Uncategorized

UNAWEZA KUWA ULIMTENDEA MTU UBAYA MIAKA YA NYUMA NA UMESAHAU LAKINI YEYE HAJASAHAU NA ANAKUWINDA KULIPIZA KISASI!!

By  | 
Kawaida yetu sisi kwenye leo tena tukimaliza tu kipindi ni lazima tukute wageni kibao waliokuja kutusalimia,kutuletea zawadi,kutueleza matatizo yao wengine wakiwa na dukuduku wanalotaka kutoa mioyoni mwao n.k
Leo mchana nimemaliza kipindi nikashuka chini lakini Gea akiwa amenitangulia kushuka.Kawaida tunaeneo huwa tunaweka viti tunapaita kijiweni hapo ndio tunakaaga na wageni wetu.
Nikamkuta Gea anaongea na mama aliyekuwa akilia kwa uchungu kilio kile cha kwikwi Gea akaniambia Dina msikilize huyu mama ana machungu yake tuone tutamsaidiaje kwenye kipindi
Mama akaanza kunisimulia kisa chake kilichonifanya nihisi naangalia movie.
(picha sio ya muhusika)
Anasema miaka 12 iliyopita aliletwa Dar es salaam akitokea kijijini kwao kuja kufanya kazi za ndani.Alifika kwenye familia ya mama na baba waliojaaliwa kupata watoto wawili mdogo kabisa akiwa na mwezi mmoja.Anasema aliishi kwa furaha akafanya kazi zake na kulea watoto huku kukiwa hakuna tatizo kati yake na mama au baba mwenye nyumba.
Baada ya mwaka na miezi kadhaa kupita mtoto mdogo alishaanza kutembea na alikuwa akimpenda mno.Yeye amejaaliwa nywele nzuri tu za asili sasa kuna kipindi ilikuwa sikukuu mama akamwambia azitie dawa zitapendeza zaidi kweli akaweka dawa na nyweli zikawa nzuri tena ndefu zaidi.
Siku zikazidi kusogea mama akaanza kumbadilikia akawa mkali anamtreat vibaya kama vile kuna kitu ambacho yeye hakijui.Kila siku mama akawa ana kisirani nae mpaka akafika mahali akamfukuza nyumbani bila sababu yoyote.
Alimfukuza akijua hajui chochote hapa Dar es salaam wala namna ya kurudi kijijini kwao na wakati anafukuzwa baba mwenye nyumba hakuwepo.
Basi akatoka hapo nyumbani akaulizia stesheni ya treni ilipo maana anakumbuka alikuja kwa treni.Kufika stesheni hakuna treni siku hiyo akabaki anashangaa shangaa hapo na kilio juu hajui pa kuelekea wakati huo ni jioni wakatokea vijana wakajifanya wanataka kumsaidia wakamchukua kumbe walikuwa wahuni wakaishia kwenda kumbaka.
Baada ya kubakwa wakamtelekeza akiwa hajiwezi ndio kuna mama akamkuta katika hali mbaya akamchukua na kumsaidia.Akakaa kwa huyo mama akatibiwa majeraha akapona lakini ikabidi apime kama ameambukizwa magonjwa na mimba pia kama amepata.
Dada wa watu akapimwa akakuta ameambukizwa H.I.V  na mimba juu.
Anasema alilia sana na yule mama kumtia moyo kuwa ndio dunia.Baada ya kukaa pale mimba ikakua akaona bora arudi tu kijijini kwao basi akarudi kijijini akakakaa huko mpaka alipojifungua.Alijifungua salama mtoto wa kike na uzuri mtoto hakuambukizwa yupo salama mpaka leo amekuwa na anasoma shule yupo darasa la tano.
Dada anasema japo anaendelea na maisha yake na kujishughulisha na shughuli za upishi amekuwa na roho mchafu wa kulipa kisasi anamsumbua.Amekuwa akiishi na mawazo mabaya ya kuua kwa miaka mingi.Tukio alilofanyiwa linamtesa sana anasema kuna wakati anasahau kama ameathirika lakini ile hali ikimjia ya kumkumbusha kuwa anaishi na virusi vya ukimwi humfanya hapo hapo aanze kwenda hedhi.
Ni mara kadhaa ameshapanga mauaji ya huyo mama na watoto wake.Yeye anaishi mkoani alishakuja Dar es salaam mara mbili na kufika mpaka kwenye hiyo nyumba.
Kuna siku alishakuja akaingia mpaka ndani watoto walikuwa wenyewe akawatazama akawasalimia kutoka atokako alikuwa amepanga kuua lakini alipowaona wale watoto na akakumbuka aliwalea roho ya imani ikamuingia akaondoka.
Siku nyingine alishapanga kuchoma hiyo nyumba moto lakini akawaza je wakifa wasio walengwa je?Kumbuka anatoka mkoani kwa lengo hilo moja kulipa kisasi.
Anasema anataka huyo mama apate pigo na yeye asikie uchungu kuvurugiwa maisha yake.Wakati mwingine anawaza ajichome sindano atoe damu yake akimuona huyo mama amchome na kumuwekea hiyo damu na yeye apate H.I.V ana mawazo mengi mabaya kiukweli.
Akisimulia hayo yote analia kwa uchungu kwa nini alimtenda vile,kwa nini alimfukuza?alimkosea nini?kwa nini asingempandisha basi akarudi kwao.Ndio sasa anamtoto lakini mtoto ipo siku atamuuliza baba yupo wapi?yeye mwenyewe japo ana afya yake haumwi ipo siku atakufa mwanae atabaki na nani?
Anasema baada ya kuteseka na hicho kitu ndio akafunga safari kuja kukiongea ili asaidiwe kimawazo au vyovyote maana amekuwa akisikiliza leo tena watu wengi wanaongea yanayowasibu.
Nikamuuliza iwapo tukimtafuta huyo mama na familia yake yupo tayari kuwaona ana kwa ana na kumueleza matokea ya tendo alilowahi kumfanyia miaka 11 iliyopita?akasema hajui.
Mimi kwa kumsikiliza nimeona huyu mama anahitaji kusamehe ili aishi kwa amani.Pia akutane ana kwa ana na huyo mama amwambie kidonda alichosababisha kwenye maisha yake.Mama akubali makosa na amuombe msamaha kwa dhati.Pia asaidiwe uponyaji wa kiroho ili aweze kusamehe na kukubali yaliyotokea kwenye maisha yake na afungue ukurasa mpya.Na ikiwezekana apewe msaada wa kisaikolojia ili akili ikae sawa.
 
Kesho utamsikia katika leo tena ya clouds fm kuanzia saa nne asubuhi na utatupa mawazo yako ili kumsaidia.
Sijaweka jina,mkoa anaoishi,nyumba aliyoifanyia kazi hapa Dar kwa sababu maalum.
 

49 Comments

 1. RUKY

  November 12, 2013 at 4:53 pm

  DAA KWELI KM MOVIE OMG..DU… NINGUMU SANA KUSAHAU HUYO MAMA SIJUI KM TZ TUNA WATAALAM WA KISAIKOLOGIA YA UHAKIKA COZ UWII LONG TIME NA ASIPOSAIDIWA HARAKA ATAFANYA ANACHOFIKIRIA KUFANYA.. KINGINE KIKUBWA NI KUFANYA IBADA ANGEKUWA NI MTU WA IBADA MBONA ANGEONA KM NI MITIHANI YA ALLAH NA ANGESHA SANEHE SIKU NYINGI ISHAALAH MOLA AMFANIE WEPESI.. ILA DINA NAHITAJI PIYA MAWAITHAH JUU YA KUSAMEHE KIISLAAM TUNAITA HIVYO AU DAWHA..DAA MUDA HUO NITAKUWA JOB I WISH NIMSIKILIZE

  • dinamariesblog

   November 12, 2013 at 5:26 pm

   tutajitahidi kwa namna itakavyowezekana,lakini kama ulivyosema imani ya dini yake na kumjua Mungu na duwa ya kumpa ujasiri na moyo wa kusamehe maana yeye ni muislam inaweza kumsaidia.

  • josefu tamaha

   November 14, 2013 at 8:25 am

   kwa kweli huyo dada kapatwa na majaribu makubwa sana,,,yaaani katika hali ya kawaida ni vigumu kusamehe ila kwa msaada wa mola ataweza kumsamehe na kusahau ,,,ila inauma sana…..POLE SANA DADA AMINA MUNGU AWE NAWE….

  • josefu tamaha

   November 14, 2013 at 8:27 am

   inauma sana ,,,,,,nampa pole sana dada amina ,,NAMUOMBER AMRUDIE MOLA WAKE NA KUMSAMEHE ,,MAANA HAPA DUNIANI WOTE TUNAPITA…

 2. Anonymous

  November 12, 2013 at 7:53 pm

  duu inasikitisha.kuna movie ya ki nigeria unaweza kuiona youtube part one inaitwa my unborn son,ina part kama 3 kama sikosei,ni true story kulikuwa na housegirl na mwenye nyumba {ame act mwenye nyumba kama oge okoye}jamani huyo mama alikuwa anamnyanyasa sana huyo house girl,alikaa muda mrefu kabla hajapata ujauzito,baadae huyo mama akapata mtoto mmoja.mume wake alikuwa anamuonya sasa kutomnyanyasa huyo dada.hela alikuwa hampi,kukatisha story huyo dada alimuomba mwenye nyumba hela akanunue msuaki,imagine akanyimwa.huyo dada akawa anatumia msuaki wa mtoto wa huyo mama{alikuwa anaishi nae vizuri}siku yule mtoto akaanza kuumwa kuchekiwa hospitalini mtoto ameathirika wakapimwa nyumba nzima ikaonekana dada wa kazi na mlinzi wameathirika,dada wa kazi alitembea na mlinzi baada ya kumuomba hela{huyo dada alikuwa anauguliwa na mama yake}mwisho wa muvi huyo mama alilia sana maana mtoto mwenyewe alikuwa huyo huyo

 3. Cymah Wandelt

  November 12, 2013 at 9:39 pm

  Dah maskini, inauma sana. Kweli huyo dada anahitaji maombi na kusamehe, inauma sana mtu kukutenda unyama na juu yake ukaanza kuishi kwa matumaini. Mungu amsaidie dada yetu apate kusamehe nakusahau, japo ni vigumu ukiangalia mtoo ukajumlisha na maradhi. Msaidieni apate msaada wa mawazo, anti Sadaka nawengine. Kweli wakati unalia shida geuka nyuma uangalie uliowazidi raha, yaani unacholia shida kuna wanaokiona ni raha. Mungu wa rehema ampe moyo wa kusamehe na kusahau ndugu yetu. Amen

 4. Anonymous

  November 13, 2013 at 5:07 am

  Ni kweli huyo Mama amemuachia jeraha kali sana katika maisha yake na kama anavyosema anahitajika huyo Mama ili kumsikiliza, kwa sababu hatujui kwann alitenda hayo na sababu ipo. Kwakumsikiliza itanfanya huyo dada kuwa na uwepesi wa kusamehe…then hatua ya Msamaha inaweza kufuata..vp atamsamehe, hatua gani atachukua..hapo sasa Imani mbalimbali na pia watu wa kisaikologia wanaweza kumsaidia na pia kumuombea kwa Mungu apate uponyaji wa ndanikabisa.. maana tukio lake ni langu pia.

 5. Anonymous

  November 13, 2013 at 5:15 am

  Inasikitisha sana huyu mama ni lzm amtafute amuelezee aweze kuomba msamaha kama ni muelewa

 6. Anonymous

  November 13, 2013 at 6:29 am

  Duh!! very touching story!! inasikitisha sana masikini MUNGU ampe nguvu na moyo wa kusamehe huyo mama aone ni mitihani tu ya Dunia ajikabidhi mikononi mwa MUNGU japo inauma lakini aone imeshatokea, kwa kweli anahitaji ushauri wa kisaikolojia masikini.

 7. Anonymous

  November 13, 2013 at 7:44 am

  inasikitisha sana haya mambo yapo sana tu unamtendea mtu jambo bila kujua matokeo yake ndo hayo!huyo mama amsamehe tu ili apone!

 8. Anonymous

  November 13, 2013 at 7:46 am

  Kwanini waajiri wengine hawatumiagi akili, yeyote anaekusaidia kulea watoto wako anatiwa kuheshimiwa na kama umemcchoka mtu fata taratibu ulizo tumia kumpata ili umrudishe salama! nafeel maumivu ya huyu dada, na inauma mara mbili anapokumbuka mwanae, kuwa je nikifa mwanangu atabaki na nani?? nataka huyu mama aliemfukuza ashitakiwe! yes ashitakiwe! namtakia huyu dada mema, Mungu amlinde amuokeo na amuondolee roho ya kuua na kulipiza kisasi, amuachie mungu maana yeye ndie Jaji mkuu, malipo ni hapa duniani. Pia namatakia masomo mema mwanae, mungu awatangulie maisha yao yote. inauma sana!

 9. Anonymous

  November 13, 2013 at 7:53 am

  Nimejikuta nalia dina, yani mm nimwanamke nimwjifeel km nimm nimefanyiwa hy mama anahitaji na macouseler pia watumushi wamungu wamjenge kiimani,natamani kumuona hy mama. Nina kisa changu dina jp hakufanani nahicho ila natamani kushare na watu.

 10. Anonymous

  November 13, 2013 at 9:16 am

  Oh! Am speechless….uchungu ulopitiliza aisee…mpk nimelianae dah!

 11. tony24

  November 13, 2013 at 9:57 am

  pole sana dada binadamu ujafa hujaumbika kwahiyo omba mungu wewe kama kakuadhibu dnian yeye ataadhibiwa biguni

 12. tony24

  November 13, 2013 at 9:58 am

  pole kama kakuadhibu dunian bac na yeye ataadhibiwa biguni

 13. Anonymous

  November 13, 2013 at 10:17 am

  Da Dina nimesikiliza stori ya huyo dada kwa kweli kwanza nawapongeza sana kwakuwa mnajua wajibu wenu pili huyo dada mimi namshauri akubali mmtafute huyo mama waje hapo waombane msamaha pili dada iungie kwenye mambo ya ibada aokoke na ukimwi utaisha wala hata ouna tena yawezekana kwa sababu ameweka kifungu za kulipiza kisasi moyoni ndo mana hajapona ila akisamehe tu na ukimwi utatoweka…….ila tunaomba kumuona kwenye Blog yako plz!!!

 14. Anonymous

  November 13, 2013 at 10:21 am

  Dina huyo dada amenisikitisha sana mungu amsaidie atoke ktk hayo maumivu.ila liwe funzo jamani kwetu sisi wengine mabinti wa kazi ni sawa na watoto wetu tuwasidie wakitushinda tufuate taratibu nzuri kuwaondoa.maana huyu ni mmoja lkn wapo wengi wameumia na hawajapata mahali pa kusemea tubadilike. huyu mama mtuhumiwa hii ni aibu kubwa sna sidhani kama alijua baada ya miaka yote hiyo huyo dada atarudi. TUWE NA HOFU YA MUNGU KILA MTU KWA IMANI YAKE .HONGERA SANA DINA KUTUFUNGUA MACHO

 15. Anonymous

  November 13, 2013 at 10:23 am

  Dah nimebahatika kumsikiliza huyu dada japo nipo kazini lakini kasimu kangu katorch kamenisaidia kwakweli. Kiufupi huyo dada/mama alikosa ushauri mapema kulingana na hali ilivyokuwa haikuwa rahisi kupata ushauri. Councelling ni tiba muhimu sana. Najitolea mfano mwenyewe mwaka jana mwezi july niligundulika nina HIV lakini ushauri niliopewa kwa kweli sikutetereka japo nilipata hofu lakini kadri siku zinavyoenda naona kawaida. Kama sasa hivi nimenenepa nina kilo nyingi ambazo sijawahi kuzifikia na ninatumia ARVs zangu vizuri tu. Kama alivyosema Zamaradi tukisimama nae yeye ndio atanyoshewa kidole kuwa mwathirika. Sitaki kuleta hadithi yangu hapa ila ni kutaka kumfungulia njia huyo dada kwamba ajikubali,na kuhusu hicho kisasi asamehe. Huyo mama alomfukuza wala hakutegemea kama kitendo chake cha kumfukuza kwake angepata hayo madhara.Ukiangalia haraka haraka huyo mama alipata hofu huenda huyo dada angeingilia ndoa yake ni kukosa kujiamini in short.
  Kitu kingine Dina jamani siwafundushi kazi ila inapotokea habari kama ya huyu dada kwa kweli wasikilizaji huwa hatutamani akatishwe mfano matangazo au mziki. Any way kwa upande wa matangazo tunajua ni lazima yawepo manake ndio yanaendesha kipindi na radio kwa ujumla. Lakini kama hakuna ulazima msipige hata mziki mbona vipindi vipo vingi tu!!.Najua utacheka Dina.
  Kama mlivyokatisha leo tena leo mchana na B12 kaingia na mbwembwe zake za studio mpya yaani mmetuacha njiapanda hamjatuaga lakini naamini mtakuwa nae tena kesho au siku nyingine.
  Nawapenda sana Team LeoTena.

 16. Anonymous

  November 13, 2013 at 11:12 am

  Nimemsikiliza, na kwakweli inauma sanaa, na nimetokwa na machozi… Maskini anafikiri kwa kuua ndio atapona majeraha yake lkn kumbe ndio anazidisha kuongeza jeraha. Hata mm ningewaza hayohayo na labda nisingejali wengine ikiwa watadhurika au la Tatizo linakuja kuwa kwa kuua, jeraha linaongezeka na sio linapungua. Kinachohitajika ni kupona kwa jeraha la ndani kabisa na kuweza kutoa msamaha. Namuombea kwa Mungu aweze kupata nguvu na moyo wa Msamaha, na msamaha hauwezi kumalizika kwa siku moja bali ni hatua… Courage..!!!

 17. Anonymous

  November 13, 2013 at 2:02 pm

  duh yanai nimejikuta machozi yanafunika macho tu aiseee, dunia ina mapito hii jamani uwiiiiii, ee MUNGU amsaidie jamani

 18. Anonymous

  November 13, 2013 at 6:04 pm

  Hi Dina
  Nimesikiliza kipindi vizuri ila huyo mama alichomfanyia huyo dada si kizuri kwann asimrudishe kwa usalama na alikomchukua coz haya yote yasingempata may be,lkn kwa vile alimuacha yakampata cha kumuomba ni Mwenyezi mung amsaidie awe na roho ya imani na huruma kama hiyo inayompata coz km alifika mara mbil hapo nyumban kwa huyo mama na nafsi na roho inamsuta kufanya ubaya basi akiombewa na kuelimishwa zaidi anaweza kusamehe na huyo mama aitwe amuombe msamaha huyo dada.Mtihani atakaobak nao ni kuhusu mwanae jaman na watoto wa siku hizi wanavyojua kudai baba zao atamwambia nini ili amuelewe?mie namtakia kila la kheri aishi kwa amani na aendelee kumsomesha mwanae natumaini mungu atamfungulia baraka zingine amsamehe huyo mama saba mara sabini.Jaman kina mama tuache ukatili maisha haya mpaka lini tunawatesa wadada wa kazi heri kama umemchoka fuata taratibu za ulivyomchukua arud kwao kuliko kuwapa manyanyaso tukumbuke nao ni binadamu kama sisi na pia wanapata maumivu

 19. Anonymous

  November 14, 2013 at 4:38 am

  Nashauri mwende nae kwa huyo mama aliyekuwa akimfanyia kaz, na watu wazima wenye busara akamueleze yote waombane msamaha ili yaishe. Kwakwel imeniuma sana mpaka nimelia.

 20. Margareth Mkini

  November 14, 2013 at 7:22 am

  Nampa huyo dada pole kwa magumu aliyopata,namshauri asilipize kisasi aende tu akamshitaki ili akamatwe na kushitakiwa kuliko kulipiza kisasi najua inauma lakini hakuna jinsi,

 21. sarafina

  November 14, 2013 at 8:56 am

  Pole ndugu! inauma sana, kwa ayo uliopitia, ' usilipize kisasi iyo si kazi yako wewe' Mungu anamakusudi yake ndiyo maana umeshindwa kutumia izo nafasi za kufanya mauaji, muachie God.

 22. esther nyalusi

  November 14, 2013 at 9:07 am

  Kwakweli da Dina inabidi muwakutanishe ili yeye dada Amina amuelezee huyo mama alichonacho moyoni ili huyo mama amwombe msamaha maana yeye usikute ajui kama kitendo alichomfanyia huyo dada aliumia kiasi gani,tujifunze kuomba msamaha na tuwe tunaangalia mambo tunayoyafanya maana tunaweza kuchukulia poa kumbe linamuumiza mwenzio

 23. Anonymous

  November 14, 2013 at 9:27 am

  inasikitisha sana mungu yupo huyo mama amuombe msamaha inawezekana kwa kukiri kwake huyo dada atamsamehe

 24. Glory

  November 14, 2013 at 10:05 am

  Masikini dada wa watu, ataokokaje sasa na hiyo roho inayosukuma kulipa kisasi dina?
  Silia dina, kubwa zaidi ni kuwakutanisha wakishaonana akatoa yake ya moyoni atakuwa amepunguza uzito wa huo mzigo alobeba kwa miaka mimgi na ndipo ataweza kuamua maamuzi mengine bila hivyo kisasi hicho hakitaisha mpaka anaingia kaburini… KIUKWELI KUSAMEHE NI NGUMU kwa case kama hii ila akipata pia akipata washauri wazuri kama kina sadaka itasaidia sana. Japo kpnd kimenipta.

 25. Anonymous

  November 14, 2013 at 10:10 am

  Nimesoma na kuisikiliza yaliyomkuta huyu dada, inasikitisha. Mungu amuongoze na ajifunue kwake wakati anasamehe, huu ni muda wake wa uponyaji wake wa ndani. God's time is the best…!
  Dina jiulize kwanini watu wanakufuata na matatizo, liangalie hili kiroho, kwanini mioyo yao inaamini wewe na wenzio utawasaidia, nadhani Mungu anazungumza na wewe kitu (Tafakari hili zaidi na Mungu akusaidie) I think this is why the almighty brought you in this earth, kusaidia wanyonge. Mungu akuongoze, akupe busara akupiganie wakati unatekeleze kusudi lake duniani.

 26. Anonymous

  November 14, 2013 at 10:19 am

  MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI JAMANI, MNASEMA ASHTAKIWE, AFWATWE N.K.. LAKINI HAMJUI MAISHA ANAYOISHI SASA!! INAWEZEKANA YUPO KWENYE WAKATI MGUMU ANATAMANI AFE, KILA ANACHOJARIBU WAPI, MUME NDANI KASHESHE.. MAJUNGU HUKO NJE NA WENZIE.. OFISINI HAPAKALIKI.. ANAJIULIZA HIVI NIMEMKOSEA NINI MUNGU! KUMBE NI ROHO YA HUYU DADA BADO INAWEWESEKA NA MACHUNGU YOTE.. MUNGU KESHA MUONYESHA HABARI YAKE.. KILICHOBAKI NI AWEKWE JINA TU JAMII IMFAHAMU!

 27. Anonymous

  November 14, 2013 at 11:24 am

  jana nilisikia hii story na chozi lilinitoka leo sijapata mda wa kusikia mwisho wake. mpeleken kwa aunt sadaka amsaidie kutoa hiko kisasi. inasikitisha sana na inaumiza kwa kweli

 28. Anonymous

  November 14, 2013 at 2:14 pm

  dina loh sina hamu naanza kufikiri nilio waudhi niwaombe msamaha.kiukweli wadada wengi wa kazi wana pata mabaya mengi pia wana mabaya mengi wanayo fanaya ndanii ya nyumba .huyu mama hakutumia akili nge mrudisha kwa huyo dada .pamoja namsamaha . huyo mama anahitajika kusaidiwa kiroho sana mpak akae sawa loh ila sikia kwa.mwenzako sio kwako pia ni vyema mk mwita nayule mama aliye msaidia.baax ya kubakwa kazi ipoo.
  dina sikuhizi blog in boa hauchang mki.kma zmani upo shule au umekua biz sana badilika mwli wadau tun penda kila wakati tukut jambo jipya au hata kama hamna weka heka heka kila siku maa twazipend

 29. flora

  November 14, 2013 at 6:26 pm

  Mi naomba kama kuna uwezekano dina umkutanishe tu na huyo mama na amwombe msamaha wa dhati na amsaidie kimaisha kwa kweli du inauma km muvi vile .

 30. Anonymous

  November 15, 2013 at 8:20 am

  jamani nimejifunza kuwa na subira unapokuwa na matatizo. nina yangu yananikwaza ila nilipomsikia huyo dada niliomba msamaha kwa allah kwa kulalamikia sana mattz yangu. kumbe kuna wenye mattz zaidi yng.

  wanawake tubadilike wengi wetu tuna roho mbaya mno. na kinachonishangaza zaidi ni kuumizana wenyewe. mama anamnyanyasa dada wa kazi na kusahau ndio mlezi, mwalimu, daktari, mlinzi wa watoto wake. mwanamke anatembea na mume wa mwenzie na kutamba kuwa anamkomoa. ukizalishwa na mwanamke hosp unaweza ukapigwa na kutukanwa pia. tukiolewa na tukikuta watoto wa wanawake wenzetu watajuta. mungu atusaidie tuoneane imani ndg zng. dunia tunapita na tutaulizwa na allah wajibu wetu tulivyotimiza kama mama, dada, bosi, mwalimu, nesi n.k

  ushauri kwa dada aswali swaka tano akiwa busy na swala hayo mawazo yataondoka taratibu na aombe kwa dhati. ktk dini yetu wanasema hakuna maombi na dua nzuri kama ya kujiombea mwenyewe kuliko kwenda kuombewa na mtu. coz ww ndio unajua maumivu na nini unahitj kwa allah. kingine ataje majina ya allah kila sekunde iwe ndio routine yake. mie nina mtihani wa malezi dah kwa njia hii naona allah anavyonitendea miujiza. inshaallah mungu atamfanyia wepesi kwa kila kilicho na kheir. awaone masheikh watamuelekeza zaid namna nzuri ya kuishi kiislamu. Da J

 31. Anonymous

  November 15, 2013 at 8:50 am

  dada dina asante sana kwa story zako nyingi tunajifunza sana na kama hiyo ya hamida atofautiani na maisha ambayo nimeyapitia mimi namshukuru mungu mimi niliwahi kuondoka na mungu ameninusuru sana kwa kweli inasikitisha sana

 32. Anonymous

  November 15, 2013 at 9:37 am

  Dina i see poleni maana me nicngeweza kuisikiliza hiyo hadithi yote bila kulia sana! mpe pole huyo dada! hujafa hujaumbika! maisha yana mambo mengi sana ndio maana huwa nikimkuta mtu analia eti watu wanamsema huwa nashangaa sana zaidi huwa namwambia mhusika usipende kulia kwa ajili ya mambo madogomadogo maana maisha yana mambo mengi sana kuna mengine ni magumu, makubwa hata ukitaka kulia machozi hayatoki ukitaka kucheka kicheko hakiji. Tuangalia hali ya huyo dada na mambo aliyopitia tena katika umri mdogo kabisa kwani naamini miaka 11 iliyopta alikuwa mdogo sana. suala ni kumtia moyo, kumuombea na kumuonyesha upendo kwa kumpa msaada wa karibu kuweza kumfanya aweze kusamehe na kuendelea na maisha akiwa na amani na furaha. Dina suala la kuwaita hiyo familia hasa huyo mama na kumueleza alichokifanya kimeleta athari kiasi gani katika maisha ya huyo dada ili kuweza kuleta suluhu baina yake na huyo dada,
  lakini zaidi hata na wengine wenye tabia za aina hiyo kuwasaidia wajirekebishe na kuacha tabia hizo.
  Mwisho mwambie huyo dada kila kitu Mungu huwa anaruhusu kwa sababu ebu ajipe nafasi aingie faragha na Mungu wake naamini Mungu ni mwema na mwenye rehema atamuonyesha kusudi lake juu ya hayo yote aliyopitia, tena akiweza amuulize ehe haya nimeshayapitia na matokeo ni haya then what God! nifanye nn? sikio la Mungu likaribu atasikia alafu atamshangaa Mungu atakavyojibu yote kwa wakati wake. Naamini Mungu ana kusudi katika hilo ajipe nafasi sisi wakristo tunaamini au tumefundishwa kisasi ni cha Mungu, ajifunze kujisamehe na kusamehe wengine hizo roho za kisasi zitaenda zake. Mama Washington

  • Anonymous

   November 18, 2013 at 7:57 am

   mdau umeongea vitu ambavyo nilikuwa nawaza kwa kweli umempa ushauri mzuri sana yp majaribu ni mengi ktk maisha sometimes mpk majaribu mengine unaweza mlaumu mungu y mimi lkn hkn jaribu lisilo na majibu au lisilo na kwa nn ni kuzidi kusl na kumuomba mungu na mungu mwenyewe atajua jinsi ya kuwafanya binadam waliokutenda hvyo wewe ni kusamehe kumuomba mungu akupe maisha marefu ya kueza kulea mtt wako na upt faraja hp bdaye

 33. Anonymous

  November 16, 2013 at 9:12 am

  Da inauma lkn mumgu anamakusudio yake

 34. Anonymous

  November 16, 2013 at 9:14 am

  Dah inaumasana mungu atamsaidia

 35. Anonymous

  November 16, 2013 at 11:19 am

  Inasikitisha sana sana,huyo mama alimtimua huyo dada sababu ya kutokujiakimi na hakufikiria nn kingetokea mbele ,labda hasira zilimtawala. Tunaomba muwakutanishe Mama aelewe nn kiliendelea baada ya kumfukuza dada na aweze kuomba msamaha.

 36. Anonymous

  November 18, 2013 at 4:12 pm

  Iyo story ya kweli? Au niyakutengeneza ili kipindi kiendelee..!

 37. Anonymous

  November 18, 2013 at 4:15 pm

  IYO STORY YA KUTENGENEZA,How sure are we kama ni kweli yaliyompata huyo dada,please dina prove to us sio story ya kutengeneza ili kipindi kivutie siku ziende.

  • dinamariesblog

   November 21, 2013 at 7:50 am

   My dear kama hayajawahi kukukuta wewe au yoyote anaekuhusu utahisi ni story ya kutengeneza.Na uendelea kuomba Mungu akuepushe na akulinde lakini kama bado unaishi mengi utayaona.Naleta hadithi za maisha ya watu hapa ili tujifunze sasa kama utahisi ya kutunga mwenzangu bado hujayana ya dunia!

 38. Anonymous

  November 19, 2013 at 8:47 am

  tuko wengi tumepitia vipindi vingumu jamani mioyo imejaa vidonda sijui nani wa kutuganga kama mchangiaji mmoja alivyosema kulia na kucheka wakati mwingine vyote vinakuwa vigum kwa maumivu, mungu tusaidie wahanga, ila maumivu ni makali.

 39. Anonymous

  November 19, 2013 at 12:34 pm

  So sad… imagine siku aliyoenda kuwaua wale watoto angefanikiwa ingekuwaje? Kwa kweli sisi wazazi tunafanya mambo ambayo yanawagharimu watoto wetu kiasi kikubwa namna hii. Pole za dhati kwa huyo dada. maisha bado yapo na akiweza kutulia na kuacha kuwaza ya nyuma atapata faraja kubwa na kuendelea na maisha yake mapya. hata hivyo nashauri mkiweza mumkutanishe na yule mama, naamini huyo mama aliyekuwa muajiri wake hajui kinachomsibu huyo dada mpaka sasa. Kukutanishwa huko kuwe na nia ya kumpa huyo aliyekuwa mwajiri wake mrejesho wa kile ambacho yeye hakuona shida kumfanyia huyo dada kimeleta madhara kiasi gani kwa mtu aliyemtunzia wanae kwa muda mrefu. She will pay back…hata kwa machozi na sikitiko la dhati inatosha, ingawa nia yangu kubwa ni huyo mwajiri kupata feedback. Pia kwa kukutanishwa kwake ikibidi mumewe awepo manake nina uhakika mumewe atakuwa hakuelezwa ukweli kuhusu kuondoka kwa huyo dada. Tahadhari ichukuliwe ili hilo jambo lisije kuleta madhara zaidi kwa hiyo familia! Kila la kheri Dina.

 40. Anonymous

  November 20, 2013 at 1:05 pm

  Dina, hii story niliisikiliza katika LT, nakumbuka ulisema mtakwenda kwa huyo mama muwakutanishe, sijasikia tena nini kiliendelea je mlikwenda au ilikuwaje, hetu tujulishe hata hapa kwenye blog yako, ilikuwaje?

  • dinamariesblog

   November 21, 2013 at 7:51 am

   Ntawaelezea itakavyokuwa bado tupo kwenye process

 41. Anonymous

  November 21, 2013 at 11:54 am

  Huyo annony hapo juu ana matatizo gani cjui. Anavyosema ya kutunga ana maana gani hayajamkuta ndiyo maana anasema ni ya kutunga. Hujafa hujaumbika ndugu watch out of what you are speaking!

 42. Anonymous

  December 6, 2013 at 10:19 pm

  Dina for the sake of the kids, naomba umkutanishe na huyo mama na naomba umwambie asije ua hao watoto jamani hawana makosa yoyote yeye are deal na huyo mama sio watoto. mimi hii story imeniuma sana ila asifanye chochote kwa watoto jamani. I love kids uwiii

 43. Dinna Kaiza

  January 24, 2014 at 9:03 pm

  ki ukweli hii habari imenitoa machozi mpaka sielewi hata cha kuwaza najaribu kujiweka ktk nafasi ya huyo mama nashindwa kupata majibu ingekuwamimi ningefanya nini inaumiza sana namuomba Mungu nisiwe mama wa aina hiyo aliyefanya kitendo hicho cha kumfukuza mtoto wa watu bila kujua madhara na hatari zitakazo mpata MUNGU Amsaidie Amina aweze kuwa ktk hali yake ya kawaida japo si rahisi.

Leave a Reply