANGU KWA WANAWAKE WENZANGU, JAMANI PENZI LIKIISHA LITACIPUKA LINGINE ILA UHAI HAUNA MBADALA,, KWA MAANA HIYO BASI VITUKO VIKISHAANZA NI BORA KUANDAA AKILI NA MWILI ILI KUACHANA NA HAYO MAHUSIANO HATA KAMA ULIFUNGIA HARUSI ANGANI. pls jamani roho huwa inaniumaga sana kusikia vifo vya wadada coz of Love. HAMIDA UMENIUMA AS IF NINAKUFAHAMU MPK MACHOZI YAMENITOKA. MUNGU AKUPUMZISHE KWA AMANI.. Yahaya huwezi kukimbia milele, utakutana na mkono wa sheria soon.

  • Anonymous

   November 9, 2013 at 5:55 am

   mimi mwenyewe imenitia hasira kwa kweli hii jamii yetu inabidi tubadilike mkiona mwanaume anamtendea mwanamke matendo ya unyanyasaji jamii iingilie kati hapo majirani mlikua mnaona vitendo hakuna aliethubutu kuingilia kati au wanaume wenzake kumuita huyo Yahaya na kumuasa, pengine wengine mlikua mnawafanya kama hadithi tu mnaishia yule baba anampiga mke wake kila siku inakua ni kicheko badala ya kuchukulia jambo kwa uzito, wananchi muamke mkiona mwanajamii mwenzenu anamatendo yasiyoendana na jamii mumtolee macho na kama hasikii mumfukuze kwenye jamii mtaa wenu hapo msifikiri walioathirika ni wanafamilia peke yao hata nyinyi na watoto wenu wameathirika kuona unyama wa aina hii badilikeni haya mambo ya eti wanaume ndivyo walivyo vumilia tu haya leo hii mnazika kijana mdogo kabisa ambaye ni tegemeo la Taifa

  • Anonymous

   November 9, 2013 at 5:59 am

   wabongo na nyie muachege tabia ya kuchekana mwanamke ndoa ikiwa chungu anaogopa kuondoka kuogopa kuchekwa na waliomzunguka utasikia ndoa imemshinda nawaasa muwe mnapeana moyo muache kucheka wenzenu kuna ndoa zingine sio za kuvumilia kama hii unavumilia kitu gani hapo? umeona mwisho wake? mkiona mwenzenu ameacha ndoa mumsifu ameepuka makubwa sio kucheka na kumfanya ajisikie anachofanya sio sahihi wanawake wenzangu ukiona dalili ambazo zinaelekea kubaya ondoka kwenye hiyo ndoa rudi kwenu utapata anayekupenda na kukuthamini kuna binadamu wamezaliwa na ugonjwa wa akili

  • Anonymous

   November 20, 2013 at 6:32 pm

   jamani muda mwingine unakuta watu wanasema siri za wanandoa waachieni wenyewe. Sasa wakigombana usiku, makelele na vilio huku wamefungiana ndani,,alafu asubuh wanaamka wapo kawaida na maisha yao, ni vigumu kuamua mambo ya ndani maana hayakuhusu. Ndio maana hata majirani nahisi walishindwa pa kuanzia jaman. Ila imeniuma sana,,kiukweli watu tumrudieni Mungu hakika hizi ni nyakati za mwisho

 2. Anonymous

  November 7, 2013 at 7:22 pm

  Mungu ampumzishe huyu dada kwa amani.Kweli kuna wanaume wanyama sana.

 3. Anonymous

  November 7, 2013 at 7:23 pm

  Kuna wanaume ni wanyama sana jamani

 4. Anonymous

  November 7, 2013 at 9:33 pm

  It hurts were r we goin pliiiz du samtin inauma sana pole kW familia

 5. Ruky

  November 7, 2013 at 10:45 pm

  JAMANI INASIKITISHA ONA POLISI WETU WALIVYO WAPUUZI..ETI LABDA WANAKUMBUSHIANA UWIII MI NTAOZEA HUKU KWA WAZUNGU HATA NIKIJIKWA NIKIPIGA 999 NUSU SAA WAPO MLANGONI..NAHII KESI WANGE INGINZWA MPKA MAPOLUC WALIYOPO ZAMU WAKAJIBU UTUMBO…INAUMA SANA KUONA WANANCHI HATUPO KWNYE MIKONO SALAMA YANI MPKA MTU KAOZA NDIYO INAJULIKANA MAMA YAKE ANALIYAJE….DINA TUMALIZIE HUMU WENGINE MUDA HUO WA HEKA HEKA NDIYO TUNAELEKEA KAZINI

 6. Anonymous

  November 7, 2013 at 11:21 pm

  Maskini Hamida. R.I.P
  Yaani kuna wanaume ni washenzi kupindukia. Naamini sheria itachukua mkondo wake pindi akikamatwa.
  Poleni sana familia ya marehemu.

 7. Anonymous

  November 8, 2013 at 6:44 am

  INASIKITISHA JAMANI..SO INNOCENT GIRL..MAY HER SOUL REST IN PEACE

 8. Anonymous

  November 8, 2013 at 8:39 am

  Me jamani napata hasira na watu kama hawa jamaniiii!! hivi ni nini hiki!? ni kitu gani haswa kinachomfanya mtu kumuuua mtu ilihali ukiwa umpendi!! unajisikiaje ukiwa unaumiza roho ya mwenzako na mwenzako akaamua akapumzike kwao ukutosheka ukataka ummalize kabisa usimwone duniani ni nini hiki?? wanaume mbona makatili hivi? Dina naomba ulete mada hizi kwenye kipindi chako ambayo itaweza kuwaelimisha hawa wanaume, wawe kama wanaume wa nchi za wenzetu, kama mtu umemchoka unaona kabisa mimi na yeye upendo umekwisha kabisaaa na hujisikii chochote chonde chonde mwacheee, maana huyu mwanaume hakuwa kabisa na upendo wa dhati kwa mkewe, yaani roho inaumaa sana ili janaume linyongwewe mbali hukooo.

 9. Anonymous

  November 8, 2013 at 8:59 am

  binadamu binadamu binadamu tumebadilika sanaaaaaaa ni zaidi ya shetani, maana tunatenda dhambi za dhahiri kama mungu hayupo jamaniii, maana watu wanatenda dhambi mpaka shetani anaogopa, jamani inauma sanaaaaaaaaa, duh pole sana familia ya hamida Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hichi kigumu

 10. Anonymous

  November 8, 2013 at 9:57 am

  wanaume ni makatili sana huyo mwanaume alaaniwe mpaka kufa

 11. Anonymous

  November 8, 2013 at 10:08 am

  JAMANI DUNIA INAENDA WAPI? WANAWAKE TUSIACHE MAJONZI KWENYE FAMILIA NA WATOTOWETU TUKAWAPA TABU DUNIANI KISA MAPENZI TUAMUE SASA TUSITESEKE KWA WANAUME -TUWE NA MAAMUZI PENZI LIKIINGIA DOSARI TUACHANE NALO
  WAZAZI WA PANDE MBILI TUSIFATE MILA NA DESTURI ZA ZAMANI ETI KUSULUHISHA MATATIZO MWANAMKE ARUDU KWA MUMEWE WANGAPI WAMEACHIKA DUNIANI
  HAMIDA LALA PEMA PEPONI UMEUMIA MAISHANI MPAKA SIKU YA MAUTI
  WANAUME KAMA YAHAYA JARIBUNI KUYAKABILI MATATIZO KIHWANI UKIANZA KUTAMANI NJE MPE TALAK MKEO KULIKO KUUMIZANA
  ILA HUYU KAKA ANAUGONJWA KICHWANI

 12. Anonymous

  November 8, 2013 at 10:28 am

  Imeniuma, sijui binadamu wakati mwingine huwa tunapumbazwa vipi mpaka tunavumilia namna hiyo, halafu unamuamini mtu kupitiliza. Poleni wanafamili, huyo yahaya asubiri hesabu yake tu, na siku hizi ile ya kusema "malipo kesho kwa Mungu" haipo tena, malipo ni hapa hapa, asubiri damu ya mke wake itakavyoanza kumtesa. Pumzika kwa amani Hamida

 13. esther nyalusi

  November 8, 2013 at 11:12 am

  Daaaaa kweli binadamu tumekuwa wanyama may her soul rest in peace

 14. Anonymous

  November 8, 2013 at 11:44 am

  Mi sielewi najiuliza wala sipati jibu inamaana Yahaya alimpenda sana Hamida? na kama alimpenda sana Hamida kwa nn alikuwa akimtenda kiasi hicho, inawezekanaje mtu umpende halafu umsaliti, umdharau, umkere, maana Yahaya anajifanya alimpenda sana Hamida ndo maana akaona hawezi mksosa bora amuue.kama si alikuwa pretenda tu, sijamuelewa Yahaya. damu ya mtu bwana huwa haipotei hata ukimbilie ulaya damu yake itakutesa hata usiposhikwa na polisi cha moto utakiona huko uliko. dhambi zote za hamida umezibeba yahya maama umeingilia mamlaka ya Mungu. Ujue Dina hii inafanya watu wachukie wanaume, inafanya watu waogope kuolewa kwa mwanaume mkatili kama huyu. story hii imenitesa sana kiakili."Pumzika kwa Aman Hamida"

 15. Anonymous

  November 8, 2013 at 12:08 pm

  huyu yahya ni mnyama kiasi hiki jamn dada mzuri hv alimkosea nn kikubwa hvyo mpk amuue duh nimesikitika sana laiti angejua asingeenda mama hamida pole sana kwa msiba!!!! jamn polce kwakweli haki itendeke

 16. Anonymous

  November 8, 2013 at 12:35 pm

  inahuzunisha kweli..uyo yahaya ata nayee anyongwe kabisa… rip hamida…

 17. Anonymous

  November 8, 2013 at 4:27 pm

  Jaman namna hii ata tutaogopa kuolewa mana da dina ujui mwenzio anakuwazia nini ee mwenyez mung tunusuru inatisha sana lala peponi hamida roho inauma jaman wanaume. Hawa

 18. Cymah Wandelt

  November 8, 2013 at 9:10 pm

  Pumzika salama Hamida, umenikumbusha rafiki yangu wakatibu tulimaliza Wote la saba na akaolewa, limume likamuua hivi hivi. Inauma sana. Asante Dina kwa maelezo ya Kina, nilisoma global ila haikuwa hivi. Ubarikiwe

 19. Anonymous

  November 8, 2013 at 9:35 pm

  May God rest her Soul in peace! Ameeeeeeeeeeee!!

 20. Anonymous

  November 9, 2013 at 9:52 am

  kwakwel mpaka nalia jamani, hivi ni kwann mtu ana hata hofu ya kumuogopa Mungu anazani alijumba mwenyewe na yeye kama pua imeangali chini basi atamfuata tu hamida kama alivyomtanguliza mwenzake. na hata kama ukikimbia vipi serikali haikimbiwi bwana yahaya usiekuwa na pakuishi jela inakuhusu we mwanaume na ulaaniwe na Mungu.Eeehe Mungu tupe moyo wa kushaimmili matataizo na ofu yakukuogopa wewe Mungu

 21. Anonymous

  November 9, 2013 at 10:38 am

  pole sana kwa familia

 22. Anonymous

  November 9, 2013 at 10:42 am

  huyu kaka tulikua twafanya nae kazi alikua mpole mfano hakuna, kumbe rohoni ni mnyama, sijaamini yahaya anaweza fanya jambo kama hili, inauma sana, Mungu ampumzishe kwa amani huyu dada.

 23. Anonymous

  November 9, 2013 at 7:01 pm

  Ctaki kuamini kama kitendo cha mauaji kinafanyika na vyombo vya usalama vinapuuzia r.i.p Hamida ila aliyeua kwa upanga atauwawa kwa upanga

 24. Anonymous

  November 9, 2013 at 7:01 pm

  Ctaki kuamini r.i.p hamida

 25. Mwanaisha Saidy

  November 11, 2013 at 6:03 am

  Inasikitisha sana

 26. Anonymous

  November 11, 2013 at 6:20 am

  Hi Dina
  Mie nimesikiliza toka mwanzo kwa kweli inaumiza na hawa polisi wetu awapo makini na kazi zao eti wameenda kukumbushiana wakati mzazi moja haikai wala mbili jaman damu nzito wabadilike na mtu akienda kutoa report wafuatilie kwa umakini wao pesa mbele wangepewa pesa wangeenda haraka sana.Pole kwa familia lakini damu ya mtu haipotei hivi hivi huyo yahaya atakamatwa tu na yy auliwe mbali coz si binadamu ni shetani tu

  Kwa upande wa wasichana walioolewa jamani ugomvi ukizidi sana majumbani na kuwa kero kwa family ni heri kurud nyjmbani kuliko kung'ang'ania suluhisho kila tunapogombana na wanaume zetu majumbani inasikitisha na kuudhunisha jamani.

 27. Anonymous

  November 11, 2013 at 7:35 am

  this is a very sad story, binadamu wengine wana roho ngumu sana, how can you kill someone? Eeh mwenyezi Mungu tuepushie mbali na majanga haya

 28. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:01 am

  Yaani huu YAHYA jamani ikitokea nimekutana naye kwa bahati nikamkumbuka sura yake nitapiga kelele za mwizi kuwa ameniibia mpaka watu wajae wamkung'ute mpaka ashike adabu yake. Kwa kweli inatia uchungu sana kama alikuwa kamchoka mke wake angemuacha tu. Kwanza anaonekana ni LAYMAN tu hata elimu hana. Maskini Hamida alikuwa anakuonea wivu kwa kuwa umemzidi elimu. Mshenzi kabisa na alaaniwe na Mungu wetu. Nina hasira naye sana. Dada yake kajieleza kwa uchungu hadi nimelia jamani.

 29. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:04 am

  Mungu wangu binadamu tumekuwa hatari sana kweli pole kwa familia ya hamida, ila huyu mwanaume na ndugu zake wajue Malipo ni hapa hapa duniani, hasa ndugu walisema yahaya pia amefariki na ilihali yuko hai watakipata tena kitakuwa hatari

 30. grace

  November 11, 2013 at 10:07 am

  Duuh!kweli ni wenzetu ila tuishi nao kwa akili sn,jamani ndoa ngumu

 31. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:10 am

  Aaa mungu amlaze peponi narehem

 32. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:16 am

  Wanaume watu wa ajabu sana, . . . .Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi

 33. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:16 am

  Dah. Hilo jamaa natamani nilikamate. Nalo lipige lizime

 34. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:18 am

  r.i.p Hamida!

 35. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:23 am

  Mungu ailaze roho ya Hamida mahala pema pepon…amen,,,,,ningeomba sheria ifate mkondo wake juu chini huyo asiye binadamu(yahya)akamatwe yan km sheria ingekuwa unachukulia kiholela kwa m2 km huyo mm ningempa adhabu yake…nawachukia wanaume wenyemikono ya kupiga na kutothamin wake zao….mungu nyoosha fimbo yako imfikie yahya

 36. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:25 am

  R.I.P HAMIDA upumzike kwa amani

 37. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:26 am

  nmejkuta nalia tu mwanzo mpaka mwisho

 38. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:27 am

  malipo ni apa apa dunian roho ya mtu aipotei ivi ivi,

 39. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:37 am

  KINGU.Maskini dada wa watu mrembo na msichana mbichi mwenye malengo yake ya baadae! kweli inasikitisha,wenda ukute huyo bwana alikua bonge la mshika dini mnafiki.Mungu amrehemu marehem kwa wingi wa rehema zake amina

 40. Deogracia Mabuga

  November 11, 2013 at 10:45 am

  yani huyo kaka ana roho ngumu kiasi gani kuua mtu hadi kufa…!yani hadi nasisimka hapa,baya gani alomtendea binti wa watu maskini!

 41. Anonymous

  November 11, 2013 at 11:00 am

  Utashangaa sn kuona huyu mtu hatapatikana kweli hata kama akitokomoe nje ya nchi kwa kuzamia au vipi akamatwe tu jamani inauma mno mno mno nyie wanaume msiopendwa kuachwa basi heshimuni ndoa zenu… Iweje mpende kuvumiliwa tu jamani?wapo watu wameua wanawake na hadi leo hawajakamatwa. Mm nina binamu yangu alichinjwa miaka mingi sana n hadi leo huyo mwanaume hajapatikana. Kisho chake kilipelekea hadi baba yake kufa na mama yake kuwa kama chizi hadi leo lakni huyo mtuhumiwa hajakamatwa. Wanaume ikishindikana kubalini kiachwa jamanj kuliko kumwaga damu kwa makosa yenu wenyewe. Hata mimi nimelia sana yani inauma mno mno mno. Mungu aipe nguvu familia ya Hamida.

 42. Anonymous

  November 11, 2013 at 11:03 am

  Dada diva picha haionekani jaribuni kuweka picha inayoonekana mana huwezi kumtambua

 43. Anonymous

  November 11, 2013 at 12:00 pm

  wanawake muwe carefully kwny love, pindi uonapo vitimbi, achana nae kwan mbna wanaume wapo wengi2.
  Yahaya c binadamu wa kawaida, pindi akamatwapo afanyiwe reseach ya lyf yake pamoja na kazi anazojihucsha nazo. Yaonesha anaweza kua na mambo ya hatari anayojhucsha nayo pia yaweza ikawa Hamida c mwanamke wa kwanza kumtendea hvo.
  Mapolic fanyen utafiti wa kina kupata nyeti za huyo Ibilic.
  KWENU FAMILIA MUNGU AWATIE NGUVU KTK KIPINDI HICHI CHOTE KIGUMU.

 44. Anonymous

  November 11, 2013 at 12:10 pm

  huyu mwanaume naona kama hakua binadama manake yaweza akawa ni pepo lilloilovaa uhucka wa kbinadam…haiwezekani mateso aliyoyapata marehemu na bado ndugu wapumbazike kias kile pacpo hata mwenye upeo wa hekima wakutatua mgogoro huo huku wakicghunguza mwenendo wa mtuhumiwa…Imeniuma sana kwa kifo cha dada huyu amepata mateso makali sana.Endapo aliefanya ukatili huu akawa ni binadam kamili basi hapana pasikumnyonga kabisa au afie jela milele….
  JK..Chugga

 45. Anonymous

  November 11, 2013 at 12:39 pm

  Tukida haki zetu na kuutokomeza mfumo dume tunaonekana jeuri…….wanawake tusikate tamaa,mwisho wa hizi tabia utafika…nyie baadhi ya wanaume hebu tambueni nafasi yenu na muheshimu wanawake jamani

 46. Anonymous

  November 11, 2013 at 12:43 pm

  pole mtoto Tayana na familia ya Hamida,RIP Hamida umekufa ktk hali ya manyanyaso mengi na mtu ambae mliahidiana mengi ktk mwanzo wa mapenzi yenu,binadamu sasa tunawindana afadhali ht ya wanyama.

 47. Anonymous

  November 11, 2013 at 12:53 pm

  Story hii imenisikitisha sana, hizi ndoa sijui zimekuaje siku hizi na mapenzi sijui yameingia dosari gani. Mdogo wangu tumemzika juzi, alikufa katika mazingira ya kutatanisha, mpaka sasa ndugu zake tumebaki na kitendawili kisichotenguka na ndugu wa mume na mume mwenyewe wakitucheka maana wanajua walichokifanya.
  Eeeehhh…. Mwenyezi mungu tunusuru sisi na wanetu kwenye majanga ya namna hii.
  Dina usiache kutupa taarifa huyu shetani Yahaya akipatikana.
  Polisi nao wanapaswa kujua wajibu wao wakiletewa janga, sio kujisema mambo ya kubuni bila kufanya utafiti wa kina.
  Kina dada na nyie mkiona ndoa haiendi hebu ondokeni jamani, talaka itakufuata huko uliko. uhai wako ni muhimu kuliko huyo mume mwenye roho ya kishetani. Kama unagombea mali, utapata nyingine.
  Huyo mdogo wangu kilimponza mali, kisa alidai wamechuma vitu vingi na mumewe hivyo hataki kuondoka hadi wagawane, ndipo mauti yalipomfika tukaachwa midomo wazi, Warangi wakitucheka…

 48. Anonymous

  November 11, 2013 at 1:15 pm

  Da dinnah mbona Huyu yahaya mkatili haonekani vizur tutafutien picha inayomuonyesha vizuri ili nikimuona nimkamate mwenyew mtamkuta police

 49. Anonymous

  November 11, 2013 at 1:20 pm

  Jaman vituko vyote alivyomfanyia kaona haitoshi mpk amuondoe Dunian,nimelia sana na hii stor,damu ya mtu haiendi bure atakamatwa tu huyo YAHAYA,pole kwa familia ya HAMIDA na Mungu ampe kauli thabti marehem hamida

 50. Anonymous

  November 11, 2013 at 1:45 pm

  Huyu kaka katili sana kashindwa hata kumfikiria mtoto wake ambae ni malaika hajui kitu,looooo kama movie vile kumbe reality.RIP Hamida poleni sana wana familia

 51. Anonymous

  November 11, 2013 at 5:28 pm

  Inasikitisha sana mungu ailaze roho ya marehemu mahalipema peponi. TUNAOMBA UTUWEKEE PICHA YA MTUHUMIWA YAHAYA INAYOONEKANA VIZURI ILI TUMTAMBUE VIZURI. Nawapa pole wafiwa wote mungu awape nguvu.

 52. Anonymous

  November 11, 2013 at 6:54 pm

  Mmh nimeishiwa maneno!!ila mtu kuwa na hofu ya mungu Ni kila kitu,..r.i.p mrembo

 53. Anonymous

  November 11, 2013 at 8:30 pm

  inasikitisha sana duh

 54. Anonymous

  November 12, 2013 at 6:48 am

  Inauma sana kwa familia poleni sana. Mwanaume kama Yahaya hafai katika jamii!!!! na ndugu zangu wanaume kama mnaona bado maisha yenu si ya kuwa na mke mmoja bora kuacha kuoa kwanza ili mfanye ufuska mpaka mtosheke ndiyo muamue kuoa.

 55. Anonymous

  November 12, 2013 at 9:18 am

  Inasikitisha sana jamani, yaani binti mdogo ameondoka sababu ya mapenzi. Kina dada au wanawake wenzangu, ifikie hatua tuwe tunahiamini, mapenzi yanaishaga, sasa ukiona mwenzako hana mapenzi tena na wewe usilazimishe, tunaweza sema ndoa ni uvunilivu, lakini sio kweli kwamba vyote vinavumilika, ukiona Kuna vitisho visivyoeleweka ondoka ndugu yangu, Rudi hata kwenu ukajipange upya, achana na mambo ya talaka, kwani talaka si ni maandishi tu? Kama hataki kukupa hiyo talaka wewe ondoka, na ukiona kwenu atakisumbua kajifiche popote kwa muda. Tena kama mna watoto beba na wanao maana watateseka tu hapo. Tatizo wengi wahajiamini kuwa maisha lazima yaendelee, ama uko na huyo mwanaume ama uko mwenyewe, lazima maisha yaendelee tu. Angalia yaliyomkuta Hamida, lies somo kwa wengine jamani, ukifanya maamizi usirudi nyuma, yaani asikilaghai kwa lolote, eti ukachukue vitu vyako, vya nini? Kwani ukishajipanga si utapata vingine? Tena vizuri zaidi na hata mume utampata mwingine atakayeendana na wewe. R.I.P Hamida.

 56. Anonymous

  November 12, 2013 at 10:22 am

  Yaani ingekuwa ni kufa kwa ajili ya mapenzi basi kusingekuwa na mwanamme hata mmoja wote wangeshakufa. Ila sijui cc wanawake tuna mioyo ya chuma!..tunafanyiwa vitimbwi vya kila rangi lakini walaaaa tunasamehe maisha yanakwenda…ila wafanyie hao wenye moyo wa nyama weeeeee….ni kunyongwa tuuuu. Ohooo lord mpokee mtumishi wako Hamida apate pumziko la milele….. AMINA

 57. Anonymous

  November 12, 2013 at 12:27 pm

  Innalilah wainnaillayh rrajiun

 58. Anonymous

  November 12, 2013 at 1:42 pm

  Poleni sana Mr & Mrs I. Urembo.

 59. Anonymous

  November 12, 2013 at 2:01 pm

  Dada Dinna tuwekee picha nzuri.TUMUONE VIZURI MUUAJI YAHAYA.

 60. dinamariesblog

  November 12, 2013 at 4:28 pm

  Kuhusu picha ya YAHAYA familia ilikuwa na picha hii kwa wakati huo na ilikuwa haiwezekani kuichukua kufanyia scanning kwa wakati huo maana na wao walikuwa wakiihitaji ndio ikapigwa ikatokea hivyo ikiwa ahionekani vizuri.Labda tuulize tena kama walipata ingine maana ilikuwa siku ya msiba.

 61. Ramadhani Hayeshi

  November 23, 2013 at 4:22 am

  Ni tukio baya mno na la kusikitisha, huyu mwanaume ni wa ajabu sana na anatakiwa kusakwa ili sheria ichukue mkondo wake. po haja baadhi ya watendaji katika Jeshi la Polisi wabadilike, nimeona ile story ya mauaji ya Ilala Bungoni kuna uzembe wa Polisi walioripotiwa matukio ya domestic violence hadi yakaj tokea makubwa na yasiyosemeka.

 62. Anonymous

  January 15, 2014 at 10:28 am

  dah! inauma sana tena sana Mungu ampunzishe kwa Amani pia awape nguvu familia nzima ya akina Hamida inaniuma sana
  jamani

Leave a Reply