Uncategorized

WASEMAVYO MARAFIKI ZANGU WA FACEBOOK:MASANJA MKANDAMIZAJI

By  | 
Masanja Mkandamizaji ni mchekeshaji wa Original Komedi ambae naamini watanzania wengi tunamjua.Kwenye mitandao ya kijamii kama facebook,twitter huwa haachi kunivunja mbavu wa post zake anazoweka kila siku ambazo marafiki zake huko tunaweza kusoma na kulike au kucomment.
Leo aliandika hii ambayo nilicheka kweli nikasema ngoja nikuwekee na wewe.
 
Kwa dada zangu wote wa kizazi hiki chetu: Sababu zinazoweza kukufanya ukose mchumba ukabaki singo muda mrefu au maisha yote huku unalialia:

1. Kutokuwa na hofu ya Mungu. Binti huenda kanisani wala msikitini upo tu nyumbani. Mvulana serious akikuangalia ataona ni mtu wa kutumika tu na si mtu unayeweza kulea watoto katika misingi ya maana na kuwa muhimili wa familia.

2. Masaa 24 wewe uko kwenye simu na TV. Ukitoka channel hii unahamia ile. Tamthilia zote unazijua wewe. Hebu niambie kichwa chako kitakuwa kimejaa nini zaidi ya mapenzi ya Kifilipino na Kimeksiko ya kwenye hizo tamthlia?…

 
3. Hutaki kufanya majukumu ya msingi ya kike kama kupika na kuosha vyombo, kisa TV na sinema zimekuonyesha kuwa hayo pia ni majukumu ya wanaume. Hii ni Afrika mama, utaumia. Unaenda kwa mpenzi wako kumtembelea vyombo unakuta vichafu huoshi, unakaa tu. Unajishushia pointsi. Osha na mwambie si vizuri kuacha vyombo vichafu.!

4. Kuwa mtumwa wa kila kitu kipya. Mtu gani atapenda kuwa na mwanamke ambaye ni mtumwa wa kila aina mpya ya simu, kila aina mpya ya kiatu, kila aina mpya ya nguo, kila saluni mpya anataka kwenda?

5. Kutumia vipodozi hadi unapitiliza. Badala ya kuvutia unatisha!

6. Muda mwingi kutumia kwenye mitandao. Mara Twitter, Mara Facebook, mara Instagram! Wataalam wanasema binadamu ana uwezo wa kuwa na marafiki si chini ya 150 tu. Lakini wewe kila mtandao una watu 2,000! Sasa hivi unaweza kuona haina maana ila ngoja ufike miaka 35 ukiwa single and searching ndo utaelewa.

 
7. Acha kutoa namba yako kwa kila mwanaume! Hakuna mwanaume ambaye anataka kuwa na mwanamke ambaye kila muda anawasiliana na watu hata wasioeleweka.

8. Jipe thamani na ongeza thamani kwenye maisha ya mpenzi wako. Kama uko shule soma, kama unafanya kazi fanya vizuri, kama una biashara jitume na kila mara mshauri vizuri mpenzi wako. Hakuna mwanaume anataka kukaa na mwanamke ambaye yupo yupo tu!

9. Acha tabia ya kila saa kuruhusu marafiki zako kuongoza maisha yako. Kuwa na misimamo yako.

10. Kutembea tembea na makundi ya wasichana wenzako kila mahali. Kwani lazima? Huwezi kutembea mwenyewe? Inawezekana kabisa katika kundi la wasichana wenzako yuko ambaye ana tabia za ajabu na mwanaume akimuona tu na wewe atakuhukumu kwa kuwa mko kundi moja. Sio muda wote ni muda wa kutembea na kundi la marafiki.

Naachia hapa kwa leo.

18 Comments

 1. emu-three

  November 13, 2013 at 7:48 am

  Mmm, unasema ?

  • Anonymous

   November 17, 2013 at 3:33 pm

   kuna ukweli wa maneno yake lakini mkumbuke kuolewa sio ajira kaka yangu ndoa ni masikilizano na mapenzi ingekua sio hivyo basi huko vijijini kungekua hakuna single laday wote wangekua wameolewa maana wanawake wa vijijini mtindo wa maisha ni wa mikiki saa yote haya nisianzishe debate bure haya atuwekee na wanaume nao maana kuna wanaume hawana point ni zero kabisa muwarekebishe na wao msikalie kutuchamba wanawake kila siku hata nyie wanaume mna yenu mengi tu yanayokera

 2. Anonymous

  November 13, 2013 at 7:49 am

  Ni kama ucheshi but it is very true..

 3. Anonymous

  November 13, 2013 at 11:14 am

  MASANJA KAFUNIKA,UJUMBE MZURI MNO

 4. Anonymous

  November 13, 2013 at 8:16 pm

  Masanja kaongea kweli tupu. Ila mimi sapo Namshukuru Mungu.

 5. Ruky

  November 14, 2013 at 7:04 pm

  DUUU YANACHEKESHA NA YANAUKWELI USIPOZINDUKA KWA HAYA MAANDIKO BC TENA

 6. Ruky

  November 14, 2013 at 7:05 pm

  DUUU YANACHEKESHA NA YANAUKWELI USIPOZINDUKA KWA HAYA MAANDIKO BC TENA

 7. Anonymous

  November 15, 2013 at 12:05 pm

  Ingekuwa ivyo dina ungekuwa wa kwanza kuolewa iyo ilikuwa zamani

 8. Anonymous

  November 17, 2013 at 1:47 am

  maneno yake yana ukweli,ila nasikia na yeye ni mtu wa totos,na ana utapeli wa mapenzi

 9. Judy

  November 17, 2013 at 6:14 pm

  Nimemuelewa sana pastor huyu. Asante kwa kushare uku.

 10. Anonymous

  November 18, 2013 at 5:59 am

  MASANJA YUPO JUU…..NI KWELI KABISA NA YAMENIGUSAAA SANA!!! NITAYAFANYIA KAZI…ASANTE MASANJA KWA USHAURI MZURI….NI FUNDISHO TOSHA KWA SS WASICHANA WA KILEO, INABIDI TUJIREKEBISHE KWA KWELI

 11. esther nyalusi

  November 18, 2013 at 9:19 am

  Kaaaa tunacheka but yanaukweli ndani yake

 12. Anonymous

  November 18, 2013 at 10:34 am

  hahaaa masanja! mbona mie pmj na kufanya yote hayo mazuri na kuyaepuka hayo mabaya sijaolewa hadi sasa jmn?

 13. Anonymous

  November 18, 2013 at 11:57 am

  Ukweli mtupu live bila chenga.

 14. Anonymous

  November 19, 2013 at 7:36 pm

  Safi nmepata k2 hapo.

 15. Anonymous

  November 21, 2013 at 8:21 pm

  Na wewe mbona unakaa kisela tu si uoe tukuone jinsi unavyotunza ndoa na familia.kazi kuwachamba wadada tu kwa nini wewe umeshindwa kuoa, au kwa sababu umejenga vibanda na magari ndo umakini wako ulipo zaidi?

 16. Elia Kihoyo

  November 25, 2013 at 8:07 am

  mh!!!

 17. Elia Kihoyo

  November 25, 2013 at 8:08 am

  mh!!!

Leave a Reply