Uncategorized

AMARULA KITCHEN PARTY GALA ILIPOFANYIKA DEC 8

By  | 
WOMEN IN BALANCE KITCHEN PARTY GALA ILIFANYIKA TAREHE 8 DEC 2012.
KATIKA UKUMBI WA GRAND HALL PICOLLO IKIWA NI YA MWISHO KWA MWAKA HUU.ILIPEWA NGUVU KUBWA NA KINYWAJI CHA AMARULA CREAM.
 Wageni 100 waliokuwa wakiingia mwanzo walipata kila mmoja glass ya amarula cream.
 Brand manager wa Amarula cream Diana Balyagati akizungumza.
 Kulikuwa na kipengele cha kutoa chupa ya Amarula kwa wale waliopendeza.Kila mmoja alikuwa kapendeza kweli kweli lakini wachache walipata bahati ya kupata chupa hiyo nzima.Ilikuwa kama zawadi ya awali ya msimu wa sikukuu unakuja.
Asante Amarula,asante Diana brand manager wa Amarula kwa support yenu katika kitchen party gala mwaka huu.Tunaamini mwaka ujao 2014 tutaendelea kuwa pamoja
Tulikuwa na sponsors wetu wengine HC Human cherish pad.Wanakutengenezea pad,pantliner,maternity pad,shower gel,hand lotion na lotion za olive oil.
Wanawake 50 wa mwanzo walijipatia pantliner za bure kutoka kwa mkurugenzi mwenyewe Bi Celina Letara.
Bi Celina Letara akiongea na wanawake
 Sponsor wetu wengine walikuwa Cassandra lingerie mambo ya chupi,sidiria,nguo za kuogelea,kulalia na sasa hivi wana hereni,cheni,pete kwa wadada na wamama.
 Chupi na sidiria zilinunuliwa maana katika masomo tuliambiwa pia sio ishu unavaa nguo ya ndani miaka na miaka mpaka mipira inaanza kuachia.Sidiria imeshachoka wewe bado umo tu mpaka hela ulonunulia ishaisha.Sio mbaya mara kwa mara kujifurahisha mwenyewe kwa kujinunulia nguo za ndani za kutosha.
Mkurugenzi wa Cassandra Nambua alipata wasaa wa kuongea pia.
Asante wadhamini wetu woote amarula cream,pad za HC,cassandra,clouds fm bila kuwasahau Picollo hotel.
Tukutane mwakani tena tulijaaliwa tuendelee kushirikiana kwenye women in balance kitchen party gala.

1 Comment

  1. Anonymous

    December 16, 2013 at 12:03 pm

    Nakuona Dina na kitumbo mwenyewe, umependezaje!!! Mungu akubariki umalize salama mwaya.

Leave a Reply