Uncategorized

WEMA WANGU UMENIPONZA!

By  | 
Habari za siku nyingi,humu ndani sijui kuna kimtu kilipita kikachokonoa maana kwa muda nilikuwa najaribu kuingia siwezi.Ilianza nikiupload inakuja post moja tu zingine hazionekani ghafla nikawa siwezi kabisa kuingia.Kwa msaada wa kaka anaitwa Clement ndio leo nimeweza kuingia tena.Na leo tuna email kutoka kwa mdau hapo anadai wema wake umemponza.
 
Hi Dina,
Nimetafuta email yako hadi nimeipata unisaidie kwa haya yaliyonikuta.
Kwa kifupi ilikuwa siku ya ijumaa juzi tar. 25/10 nilipita bar moja pale Tegeta inaitwa ZERO PUB kupata moja baridi kabla sijaenda home, si unajua tena weekend sio mbaya kufanya hivyo? Mara nyingi nakuwa na jamaa zangu wawili lakini siku hiyo nilikuwa na kazi nyingi ofisini kwahiyo walitangulia na nikawapita maeneo ya mbezi mimi nikaendelea hadi maeneo ya home Tegeta.
Basi nikakaa kaunta na kuagiza kinywaji changu. Ikaja gari aina ya Landcruser GX ya zamani kidogo, sikujua kulikuwa na watu wangapi sababu niliona hainihusu lakini niliangalia sababu alikuwa anapaki nyuma ya gari langu, akashuka mzungu mmoja na kuja hadi pale kaunta. Akamsemesha yule dada wa kaunta na alikuwa anataka chupa ya Grants. Yule dada hakujua kizungu ila alielewa na kwenda kuleta hiyo Grants. Lakini mkononi yule mzungu akawa ameshika sh. 20,000 na yule dada akamwambia inauzwa 48,000/=. Yule mzungu akawa anajaribu kumwambia yule dada kuwa hana TSH kwa hiyo anaweza kulipa kwa dola? yule dada akawa haelewi hivyo yule mzungu akanigeukia mm sababu nilikuwa hapo hapo ila naendelea na kinywaji changu. Akaniuliza je nazungumza kiingereza? Nikamjibu ndio. Akanieleza alivyo mweleza yule dada na wakati huo ana dola 100 mkononi. Mimi nikamwelewesha yule dada kuwa mzungu anataka kulipa kwa dola kisha hiyo change amrudishie tu TSH. Yule dada akakubali ila change ikawa tabu sababu tsh. 48000 ni sawa na dola 30 tu hivyo alitakiwa kurudisha change ya TSH iliyo sawa na $70. Basi mm nikasema leta hiyo hela niwasaidie change angalau $50×2. Mzungu akafurahi sana na kuanza kushukuru. akasema “Sikutegemea kupata mtu wakunipa msaada mkubwa namna hii hapa” Thank you ten times. Nikawapa change na mm nikaweka dola 100 kwenye wallet na nilichoangalia ni mwaka tu. nilipoona 2006 nikaona iko poa. Yule dada akarudisha change yenye thamani ya doda 20 na mzungu akachukua Grants yake huyoooooo akaenda kwenye gari huku haishi kunishukuru.
Alipofika kwenye gari, nilishangaa alipanda kama ninja na gari iliondolewa kwa spidi sana. Hii kidogo ikanipa wasiwasi nikaenda msalani nakutoa wallet ili niikague ile hela vizuri. Katika kuiangalia nikakuta kumbe ni karatasi kabisa. yani kila kitu wamepatia kiasi kwamba naona zile taa za kaunta zilinichanganya sikuweza kugundua kuwa ni noti bandia. Yani dada yangu hicho kitu kiliniuma sana sana sana hadi ile bia haikushuka tena nikaenda zangu home hata usingizi sipati. Nikajiuliza hivi huyu mzungu kwa nini anatufanya tusiweze kusaidiana? kwa sababu mm nimeogopa kabisa hata kumsaidia mtu change au nikiona mzungu nasema ni wale wale tu. Ukizingatia hizi dola nilikuwa nazikusanya kila nikipata hela naenda kuchange nipate dola ili zikifikia kiasi Fulani kuna jambo langu la maendeleo nataka kufanya. Hii ni njia yangu yakutunza pesa pia coz ukipeleka bank ni rahisi kutumia.
Basi dada yangu nikakumbuka katika kipindi chako (huwa nawasikiliza kila nikipata nafasi au nikiwa barabarani kwenye gari)kuna siku mlikuwa mnazungumzia mzungu tapeli aliyekamatwa Mikocheni na alikuwa akitapeli watu kwa kuwapa dola feki. Je, mlifuatilia hadi mwisho? Alirudishwa kwao? Huyu wa kwangu ni mwembamba na anazungumza kistaarabu sana na kwa fadhila zetu waTZ ni lazima umsaidie mtu yeyote hasa akiwa mgeni tena hatutaki apate shida.
OMBI.
Embu cheki na vyanzo vyako mjue hatma ya yule mzungu ilikuwaje? na je huyu ni mwingine au la? Pia uangalie namna yakuliweka hili kwenye blog yako au kipindi chako kuwasaidia waTZ maskini wenzetu wasijefika nilipo fika mm. INAUMA SANA DINA.

11 Comments

 1. Anonymous

  November 4, 2013 at 6:55 am

  Immigration wanatakiwa mtu kama huyu akikamatwa waitwe wote aliowatapeli awalipe kisha arudishwe kwao. Pole sana bro.

 2. Anonymous

  November 4, 2013 at 9:39 am

  pole dada angu hata hivyo kwa sasa dunia imebadilika sana hakuna cha mzungu wala mbongo, watu tunaogopana na hata ukiwa na shida kweli kupata msaada inakuwa ngumu

 3. Anonymous

  November 4, 2013 at 9:50 am

  Pole sana ndugu yangu kwa kukutana na mzungu tapeli. Kwa sasa hapa Dar usimuamini hata Mtanzania mwenzako. Kuna mdada namfahamu yy kazi yake ni hiyo ya dola feki. Nasikia anaenda kwenye maduka ya vifaa vya electronics na maduka makubwa anafanya manunuzi akifika kulipa anatoa dola feki then anaenda kuuza zile bidhaa kwake na kujipatia TShs za kujikimu. Kwa hiyo watu wote inapaswa tuwe waangalifu sana, hatujui huyo mzungu anashirikiana na watanzania wangapi.

 4. emu-three

  November 4, 2013 at 10:40 am

  Dunia ya sasa unashindwa umwamini nani, maana hata wale wenyeshida ya kweli watashindwa kusaidiwa, sijui tunakwenda, wapi…

 5. kaisiki

  November 4, 2013 at 2:11 pm

  pole kijana,kupotea njia ndio kujua njia, na imani utakuwa makini siku nyingine na funzo kwetu pia kupenda kupapatikia wazungu ndo tukome kwani ata wao wana njaa vilevile.

 6. Mai

  November 4, 2013 at 2:25 pm

  duuuh hakuna kusaidiana sasa hivi ndugu zangu. yaani kuna mbinu za kila aina sasahv. kwasie wenye biashara za tigopesa na zunazofanana na hizi ndio kabisa tunawindwaje??? na kila siku wanabuni mbinu mpya.

 7. esther nyalusi

  November 5, 2013 at 5:24 am

  Pole Sana kijana ndio ulemsemo WA sema wangu umeniponza sasa hii itatufanya tuwe waoga kuomba chenji na ndio tutaonekana tuna roho mbaya

 8. Anonymous

  November 5, 2013 at 6:04 pm

  pole sana ndugu yangu kwa matatizo yaliyokupata kwa huku, wenzetu wana peni zao ikiwa pesa ni feki inajiandika na ikiwa ni yenyewe haijiandiki.

 9. Anonymous

  November 7, 2013 at 6:29 am

  Pole kwa mkasa uliokupata. Siku nyingine kuwa makini hata ikiwa ni madafu yetu, matapeli wapo kona zote za dunia. Lakini kwa nini mnatumia dola ndani ya Tanzania? Mnashusha thamani ya hela yetu na kusababisha mfumko wa bei (inflation). Nchi zilizo imara haziruhusu upuuzi huu, kama mtu ana hela ya kigeni akachange bank au bureau de change wenye uwezo wa kuhakiki hizo hela zaidi. Msilipe malipo ya huduma mnayopata ndani ya bongo kwa dollar labda kama mtu anasafiri nje ya nchi. (Nauli).

 10. salha senga

  November 8, 2013 at 1:25 pm

  habari pole sana, huyo mzungu nishamjua alishawahi kunitapeli na mm hivyo hivyo, kaja dukani kwangu nilikuwa nauza vitu vya umeme kama pasi birika na venginevyo, basi nishampa rice cooker akaniambia ana dola nawezamrudishia chengi kwa tshs nikamwambia sawa, alivyonilipa alikuwa kaikunja, lkn jinsi alivyoondoka mbio nilishktuka na kuangalia kumbe ni feki tena ni mia…….
  basi ikawa imekula kwangu sasa nikaja nikafunga ile biashara nikafungua biashara ya chakula basi akaja usiku akaagiza kuku 3 akaniambia mbona dada umenipokea vibaya hivyo nikamwambia wala nimechoka tu(kumbe nimeshamkumbuka) akaniambia unajua sasa ni usiku na hakuna bureau de change iko wazi naweza kukulipa kwa dola nikamwambia sawa….. akasema naenda kukaa kwenye gari uniletee chakula kule ikamwambia sawa lkn niletee kwanza hiyo hela.. naona alishashtuka basi alivyoenda kwenye gari ikakimbizwa mbio… na mm nilisema kama angeleta ile hela nilikuwa namwita mwizi ili akome na huo mchezo wake mchafu….
  hiyo ndio tabia yake kashatapeli wengi kwa njia hiyo….na huwa anabadilisha magari
  ukimwona ni mrefu wa wastani, ana blond hair, kama blue eyes, bad saving mwembamba alafu anapenda kuvaa jeans na kuchomekea shati mwondoko wake kama alazamisha kudunda

  tumtangazeni jamani huyu mzungu akamatwe fasta atawamaliza wengi sio mtu mzuri kabisa wewe unahangaika na maisha yeye anajua kuja kukutapeli
  watu kama hawa wanatakiwa wakomeshwe kabisa na wapewe adhabu kali….

 11. Anonymous

  November 11, 2013 at 9:00 am

  POLE SANA KWA YALIYOKUKUTA NA ASANTE PIA KWA KUTUJUZA SISI WENGINE AMBAO HATUKUJUA.

Leave a Reply