Uncategorized

SHUKRANI ZA DHATI KWA SAPOTI YAKO KWA MWAKA JANA 2013.

By  | 
Kwenye maisha yangu sikuwaza kama ipo siku nitaweza kupewa tuzo ya heshima kwa kile ninachokifanya katika kazi zangu za kila siku.Msingi wa yote ni kipindi changu cha leo tena kufanya kipindi haitoshi wewe kama mtangazaji unajiongeza vipi katika taaluma yako?hapo ndio nikajikuta nafanya mambo mbali mbali yaliyoniwezesha kupewa heshima mwaka jana mwezi wa tatu.Ilikuwa tarehe 28 mwezi wa tatu nikapata tuzo ya WOMAN OF THE YEAR ya TANZANIA WOMEN OF ACHIVEMENT.Wakati jina langu linatajwa nilihisi kama naota hivi au nimesikia vibaya sikuamini maana nilikuwa nipo na mama zangu wengi waliofanya makubwa katika sekta mbalimbali nilipojihakikishia ni mimi kweli wala sioti ndoto ndio nikasimama kwenda kupokea tuzo yangu.Namshukuru Mungu sana sana kwa baraka hiyo katika mwaka 2013.
Mwaka jana 2013 pia nilipata nafasi ya kuteuliwa kuwa miongoni mwa mabalozi wa shirika la OXFAM.Shirika linalojihusisha na wanawake,chakula na kilimo.Tuliteuliwa mabalozi 7 na kukabidhiwa tuzo maalum ya mabalozi.Mwaka huu tukijaaliwa kuna wanawake watafanikiwa kushiriki nami katika mradi wangu kama balozi wa oxfam utakaohusu mambo ya chakula.
Kwa kushirikiana na UWF tulifanya tena tuzo ya mwanamakuka kwa mwaka wa pili.Tuzo kwa wanawake wajasiriamali wale ambao bado wana struggle na tuzo ilienda kwa Aziza Mbogolume mama mchora picha.Alijishindia tsh ml 6.
Mwaka jana nilianzisha mradi unaitwa dada dina cares.Kwa kutembelea vituo vya watoto yatima nimegundua watoto wanalelewa na watu wenye mapenzi ya kulea watoto lakini bado hawawezi kuwapa huduma mbalimbali muhimu kwa uhakika.Malazi,chakula,mavazi,vifaa vya shule bado wanahangaika.Ndio nikaanzisha hiki kitu ili kushirikiana na wadau mbalimbali tuweze kuvisapoti hivi vituo.
 Tulipata vituo vitatu tulivyoweza kuchanga pesa na kuwanunulia chakula,unga,mchele,sukari na maharage.
 Vifaa vya shule kuanzia madaftari,pen,pensil,vifutio,rula n.k
 Vitanda,mashuka,magodoro,mapazia,nyavu za madirisha,na vyandarua

 Nilipata chance ya kukaa na watoto,kuongea na kuconnect nao.
 Tulikula na kucheza nao
 
Toka nilipoanza Dada Dina Cares nimepokea simu nyingi sana za wadau,watu binafsi,vikundi,makampuni,mashirika mbalimbali yakiomba kuelekezwa namna ya kuvifikia hivi vituo ili kuvipa misaada mbalimbali.Na wao wananipa feedback kila wakati ya namna wanavyoendelea kupata misaada.Watu kujitolea kwa yatima wanaweza ila kuwa na taarifa sahihi ya wapi waende ndio wanakuwa hawajui.
Mwezi dec ilikuwa nifanye tena huu utaratibu lakini sikuwa kwenye hali nzuri ya kuhimili mikiki mikiki.
Pia nilianzisha vibubu viwili hapo ofisini ambavyo watu wamekuwa wakidumbukiza pesa humo,hata wale ambao wamekuwa wakituma nimekuwa nadumbukiza humo ili kukusanya hela zitakazoendelea kusaidia mahitaji ya vituo vya watoto yatima.Nina vibubu kama kumi hivi ukiwa intrested nicheki nikupe kimoja utakaa nacho mpaka mwezi wa saba tutakifungua na hela zitakazokuwemo tutazitumia kwa mchakato mwingine wa dada dina cares utakaofika mpaka vituo vya mikoa nje ya Dar es salaam.
Kwa mwaka wa tatu mimi na my patner Vida Nassari tumefanikiwa pia kuendeleza semina za wanawake za kitchen party gala.Tulianza mwaka 2011 na mwaka huu wa 2014 ni mwaka wetu wa nne.Kwa hilo tunamshukuru Mungu tunaendelea japo kumekuwepo na chagamoto nyingi sana.
 
Ninachosikitika mwaka jana sikuweza kufanya tuzo ya dada bora wa kazi za nyumbani.Ni tuzo tuliyoweza kuifanya kwa miaka miwili mfululizo tena kwa mafanikio.Tumeweza kuwafanya wasichana wa kazi za majumbani kuonekana na wao ni watu na wanapaswa kuheshimika kwani mchango wao katika malezi na ustawi wa familia ni mkubwa wasipuuzwe,kunyanyaswa na kubezwa na waajiri wao.Ilishindikana kufanyika kwa sababu za kiofisi ratiba ilikaa vibaya mwaka huu panapo majaaliwa tutafanikisha naamini.
 
Malengo ni mengi ndoto ni nyingi lakini huwezi kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.Kila jambo na wakati wake tusichoke kuamini katika ndoto zetu na kuzifanyia kazi.Ukiwa na ndoto bila uwajibikaji katika kutimiza ndoto husika ni sawa na ndoto ya usiku ukiwa umelala umeokota mahela mengi na asubuhi kuamka na kukuta ilikuwa ni ndoto tu na sio kweli.Wakati mwingine ni ngumu kutimiza malengo flani lakini usichoke kujaribu.Jaribu tena na tena na tena ni bora ujaribu ushindwe kuliko kutokujaribu kabisa.Na uwe na imani kama huna imani ni kazi bure.Imani yako ndio itakufikisha kwa sababu unaamini katika hiyo ndoto husika.Hata akitokea mtu kukukatisha tamaa au kukubeza hawezi kufaulu kwasababu una imani na ndoto yako.
 
I wish u all the best katika mwaka huu mpya 2014!

27 Comments

 1. maasai Gal

  January 27, 2014 at 4:26 pm

  Dina em weka sawa hili jambo la watu kusema umedhulumu watoto yatima? Em weka sawa manake nimeona kwa sinta mtu kachombeza na jamii forum pia. Em tuweke sawa tujue nikweli au uzushi

  • dinamariesblog

   January 27, 2014 at 4:51 pm

   Watu kuchafua wenzao wanapenda sana..watoto gani yatima niliowadhulumu nimedhulumu kipi?nikupe namba zao uwapigie uwaulize kama nina tatizo nao au kuna mahali nimewadhulumu kitu.Na nawadhulumu vipi?unadhani kusaidia yatima kuna faida flani unapata?Watu wana mambo sana na roho mbaya!

  • Anonymous

   January 27, 2014 at 4:57 pm

   Mmh kuwa wazi dina. Naskia kuna pesa ulipokea ukapotea nazo wala huku fika sha kwa wahusika. No me soma vizuri hili sakata kule jamii forum. Nawewe apo juu ulisema kwania yakumtetea au? Ulidhani angekubali? Peleka ushamba wako umasaini baladhuli wewe. Wakuja utawajua tu. Ptyuuuu

  • dinamariesblog

   January 27, 2014 at 5:05 pm

   pesa zipi na kutoka kwa nani?kama pesa ziilikuwa zinachangwa kununua hivyo vitu nilivyovitaja hapo nimepotea nazo wapi?kitu gani sikupeleka katika hivyo vituo?mbona hakuna alowahi kunifata kuwa nimepotea na hela.Huyo aloandika jamii forum hajachangia yatima.Waliochangia siwana namba zangu mbona hawajanilalamikia.Na nimesema wapo walioendelea kutuma hela zipo kwenye hicho kibubu nilichoweka hapo muda ukifika kitavunjwa.Sijadhulumu pesa ya mtu nina hakika wote waliochangia wana utu wa kuniuliza chochote na si kushiriki katika kupakana matope mitandaoni.Huyo aloandika huko mimi na yeye Mungu atatuhukumu!

  • juli

   January 28, 2014 at 9:15 am

   pole Dina,watu hawakosi la kusema,Mungu atakulipia

 2. Anonymous

  January 27, 2014 at 6:01 pm

  Mi nakutakia kila la kheri katika unayoyafanya, sio watu wote wanaweza kufanya kama unavyofanya. Mara nying binadamu tunapenda sana kukatisha wenzetu tamaa hasa pale wanapofanya mambo mzuri.Big up Dina!! Usife moyo….Go go go go!

 3. Anonymous

  January 27, 2014 at 9:39 pm

  Ubinadamu kazi mamito. Usikate tamaa songa mbele(Alfa song)! Watu wanapenda Sana kichafua wenzao. Yote uakabidhi kwa Mungu na endelea kutoa misaada kwa hao watoto.

 4. Anonymous

  January 28, 2014 at 10:56 am

  dina usivunjike moyo, binaadamu ndo walivyo ukifanya mema utapewa mabaya, mungu ndo atakae kulipa hisani na utu wako, unajituma na kuwajali kwa hali na mali watoto yatima, si jambo dogo.

 5. Anonymous

  January 28, 2014 at 11:01 am

  usikate tamaa dina, kuna matajiri wangapi tz, hawawasaidii yatima wakiona umejitolea wanaanza kuku let down. kaza moyo dina mungu yupo pamoja nawe. sio wale wanaojionyesha kwenye blog zao wako wapi wamestarehe vipi, wamekula nini na vibwana vyao, upuuzi mtupu.

 6. Anonymous

  January 28, 2014 at 11:57 am

  sasa na wewe kwenye HELA kwenye KIBUBU zinafanya nini? ndio maana basi unaambiwa UMEKULA, ZITOE kwa WAHUSIKA, KWISHNEY.

 7. Anonymous

  January 28, 2014 at 1:06 pm

  Usivunjike moyo ao walioandika umekula ela za yatima mbona wao awajaanzisha yakwao yakusaidia yatima? Achana zao nice day.

 8. Anonymous

  January 28, 2014 at 6:32 pm

  Hao ni wakuwapuuza tu,mungu atakulipa kwa mema unayotenda kwa yatima

 9. kiparis

  January 28, 2014 at 8:31 pm

  Me nataka kibubu nakipataje nipo Mwanza….Watu kuongea kawaida yao usitumie nguvu nyingiii kuwaelewesha mama

 10. massawe

  January 28, 2014 at 10:37 pm

  Fanya uwezavyo Na Mungu atakujalia usichanganywe Na maneno ya watu walikupa michango wanakuamin ndio maana wamekupa ongeraa Dina

 11. Anonymous

  January 29, 2014 at 6:11 am

  Hata ufanye mazuri kiasi gani, wanadamu ni wanadamu tu, wanaojua kushukuru ni mmoja kati ya kumi, wengine tisa watabeza, kutoa kasoro na kuzusha uongo, Dada dina usiangalie watu wanasema nini, wewe fanya iliyo nafasi yako kadiri Mungu unavyokujalia uwezo na Upeo.. Achana na sisi wanadamu ndio tumeshaumbwa hivyo kusema lazima!!

 12. Anonymous

  January 29, 2014 at 7:06 am

  Kazi nzur dada Dina, mungu atakulipia kwa wema wako binadamu cku zote tuna majungu hatukos la kusema hasa pale mtu anapofanya mazur na kufanikiwa! Achana na kelele za maadui wangekuwa marafik wangekuface na kuhoji! Mungu akuepushe na mabaya na kukufanikisha kwa kila njema…..nakupenda tu dada japo nakusikia tu kweny leo tena….much love siz

 13. Anonymous

  January 29, 2014 at 10:19 am

  Am moo than happy to see her once again…….. Kweli nimefurahi sana. kwamza kukuona mama mtarajajiwa.kuiona familia yako na wewe mwenyewe. Usipoteze muda wako bure kujibizana na walimwengu wenye hila zisizo na sababu. Kwani hauwafahamu? Umepost ili kusubiri wakupongeze? Utakaa sana mama. Sio woote wana penda mafanikio yako….. wanao sema umekula hela za yatima usibishane nao saana kujipa stress bure-kwakua haukuvunja nyumba wala kuiba kwenye ac zao,Mungu yupo anae elewa unayo yafanya.

 14. willy choga

  January 29, 2014 at 11:09 am

  kwanza nianze kwa kukupa pongezi dada yangu maana kazi uifanyayo inamchango mkubwa sana katika jamii,tunajifunza mengi kupitia kipindi chako na pia naweza kusema wewe ni super women, na kwawale wasiotaka kuyaona hayo ni wana husda zao tuu na pengine walitaka kufika ulipo wewe lakini wameshindwa .

 15. Anonymous

  January 30, 2014 at 10:37 am

  Dina asante sana ulichoandika au kuzungumza ni kweli tupu,bila bidii na maarifa ni kazi bure,asante nakupenda sana,nakutakia mafanikio mema

 16. Anonymous

  January 30, 2014 at 11:38 am

  Binafsi nimeliona hilo la kudhurumu kwenye blog flan lkn moyo wangu ukakataa kbs kuamini kua unawezakutenda hivyo.Wasamehee wote wanaozua mabaya juu yako kwan Mungu pekee ndie ajuae na atakulipa kwa ulitendalo.Dina umbunifu sana labda kuna waliotaman idea hiyo waianzishe want ili iwanufaishe.KILA LAKHERI NAKUTAKIA.Mama Luqman

 17. RUKY

  January 30, 2014 at 5:02 pm

  JAMANI KWANINI WATU WANAPENDA KUWAVUNJA MIYO WENZAO HIVI MI SIJAWAHI KUKUONA LIVE BUT KWA KUKUSIKIA TU KUTOKEA KWA REDIO NA BLOG YAKO MBONA NAKUAMINIA SANA TENA MI MKWUBWA KWAKO NA NAJIPANGA ONE DAY NIKIJA TZ NIKUTAFUTE TUFANYE KAZI PAMOJA..BUT GO GO DINA USIKATISHWE NA WATU TAMAA WACHACHATE HII NI CHANGA MOTO TUU ILA MUNGU ATAKUSAIDIA.. JAMANI USIACHE KUENDELEA NA BLOG COZ MI MWENYEWE MPAKA NLISAHA KUINGIA HUKU MUMMY NIKAJUA MPAKA UMALIZE LIKIZO YA UZAZI KM NILIVYOSIKIA.. LOVE U MY MDOGO..

 18. teressa simon

  January 31, 2014 at 1:04 pm

  Usivunjike moyo mpendwa Mungu anaona na atakulipia, watanzania sisi kazi yetu ni kuangalia namna ipi ya kumchafua mtu na kumkatisha tamaa.Dina mtaani wewe ni mwanamke jasiri ambae kila mwanamke angependa awe kama wewe na mwanaume angefurahi kuwa na mke kama wewe,nina furaha kubwa leo kupita na kukuta umeweka post Nilikumiss nakupenda kupita maelezo, your my inspiration.

 19. Anonymous

  February 1, 2014 at 8:26 am

  Usikate tamaa dada dina wa2 ndo walivyo wanatafuta sbb wakuchafulie hv kwanz huyo sinta una muona ana akil sawasawa kaz kukosoa wenzio ye mböna yake wanayajua sema hawatak kumuanika mshamba sana huyo bax tu.. kaza moyo dada ndo wanadam 2livyo

 20. Anonymous

  February 1, 2014 at 1:00 pm

  Tanzania hatunaga tabia ya kupeana sapoti kwa mambo mazuri ila kwa majungu tunaongoza endelea na kazi nzuri, hao wanaokupönda unakuta hawajawah kusaidia ht pipi hlf wa kwanza kuchonga mdomo.

 21. MOJAONE

  February 7, 2014 at 1:16 pm

  Asante kwa kujua mchango wetu.

 22. Hance

  May 13, 2014 at 10:08 pm

  big up Dina kwa hatua unazopiga,Mungu awe nawe katika yote unyotarajia kufanya

 23. Hance

  May 13, 2014 at 10:13 pm

  big up Dina kwa hatua unazopiga,Mungu awe nawe katika yote unyotarajia kufanya

Leave a Reply