Uncategorized

TAMKO LA FAMILIA ILIYOKUMBWA NA MAUAJI JUZI JUMANNE UKWELI KUHUSU CHANZO CHA MAUAJI HAYO.

By  | 
Juzi jumanne asubuhi hapa Dar es salaam kulitokea tukio la kutisha la mauaji na kuliacha jiji hili la Dare es salaam na maswali mengi na kila mtu kusema lake.Tukio hilo la kutisha liliikuta familia ya Alfred  na Hellen Newa katika nyumba yao iliyopo Ilala sharif Shamba.Familia hiyo ina watoto wanne Caroline Newa,Alpha Newa,Christina Newa,na Mlowi kaka yao.
Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Gabriel Munishi (35) mkazi wa kitangiri Mwaza alifika katika nyumba hiyo na kufanya mauaji na kujeruhi kwa kutumia bastola
 
Wahanga wa mauaji hayo

Captain Francis Khianga Shumila raia wa Kenya na ni mume wa Caroline (amefariki)

 Alpha Alfred Newa(alifariki)
 Christina Nando Alfred Newa mpenzi wa zamani wa Gabriel(alijeruhiwa)
Hellen Newa mama yao mzazi(alijeruhiwa)
Gabriel Munishi  mkazi wa Kitangiri Mwanza mpenzi wa zamani wa Christina(alijiua baada ya kuua na kujeruhi)
 
Chanzo cha mauaji haya
Gabriel na Christina walikuwa ni wapenzi  Gabriel akiwa anaishi Mwanza maeneo ya kitangiri.Katika mapenzi hayo yalijaa ukatili na unyanyasaji ambao Christina alishindwa kuvumilia na kuamua kuachana na Gabriel.Chanzo cha haya yote ni Gabriel kutokukubali kuachwa.
Mahusiano ya kimapenzi kati ya Gabriel Munishi na Christina Newa
Wawili hawa walikuwa wapenzi lakini mapenzi yaliyojaa mateso ya hali ya juu.Gabriel alikuwa akimtesa sana Christina kwa vipigo na vitisho vya bastola kuwa atamuua.Miezi miwili iliyopita Gabriel alikuwa amemfungia Christina ndani ya nyumba akimpa vipigo na akiwa hawezi kutoka nje.Tukio ambalo ilibidi ndugu zake watoke Dar es salaam mpaka Mwanza  na kuhusisha polisi Dar es salaam na polisi Mwanza kuomba msaada ilikumtoa ndugu yao ndani ya nyumba hiyo.Baada ya kufanikiwa kumtoa wakarudi Dar es salaam na Christina kusitisha uhusiano huo.Baada ya kufanya hivyo Gabriel akawa akitoa vitisho kwake akimwambia akimuacha ataiteketeza familia yake.
Kabla ya tukio Gabriel alikuwa akibembeleza sana Christina amrudie lakini Christina alimwambia apumzike kwanza kwa miezi mitatu na akamshauri atafute psychological help.Amekuwa akimuona ni mtu wa hasira kila wakati,vipigo visivyoisha na mbaya zaidi akimtishia kumuua mara kwa mara  kitu ambacho sio cha kawaida hivyo ni bora akamuone daktari.Akishapata msaada ndio atakuwa tayari kuwa nae tena ila kwa sasa amuache kwanza.
 
Siku ya tukio miezi miwili toka christina na Gabriel kuachana
Kabla ya tukio Gabriel alikuwa akifika mara kwa mara maeneo ya nyumbani hapo.Alikuwa akifikia katika hotel ya Double M anakaa juu gorofani na kuchunguza kila kinachoendelea kwenye nyumba yao.Maana ukiwa hotelini juu unauwezo wa kuona nyumbani kwao sababu ni pembeni tu ya hotel.
Siku ya tukio Christina alikuwa akisafiri kwenda syprus.Kwenye gari alikuwa akiendesha mume wa dada yao Caroline marehemu captain Fransis Shumila,pembeni alikaa mdogo wao Alpha ambae ni marehemu.Nyuma alikuwa amekaa Christina na mama yao mzazi.Wakiwa wanatoka nyumbani walikuwa wanaenda kumdrop Alpha kazini ambae alikuwa akifanya kazi Barclays bank,Christina akamalizie shopping zake za mwisho halafu wampeleke airport.Wakiwa wanatoka getini ndio Gabriel akatokea na bastola akafyatua risasi na kufanya mauaji ya Alpha na Fransis aliyefia hospital jana kisha kuwajeruhi mama yao mzazi pamoja na Christina.Alipomaliza aliona kashaua na yeye kujiua kwa kujipiga risasi.
 
Maelezo haya ni kwa mujibu wa dada yao Caroline Newa aliyezungumza na clouds fm leo.
Malalamiko ya Caroline kwa polisi
Caroline na familia wamesikitishwa na polisi kushindwa kuwapa ushirikiano.Baada ya kupokea vitisho kutoka kwa Gabriel kuwa atawauwa na kuteketeza familia nzima waliripoti polisi.Wanasema walishafika mpaka kwa CID Ilala kumueleza juu ya vitisho vilivyotolewa na Gabriel wakaomba wapewe hata RB lakini polisi waliwaona wazushi.Matokeo yake madhara yamekuja kutokea wakati polisi walikuwa na uwezo wa kutoa msaada kabla ya hili.Pia alielezea kwa familia ya Gabriel kushindwa kuwapa ushirikiano toka mwanzo wakiwajibu hayo ni mambo yao ya kimapenzi wao hayawahusu walivyokutana hawakuwepo.
 Marehemu Alpha na mumewe na watoto katika picha enzi za uhai wake
Alpha Alfred Newa alikuwa mfanyakazi wa bank ya barclays toka 2004.Wakati mauti yanamkuta alikuwa Corporate Service Manager wa bank hiyo  na hivi ndivyo wafanyakazi wenzake walivyopewa meseji official ya maombolezo ya msiba huo mzito wa mwenzao.
Marehemu kuzikwa Goba jumamosi hii shambani kwa mama yake ameacha mume na watoto wawili mmoja wao akiwa na miezi 6 tu.
 
Pole kwa familia zote zilizokumbwa na majanga haya Mungu awape wepesi wa kupita kwenye kipindi hiki kigumu.

22 Comments

 1. Amor

  November 21, 2013 at 4:37 pm

  Hasira hasara. Mungu afariji hii familia. Jamani this is so wrong. Sio utanzania. Tukatae ukatili.

 2. Ruky

  November 21, 2013 at 5:44 pm

  JAMANI JAMANI HIVI POLIC WETU LINI WATAKUWA WANATULINDA WANACHI WAO JAMANI…YAANI NAKUMBUKA STORRY MOJA BINTI ALIKUWA ANATISHIA KUWA AWACHOMEEA NDANI NDUGU ZAKE KISA WALIKUWA WAKIMUONYA TABIA YA KULALA NJE NIKAMSHAURI AENDE POLIC ILIKUWA ARUSHA AKAENDA AKAJIBIWA RUDI MKAYAMALIZE WENYEWE NYIE NI NDUGU BASI AKAJA AKANIAMBIA RAFIKI YANGU WAKAWA HAWALALI KWARAH COZ KILASIKU VITISHO VIKUBWA NIKWAMBIA CK NYINGINE HEBU TWENDE WOTE NILIPOFIKA MAJIBU YAKAWA HAYO HAYO MI NIKAWA NAWARECORD MOJA AKANISHTUKIA HAPO KAUNTA AKAMUITA MWENZAKE KUMDOKEZA WAKARUDI KUJIFANYA ETI TUTAKUJA SIJUI NINI MI NIKAWA MKALI NIKAWAAMBIA CHOCHOTE KITAKACHO TOKEA HABARI WANAZO HAO WAKAKUBALI KWENDA KUMTIA NDANI BINTI ALIKUWA MJEURI HUYO MAMA YAKE ALAOMBA AKAE HUKO WAPUMZIKO MBONA ALIKOMA CK 3 ALIZO KAA HUKO NDANI BUT NOW WAPO OK HAKURUDIA HATA KUTAMKA TENA

 3. Anonymous

  November 22, 2013 at 4:47 am

  Pollen can jamani.

 4. Anonymous

  November 22, 2013 at 6:20 am

  Dada Dina, hivi hakuna fursa ya kulishitaki (sue) jeshi la polisi kwa uzembe? Poleni sana wafiwa.

 5. lily Z

  November 22, 2013 at 6:41 am

  Jamaniii jamaniii mwemwemeee nimeumiaje na huu msiba mbona haya mambo ni magumuuu!!!!sema tena Mungu awasimamiee na kufanya kazi yakee kwa hali ya kawaida kwa wahanga ni kuitu kikumu saaanaaa!!,,,masikini babyyy wa 6monthss ahhh!!!

 6. zena juma

  November 22, 2013 at 7:04 am

  masikini nashindwa hata kutoa comment inasikitisha, kinachoniuma kuwauwa watu wasio na hatia, hata hivyo shetani amekuja kivingine kuwa watu na familia zao. maana tumeona kwa ufoo saro sasa familia ya newa, so sad, mungu awapumzishe kwa amani

 7. Anonymous

  November 22, 2013 at 8:04 am

  ufike wakati dina muongelee jesh la polisi kwa uzembe nahuyo kamanda wao kova aambiwe tunawalea mpaka lini wameajiriwa kwa ajili yetu iweje sasa wakiambiwa kuna vitisho vya mauaji hawatilii maanani, tumeona kwaa hamida hivyohivyo, sasa kwa huyu nae mtu katoka mwanza wameambiwa polisi walitakiwa wamuweke ndani au wampeleke kituo cha mwanza kwa escot ya polisi, mi sielewi kazi yao nn sasa kama wanakua wazembe katika kazi zao, sasa ss tukimbilie wapi ikiwa wao chombo cha usalama wanatusaidii chochote

  • Anonymous

   November 25, 2013 at 6:39 pm

   ni huzuni iliyoje unafikia mtu huna pa kukimbilia na hao polisi mtu kama huyu mmeshasikia ameanza kutumia silaha ilibidi wampeleke Mirembe huo ni ugonjwa sio wivu tena, na nyie ndugu wa mume kuzarau tabia za ndugu yenu haikua haki huyu mwanaume alikua anapiga kilio cha msaada wa ugonjwa wa akili badala yake mnatoa majibu eti walopokutana hatujui sasa sijui uso wenu mnauweka wapi? hasa kwa huyo malaika wa miezi 6

 8. Anonymous

  November 22, 2013 at 8:34 am

  Pole kwa ndugu wote walofikwa na msiba …mwenyez mungu awape wepes ktk kipind chote cha msiba ….

 9. Anonymous

  November 22, 2013 at 8:37 am

  Pole kwa ndugu walofikwa na msiba

 10. Anonymous

  November 22, 2013 at 8:48 am

  So sorry kwa familia ya Newa na ndugu wote wa karibu. I cant imagine the pain.

 11. Anonymous

  November 22, 2013 at 11:38 am

  polisi wanachojua ni kupiga vyama vya upinzani na waandamanaji but sio usalama wa raia.

 12. Anonymous

  November 22, 2013 at 12:56 pm

  Dina kwa kweli inauma cna tena cna.Nampa pole huyo dd kwa kufiwa na mume wake na familia yote kwa ujumla. Na nyie waandishi wa habar msipend kutoa habari kabla ya uchunguz kukamilika. Wapumzike kwa amani amen!

 13. Anonymous

  November 22, 2013 at 1:38 pm

  Mungu awatie nguvu familia na mliojeruhiwa. Polen cna.

 14. Anonymous

  November 22, 2013 at 8:02 pm

  dina jeshi la police ni ovyoo kabisa mimi niliwahi kwe da buguruni nikaonana na ci na kumweleza kuawatu wata kuja tarehe fulani kunifanyia fujo aka sema wee nenda walipo kuja nik mpigia cm huyo cid wa buguruni aaka nielekeza niende tabata yule watabata aka nijibu nipo biz nije kesho saa tano wale watu walinidanyia.fujo nika wa mnyonge.sana kesho yake ukweli walikamatwa lakini walipo fika yul mpelelezi wa.buguruni alikua amesha hongwa na kuambia kesi yoote ika nigeukia mie na kumbiw ndiye niliye leta fujooo sana niliumia sana waalifu wana peta na kunitishia mpka leo jeshi l police limeoza sana rushwa ipo isiku na mchana a uonevu mkuuu na.kubambikiwa kesi

 15. Anonymous

  November 25, 2013 at 3:58 pm

  Poleni familia ya Newa.

 16. Anonymous

  November 25, 2013 at 6:43 pm

  Inauma sana mhh ushauri wangu Christina uolewe na mume wa Alpha mtunze watoto wenu, wananitia uchungu hao watoto hapo sijui akiolewa mama mwingine mambo ya mama wa kambo mhh shemeji muoe Christina atunze watoto wake mungu awape nguvu muwalee hao viumbe

 17. Anonymous

  November 26, 2013 at 9:22 am

  Poleni sana jamani.

 18. Anonymous

  November 28, 2013 at 7:26 am

  Hiyo familia waende mahakamani wakafungue mashtaka kuwashitaki wote waliozembea mpaka mauaji yakatokea, labda itasaidia kuwafanya polisi wawajibike maana bila hivyo hali haitabadilika.

  Kingine tuacheni mambo ya vicheni party nini sijui namna gani ya kumfurahisha mwanaume tuanzishe kampeni maalum itakayosaidia na kupunguza unyanyasaji dhidi ya wanawake, wanawake wafundishwe kuzijua dalili za mwanaume abuser na jinsi ya kukwepa abusive relationship, tuache kujidanganya eti nitamrekebisha tabia mwanaume.

 19. Anonymous

  November 28, 2013 at 2:03 pm

  Inatisha kweli!! kwa kweli dunia imekwisha. Binadamu tumrudie Mungu. La sivyo makubwa zaidi yaja. Mungu awarehemu wote aliokufa katika tukio hili. Shetani tusimruhusu atutawale jamani, cyo polisi wala raia woote tu waasi. Tafakari badili tabia yako MRUDIE MUNGU WAKO.

 20. Anonymous

  December 3, 2013 at 6:59 am

  very very sad…binadamu tuna roho gani lakini???..sasa kisasi chote icho?…Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema na awatie nguvu sana wahanga…Amina

 21. Anonymous

  December 9, 2013 at 1:21 pm

  Pole kwa familia ya Newa na ndugu wote. Kwa ufupi niliwahi kuwa na mahusiano na jamaa mmoja anaetokea huko huko kwa akina huyo aliyefanya mauaji haya…jamani nilipata tabu sana kuachana nae sijui kwanini hawapendi kuachwa….. Aliwahi kutaka kunirusha kutoka ghorofa ya pili tukiwa chuoni. Thanks God baada ya kumaliza chuo nilipata kazi mkoani na sikufanya kosa nilivyofika kule tu nikakata mawasiliano kabisaaaaa. Yapata 4 years now.

Leave a Reply