Uncategorized

SIKUKUU NDIO HIZI ZAJA,TUPEANE IDEA ZA VYAKULA VYA KUPIKA MSIMU HUU.

By  | 
Msimu wa sikuu ya christmass ukifika watu wengi hufikiria nguo,mapambo ya nyumbani,vinywaji na chakula.Chakula ndio kiunganishi kikubwa cha familia kwani hutulazimu kukaa pamoja wakati huo wakula.
Shopping ya chakula hufanyika mapema kabisa hasa mama ukishajua utapika nini kwa familia yako.Na msimu huu kama ni familia basi mpo wote maana na shule zimefunga hivyo watoto wapo nyumbani.Ni kipindi ambacho ndugu jamaa na marafiki hufunga safari kuja kwako kujumuika na wewe inategemea na mlivyokubaliana.
Nilikuwa nimekaa nafikiria nipike nini siku hiyo maana nategemea wageni siku hiyo.
 
Sikukuu tumeshazoea kupika pilau yaani bila pilau sio sikukuu.Pilau la nyama ya ng’ombe,mbuzi,kuku,samaki,firigisi n.k.Kingine kinachoongezeka labda ndizi au balada la pilau kukapikwa biriani.
 
Tupeane mawazo ya vile tunavyoweza kuvipika siku hiyo.

6 Comments

 1. zena juma

  December 23, 2013 at 5:41 am

  sikukuu kama hizi zinavyoongozana kwa mfano kama vile xmass inakuwa wiki hii mwaka mpaya wiki ijao, kuna mwaka sikumbuki ni mwaka gani ilipotoka xmass, ikafata mwaka mpya halafu ikafata idd, bwana tafrani sasa ina maana wiki zote hizi utapika birian na pilau inachosha, niliwashauri home, tulipopika xmass pilau basi mwaka mpya tukapika vitafunwa tu, tulikaanga, ndizi mzuzu, viazi mbatata, sambusa, kalimati, bajia, chapati, tukatengeneza na supu ya mbuzi yenye kichuri, tukakaanga nyama ya kuku, kukawa na vinywjaji, juice na soda, ilinoga ki ukweli, then idd tuka pika ndizi za nazi na wali wa wa nazi, kisamvu cha nazi na samaki wa nazi ki ukweli was good, na walinisifia kwa uchaguzi niliofanya watu waliburudika. wakapata ladha tofauti. embu emagine sikukuu zote tatu iwe ndo pilau pilau na wewe linakinaishije

 2. Anonymous

  December 24, 2013 at 4:29 am

  kuna vingi vya kuanda kipiundi hiko ni wewe mama wa familia kuw mbunifu
  pilau ,chines mixed rice,birian,wali wa tambn.k togeher vikaendana na chapat kwa rost,ama mikat ya kilebnan,ndiz mbich viazi vya nazi ni wewe mwenyew kujipanga unataka iweje
  still unaweza kuopika pilau lakn kwa ladha tofsuti tofauti all in all ubunifu jikn wat matters

 3. Anonymous

  January 2, 2014 at 6:10 am

  jamani dina unaniudh kutokublog naipenda sn blog yako hata km hutak kuweka picha zako basi blog kuhsu v2 vngne ss km hv mjamzto hutak kublog ukshajifungua utakavokua busy na mtoto c ndo basi kublog!!! pls jitahd tunajua inawezekana upo busy sn lkn me nikiingia humu hamna mpya duh hata cfurahii

  J.

 4. MOJAONE

  January 12, 2014 at 1:41 pm

  NI KWELI

 5. MOJAONE

  January 12, 2014 at 1:42 pm

  NIMEPAKUMBUKA SANA HAPA

 6. Aphonce chadali

  January 27, 2014 at 12:09 pm

  Nomaa sanaaa

Leave a Reply