Uncategorized

REST IN PEACE TATA MADIBA!

By  | 
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ameaga
dunia.

Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye
aliongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada
ya kufungwa jela kwa miaka 27.Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa
hospitalini kwa miezi mitatu.

Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa
Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa
hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais
aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kuondoka
gerezani.
Hakuonekana sana hadharani tangu alipostaafu mwaka 2004.
Nelson Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mwafrika mweusi wa Afrika
Kusini,baada ya vita vya muda mrefu dhidi ya utawala wa kizungu.
Kama kijana, Mandela alipenda masumbwi. ”Masumbwi ni bure, Ukiwa ulingoni ,
umri na hadhi yako pamoja na mali yako sio muhimu,” aliandika katika kitabu
chake kuhusu maisha yake.

Mwaka 1961 Mandela na mkewe Winnie na mtoto wao wa kwanza Zindzi.

 
Kufuatia kesi ya pili ya uhaini dhidi ya Mandela, alifungwa maisha jela mwaka
1964.
Hatimaye zaidi ya miaka ishirini baada ya kufungwa jela,Mandela aliachiliwa
mwaka 1990.

Mandela alitawala nchi hiyo kwa muhula mmoja pekee na mnamo mwaka 1999 akawa
mmoja wa viongiozi wachache wa Afrika kuachia ngazi kwa hiari. Thabo Mbeki,
alipewa jukumu la kumrithi Mandela kama rais na kiongozi wa ANC.
Baada ya kutalakiana na mkewe Winnie , Mandela alimuoa Graca Machel. Bi Machel ni mjane wa aliyekuwa
rais wa Msumbiji Samora Machel. Bi Graca na Mandela walianzisha hazina ya
kuwasaidia watoto wasio na uwezo mkubwa maishani.
“What counts in life is not the mere fact that we have lived. It is what difference we have made to the lives of others that will determine the significance of the life we lead.”
R.I.P tata Madiba!

3 Comments

 1. Anonymous

  December 10, 2013 at 5:33 am

  R.I.P Tutakukumbuka daima milele, na tusisahau alotuachia kuyafuata, kubwa nililojifunza kusamehe, kwa hali ya kawaida mtu kateswa jela angetoka dhahili wabaya wake wakaburu wangekiona cha moto, lkn kwa Mandela ilikuwa tofauti kabisa, kubwa ni kusamehe saba mara sabini, hakika alikuwa muungwa, nani anaweza, but Mungu amuweke mahali pema peponi Amin.

 2. Anonymous

  December 10, 2013 at 11:09 am

  Lala ngoxolo Tata.

 3. Daniel kashaigiri

  February 22, 2014 at 9:35 pm

  nami,nitakukumbuka madiba hasa kwa moyo wako wa kusamehe watu waliokuweka gerezeni kwa miaka 27, pumuzika kwa amani madiba

Leave a Reply