Uncategorized

YALIYOJIRI KATIKA WOMEN IN BALANCE KITCHEN PARTY GALA DEC 8

By  | 
 Kitchen party gala ilifanyika siku ya jumapili ya tarehe 8 pale piccolo hotel Kawe.Ni siku ambayo mvua kubwa ilinyesha lakini tuanshukuru kinamama na wadada walijitokeza wa kutosha siku hiyo.MC wetu siku hiyo alikuwa  Gladys Chiduo alimaarufu Zipompa pompa.Alituongozea shughuli yetu kwa kuwakaribisha wageni na shughuli kuanza.
 Kutoka team ya waandaaji my patner Vida alielezea kwa kifupi theme yetu ya safari hii ambayo ni MWANAMKE MWENYE FURAHA.Pia mipango yetu ya mwakani uwepo wa members wa ktchen party gala.Kuna watu toka tunaanza safari hii mwaka 2011 hawajawahi kukosa wamekuwa na sisi bega kwa bega na hata kwa mawazo.Ilifika wakati tulihairisha kufanya hii lakini walitutia moyo kuwa tutafute tu hata ukumbi mdogo tufanye kuliko kutokufanya kabisa hii ni baada ya kuhangaika sana kupata ukumbi.
 Wageni wetu walishiriki kufungua champaign ambazo lengo ni kutakiana maisha ya furaha na afya njema
 Iliyowafikia walipata kwenye glass

 Wadada wamama waligonga cheers kama ishara ya kutakiana furaha ambayo kila mmoja anaitafuta au anayo,afya njema pia maisha mema katika kufunga mwaka huu 2013.
 cheers****
Tulianza mazungumzo yetu na Mama Victor ambae kawaida lazima aanze na sala.Katika somo lake mama Victor alisema wanawake wengi furaha yao inakamilishwa na vitu au watu lakini furaha ya kweli ipo kwenye NAFSI lakini kubwa zaidi tumeacha kumshirikisha Mungu awe kiongozi katika maisha yetu.
 Meza wa wazungumzaji Chriss Mauki,Aunty Sadaka amepumzika kwa sasa,na Getrude Mungai.
 Chriss Mauki kwa upande wa psychology anasema kila mtu ana namna yake anavyoitazama furaha.Mwingine anaona akipata kazi nzuri atakuwa na furaha,akiolewa na mume mwenye pesa atakuwa na furaha.Akiendesha gari kali nguo na mapambo ya gharama atakuwa na furaha na kadri anavyozidi ndivyo ambavyo anajikuta haridhiki na wala havikamilishi furaha kama alivyodhani.Wanawake karibu wote wanapenda kuwa na furaha lakini wao wenyewe wakati mwingine ndio chimbuko la maisha ya huzuni na wasiwasi.Unakuta mtu anaishi maisha ya mtu mwingine akihisi akiwa kama yule ndio atakuwa na furaha.Akiona mwenzie kapata kitu fulani yupo tayari ajinyime ajitese ili aende sawa nae.Yalizungumzwa mengi siwezi kuyamaliza hapa.
 wenye maswali waliuliza
 Getrude nae alikamilisha safu ya wazungumzaji kwa somo lake ambalo ni la ndani zaidi kikeni lakini theme ikiwa ni ile ile mwanamke mwenye furaha.
 Kawaida lazima awasimamishe mjinyooshe kike
 Kamata position…kamata dashboard…shake what your mama gave you…drop like its hot…..
Picha zaidi zinakuja watu na mishono yao mdada alitokelezea.

4 Comments

 1. Anonymous

  December 16, 2013 at 9:26 am

  dina sijakuona why, kwa nn?

 2. Anonymous

  December 20, 2013 at 11:23 am

  dina mm napenda sana kitchen part gala nashauli ianzishwe mikoani kama morogoro,alafu kama mtu ni profesional like nutritionist nurses or doctar anaweza pata nafasi ya kufundisha chochote?na je nikitaka kuudhuria nalipa shiling ngapi?

 3. Anonymous

  January 24, 2014 at 12:47 pm

  dada Dina Mambo, jaman update blog basi hatujakusikia muda sana!

 4. Anonymous

  January 29, 2014 at 12:35 pm

  Hey Dina, nashukuru kwa kuonekana tena jaman Tulikumic sana na hiv leo tena haupo shida.Hongera sana Dina na Ruben Mungu awajalie maisha mema.

Leave a Reply