Uncategorized

WAPENZI WANGU HAPPY NEW YEAR 2014.

By  | 
Happy new year wapenzi wangu woteee ni muda sijaongea nanyi hapa kwenye blog lakini wapo ambao naongea nao kwenye simu kila siku tukijuliana hali na kutakiana amani na upendo katika maisha haya tunayoishi.Mungu ni mwema tulifanikiwa kufunga mwaka 2013 na kuukaribisha 2014.Na bado tunaendelea kumuomba na kumshukuru aendelee kutusimamia na kutupigania kwani tunaweza mambo yote katika yeye atutiae nguvu.
Kiukweli mwaka 2013 kwangu ulikuwa wa baraka tele sina malalamiko yoyote zaidi ya kushukuru kwa hali zote nilizopitia.Kwa kazi ninayofanya nakutana na watu mbali mbali ambao pengine wamekata tamaa ya maisha kwa wingi wa changamoto zinazowakabili kimaisha na mimi kuona nimebarikiwa sana hata kama kuna jambo nalitamani kulipata sitalalamika kwa nini sina?bali ntaendelea kumuomba Mungu aendelee kunibariki.
 
Nimekaa muda kimyaa maswali yakawa mengi kuhusu mie kuwa mjamzito.Sikutaka kuzungumza hapa ili kukidhi kiu ya udaku kwa yule alokuwa akihoji tena wengine walikuwa wakituma comments na kashfa juu.Niliamua kukaa kimya nideal nalo mimi mwenyewe personal.Kama ulishawahi kusoma nilichowahi kuandika hapa http://www.dinamarios.co.tz/2013/05/maisha-bila-mama/
nilielezea maisha yangu ya nyuma yalivyofanya niwe muoga wa kuwa mama au kuolewa kama hukusoma ingia hapo usome.
Kwa hiyo hili lilipotokea nilihitaji love and support ili kusimama na kuamini kila kitu kitakuwa sawa.
Nashukuru Mungu nimepata hivyo vyote kutoka kwa mhusika mkuu.Anaitwa Reuben Ndege sio meneja wa skylight band kama walivyandika wadaku na wadakuzi.Amenipa love and support kwa kila hali.Tumekuwa wapenzi kwa miaka mingi sana lakini kama ujuavyo mapenzi ya ujana off and on zisizoisha kuvurugana kila leo.Ila sasa tupo pazuri.
Familia yangu pia baba yangu Mzee Peter amekuwepo na mimi bega kwa bega maana ndio baba ndio mama kwangu.
 
Pichani mimi,my brother in law Shady,mama mkwe,shadee,na mdogo wangu Ibra.
 
Namshukuru Mungu nimezungukwa na upendo na amani hilo ndio kubwa nililokuwa nahitaji.Kuna mliokuwa mnasema sijiu najificha,naona aibu,sijui sijiamini.Sasa ina maana siendi kazini?siendi hospital/clinic?siendi bank?shopping nipo tu nimejificha?
Kila mtu ana namna yake ya kudeal na vitu kwanza hata picha napiga basi sizipendi,sipendi simu wala computer naona vinanivuruga.
Kuna marafiki zangu ambao wamekuwa sehemu ya maisha yangu kwa hali yoyote sio ile ambayo ipo confortable kwao.Maana kuna marafiki watakuwa karibu na wewe wakati ule unaweza kwenda club huku na kule ukiwa katika hali nyinginge hawakutafuti na hawana mpango na wewe.Utakesha wewe ukiwatafuta ukihisi ni wenzako kumbe siku nyingi walishakudelete.Nawashukuru sana
Fide Mwakitalima,Asma Makau,Queen Geofrey,Sophy,Vida Nassari,Zamaradi,Gea Habib yaani naongea nao kila siku since day 1 wakinishauri hili na lile hata iwe usiku mwingi wapo kwa ajili yangu.
Kupitia leo tena hapa kwenye blog nina mama zangu,dada zangu,aunt zangu na kaka zangu ambao wamekuwa sehemu ya maisha yangu hata bila ya mimi kuwafahamu.Kila siku asubuhi mpaka usiku naongea nao kwa simu mpaka nahisi kama nawafahamu.Wamekuwa sehemu ya maisha yangu ni wengi siwezi kuwataja hapa.Ni upendo wa pekee kwa kweli mpaka wakati mwingine naogopa.
Mwaka huu mpya mie kwa sasa nimeuanza nikiwa nyumbani nimeanza likizo sipo kwenye leo tena.Sasa hata vya kublog sivioni,nikijaaliwa ntakuwa naandika vile ninavyoviona katika mazingira niliyopo sio ya ofisini.
 
Haya wapenzi kama kuna malengo hatukutimiza mwaka jana tuongeze juhudi zaidi kuyafikia mwaka huu….amani kwenu wote!

107 Comments

 1. Faith

  January 27, 2014 at 2:09 pm

  Hongera sana mammy, Yaani nimefurahi hadi machozi ya furaha. Binadamu tunatofautiana sana kuna wakati tunapenda ku judge au kuongea hata ambavyo hatuna uhakika navyo. Nimeipenda hiyo uliamua kuwasikiliza tu. Kusema ukweli wanakupenda na wewe ndo kioo chao ila hawataki kukiri hilo. Mungu akubariki sana Dina, wishing u all the best..!

 2. Faith

  January 27, 2014 at 2:13 pm

  Congrats mammy, binafsi nakupenda na napenda sana kazi yako. Kweli umetumia hekima sana katika kuandika, umenifanya nizidi kujifunza maisha yako. Napenda kwa jinsi ulivyo "wewe". Wishing you all the best, Siku nikikuona i will tell you this u msichana wa aina yake. keep it up mwanamke!

  • dinamariesblog

   January 27, 2014 at 4:37 pm

   Faith my dear asante…naamini ipo siku tutaonana tu.Ubarikiwe!

 3. Anonymous

  January 27, 2014 at 3:00 pm

  MUNGU ATAKUJAALIA NA ATAKUPA WEPESI WA MAMBO YOTE.

  (DONT WASTE WORDS ON PEOPLE WHO DESERVE YOUR SILENCE.
  SOMETIMES THE MOST POWERFUL THING YOU CAN SAY IS NOTHING ATT ALL)
  .DINA BINAADAMU HAWAACHI KUSEMA KWANI WAMEPEWA MIDOMO,ROHO MBAYA,CHUKI NK
  DONT LET NEGATIVE AND TOXIC PEOPLE RENT SPACE IN YOUR HEAD.
  RAISE THE RENT AND KICK THEM OUT!
  http://www.mediawebapps.com
  WATU WANAOLEWA NA WANAUME WANAKUFA WANAACHA NA WATOTO ,WATU WANAOLEWA NA WANAACHIKA , KIKUBWA KWAKO MAPENZI HATA UNGEOLEWA UTUALIKE TANZANIA NZIMA KAMA HUNA MAPENZI HUNA THAMANI .
  WANAOKUSEMA WAACHE WASEME WATAKAA KIMYA TU .
  MUNGU AWE NAWE DAIMA
  LOVE U

  • dinamariesblog

   January 27, 2014 at 4:36 pm

   Thank u so much…na nashukuru kwa kila kitu!

 4. Anonymous

  January 27, 2014 at 3:19 pm

  Nakupenda sana Dinah. Naomba nikupe hongera nyingi mno kwa mtoto unayemtaraji na pia kukupa moyo kuwa kuna tunaokupenda sana. Binafsi unaniinspire sana bila hata kusikia sauti yako; nikisoma humu bloguni tu nafurahi. NAkutakia maisha mapya na mema ya umama. Uishi kwa upendo na mani teletele. Stay blessed

  Christine

 5. Anonymous

  January 27, 2014 at 3:24 pm

  Hongera sana Dina na kila la kheri Mungu akusaidie umalize salama kipindi hichi ulichonacho na hatimaye kuwa mama. I hope itakuwa familia bora kwani kuwa kwenye relationship kwa muda mrefu inasaidia kujuana vizuri na kuanzisha familia nzuri pia. Mungu akusaidie

 6. maasai gal

  January 27, 2014 at 4:21 pm

  Mi cnamaneno mengi dina ila moja tu. Aise una hubby mkareeee. Duh nchakali ni mzuri haswa anamvuto yipo kiume, nguo zote zinamkubali kwakweli cjaona bado celebrity mwenye mwanaume mzuri kama wewe hayo mengine cjui pesa au nini zinatafutwaga tu ipo cku. Ila ndoa lini jamni yani navyokuteteaga huko mtaa wa pili watu wakikubipu hutadhani na kujua lol. Nahamu sana ya kumuona mtotowenu. Mungu ni mwema

 7. ini edo

  January 27, 2014 at 5:03 pm

  Sorry ivi reuben ndege ndo yule alikuwaga kwenye kipindi cha njia panda au??? Na kama cvyo je wanaundugu au majina tu yanafanana???

 8. Anonymous

  January 27, 2014 at 5:54 pm

  my der Dina nakumbuka hata mimi nilikusapoti kupata mtoto tuu kuolewa MUNGU akipenda. nimefurahi sana kusikia upo MJAMZITO utakapo jifungua ndio utaona raha ya maisha, najuwa ulikuwa mpweke kwa muda mwingi sana kupitia storry yako ya nyuma, my der mimi nakutakia kila la heri kwenye maisha yako MUNGU atakupa wepesi kulea mwanao….. mimi nazidi kushukuru MUNGU na vitoto vyangu wanazidi kuwa wakubwa, pia binadamu wamezoeea kuongea achana naoooo, ni yule yule mama KARIM au KHADIJA.

 9. Anonymous

  January 27, 2014 at 7:28 pm

  Kila la heri Dina,Mungu akusaidie ujifungue salama!

 10. Anonymous

  January 27, 2014 at 7:29 pm

  Kila la heri Dina,Mungu akusaidie ujifungue salama!

 11. Anonymous

  January 27, 2014 at 9:27 pm

  Mungu na akubariki Sana! Nilipitia kama yako ILA usijali ndo malimwengu, napataga vitu vingi Sana toka kwako, ktk kipondi chako cha Leo Tena na blog yako. Kiukweli najofunza mengi Sana. Mungu akutangulie ktk kipindi hiki ulicho nacho maana mm nimemaliza juzi Tu na sasa najiona niko ktk ulimwengu mpya baada ya kupata mwanangu, na enjoy wala siwezi elezea yaani. Kuwavna mtoto Ni raha Sana. Kumbuka Raha ya Dunia Ni WATOTO. All the best love.

 12. Anonymous

  January 28, 2014 at 12:21 am

  da dina binaadamu hawaachi kusema,hasa kwenye mitandao humu watu wanajificha kwa anonymous wanaandika wanavyojua mwenyewe.ila nina amini watu wengi wanaku admire mno mimi mmoja wapo.ni mdada ambae una heshima zako,ila vile vile una fan wako wanapenda kujua unaendeleaje,ambao njia yao rahisi ni kwenye mtandao tu.mungu atakujaalia utajifungua salama najua kwa asilimia zote wewe ni mama bora.please fan wako usisahau kutuwekea picha ya mtoto wako utakapozaa salama.

 13. Anonymous

  January 28, 2014 at 5:42 am

  aisee nimefurahi saaana tena sana nimekuwa busy sana, muda mrefu nimekuwa sikusikii wewe na Gea lakini nikifungua blog yako hakuna jipya nikajisemea huyu Dina sikuhizi kawa mvivu sana au anasoma? Lakini leo baada ya kufungua kukuta habari hii nzuri nikasema alaa kumbee! kazi yenyewe kubwa hiyo, inatosha kabisa kukaa kimya na kupumzika mamy, nimefuahi wewe utafikiri nimeshawahi kukuona live nakupenda sana Dina mwanangu nakuombea kwa Mungu akufikishe salama safari ya kuniletea kijukuu. Jamani uwiii nimefurahi sana Hongera sana mpe na mkwe Hongera sana. Nakupenda sana Dina.

 14. Anonymous

  January 28, 2014 at 5:48 am

  The happiest day!!!!!!!! Yaani japo ulikuwa hu post chochote humu nilikuwa naingia kila siku kwa hii blog nikiamini ipo cku nitakuta ume update yaani leo nimefurahi sana. Nakupenda sana ninajifunza mengi sana kwako. Nilihisi nimepunguza kitu kwenye maisha yangu kwa kukosa kusoma vitu vipya humu. All the best na likizo njema. Tukumbuke humu bloguni kwako tunahitaji mengi kutoka kwako. Maana duniani kujifunza hakuishi. Siku njema mam.

  Mama Alice

 15. Anonymous

  January 28, 2014 at 5:58 am

  Dina Story yako nimeisoma imesikitisha sana, ila mshukuru Mungu kwa yote hukukosa mama sisi mama zako tupo tena wengi tu, wamama wengi sana tunakupenda sana Dina.

 16. Mama 2 (Mrs M)

  January 28, 2014 at 6:22 am

  Nimekumis sana Dina! Mungu atakuongoza katika maisha yako yote. Na nina imani huyo mama Mkwe hatakuwa mama Mkwe msumbufu, nina imani atachukua nafasi ya mama mzazi. Nakutakia afya njema.

 17. Janeth

  January 28, 2014 at 7:17 am

  Hi!Dada Dina kwanza nakupenda sana tena sana, kila siku nakuombea baraka katika maisha yako. Maneno ya watu yasikukatishe tamaa Mungu ndie anaetoa na ndie atakayekusimamia katika kila hali, usikate tamaa songa mbele kwenye maisha kunachangamoto nyingi lakini Mungu akiwa upande wako hakuna atakayeweza kuwa juu yako.Mungu akutie nguvu wewe pamoja na mwenzi wako na mtoto wenu mtarajiwa kila la heri dada angu Nakupenda

 18. Anonymous

  January 28, 2014 at 7:19 am

  hongera sana Dina Mungu ni mwema na ameweza kuwaonyesha kwamba wee ni mwanadamu wa mfano wake, wal usijali maneno ya watu kila mtu kaaumbwa kwa udongo wake, mshukuru Mungu kwa kila jambo, naamii atakuongoza na atazidi kukuongoza siku zote za maisha yako, nakutaka kila la kheri katka safari yako ya uzazi my dea

 19. Anonymous

  January 28, 2014 at 8:24 am

  Hongera, Hongera sana Dina, Mungu akujalie uzima na afya njema siku zoote za ujauzito wako na ujifungue salama pia… Rahaje kuwa mama sasa!!! mimi nina mtoto mmoja tuu anamiaka 19 sasa natafuta mwingine mimba haiingii, nimechomwa mpaka sindano ya kufungua mirija lakini wapi!! Bado namtumainia Mungu atanipa tuu mwingine.

 20. Anonymous

  January 28, 2014 at 10:20 am

  nimekufurahia mnooo

 21. Thea Mtau

  January 28, 2014 at 11:02 am

  Wow! Hongera sana rafiki yangu Dina. Nimefurahi sana si tu kuona u mjamzito, bali pia kuona familia zenu zikiwa pamoja kwa furaha na upendo. Mungu aendelee kukubariki na kukujaalia kadri ya moyo wako.

 22. Anonymous

  January 28, 2014 at 11:22 am

  He Dina furaha niliyonayo haina kifani mungu akuzidishie afya na nguvu tele binaadamu ndivyo tulivyo hatukosi la kuongea endelea na mambo yako mamaaa!

 23. Anonymous

  January 28, 2014 at 11:56 am

  hellow dina
  nakuombea kila la kheri mungu akujaalie umalize salama hy safari yenye neema za Allah. sijui kwnn ukijibu hz blabla za watu unaniudhi. ukinyamaza nafurahi. mi binafsi nikikusema vby mungu atanilaani. dina hunijui ila umenisaidia. kama unakumbuka kuna mama alikuomba namba za aunt sadaka na namba za perfect, ndio mie. ninaona matokeo mazuri baada ya kumuona aunt sadaka. ahsante dina umenifundisha kuwa mwepesi kusaidia wengine.

  ushauri wng dina. muombe sana mungu hasa wakati huu wa ujauzito muombe akupe mtoto mwema. changamoto ninazopitia kwa mwanangu huwa zinanifanya niwaombee wazazi na vizazi vyote kwakweli.
  omba mungu hali hy ina changamoto nyingi na ni Allah pekeyake ndio ana majibu yote. kwa imani yangu ukiwa ktk hali hy basi dua yako inapokelewa haraka. nakuombea mamito.

  • dinamariesblog

   February 3, 2014 at 8:57 pm

   Hellow mamy…nafurahi kusikia ulipata msaada wa lile tatizo la mtoto..na anaendelea vizuri.Unajua na mie ni binaadamu kuna wakati unashindwa kujizuia kuongea hasa unapoona kuna mtu anajaribu kukuchafua ili yeye ajisikie vizuri.Ntajitahidi kukaaa kimyaa inapobidi.Asante sana kwa upendo wako na ushauri wako.

 24. Anonymous

  January 28, 2014 at 12:07 pm

  pia dina epuka kusema mama ni mungu wa pili. sio vizuri unakuwa unakufuru. mungu hana mshirika. nakubali mama kapewa daraja la juu kabisa na tunatakiwa tumuheshimu,tumpende na tumthamini. pia usiseme baba ndio baba angu na ndio "mama angu". usimpe baba sifa ya uanamke. samahani kama nimekukera ila kiimani sio nzuri. mie pia sina mama wala baba(mungu awalaze pema) na nilizoea sana hiyo misemo nikaja kueleweshwa.

  • dinamariesblog

   February 3, 2014 at 8:53 pm

   sawa sawa na nashukuru kwa maelekezo maana nilikuwa sijui.Nafurahi nikikoselewa katika hali ya kusaidana na kufundishwa pia.Ntaliweka akilni maana nilishazoea kusema hivyo.

 25. Byella

  January 28, 2014 at 12:22 pm

  Niliumia sana siku niliposoma article yako ya maisha bila mama.Hakuna kitu kigumu kama hicho hasa kwa mtoto wa kike.Nakuombea Mungu akupe mtoto wa kike,awe mama,dada,shosti,msiri wako,akufute machungu yote.Level ya juu ya mapenzi ni pale unapokuwa na mtoto.Namshukuru Mungu kwa ajili yako kwa kukupa faraja.I bet you will be so happy,utaona ukamilifu wa hali juu kwenye maisha yako.Mungu akujalie ujifungue salama,na mwanao awe na afya tele na alete baraka na furaha zaidi kwako.Much love

 26. Anonymous

  January 28, 2014 at 12:36 pm

  Luv u. Nakutakia maisha mazur na kijacho.

 27. Anonymous

  January 28, 2014 at 1:36 pm

  Hongera sana my Dina MUNGU wetu ni mwema akutimizie kila hitaji lo moyo wako, nakutakia kila la heri katika safari yako inayokuja ya umama muwe na familia barikiwa mpnz. Nimependa nywele zako hiyo umeweka ni Curl au wave? Nimependa.

 28. Anonymous

  January 28, 2014 at 2:56 pm

  I love u dina so much I'm still FIGHTING for getting pregnant I will be so happy when god bless me with Beautiful babies,Your article was so touched qeen I made me cry I love u. makigenda mak.

  • dinamariesblog

   February 3, 2014 at 8:50 pm

   Thank u so much…Mungu atakujaalia soon kwani ana wakati wake na mipango yake!

 29. Anonymous

  January 28, 2014 at 3:00 pm

  maneno yanakuja kwa vile kila wanapotaka kukuchomeka kwenye mambo mabaya na ya ovyo hupooooo,pole sana kila la kheri Insha Allah.

 30. Your Fan:

  January 28, 2014 at 3:17 pm

  Jaman Dina hujajua nimefurahije,mi nilikua siku zote nahisi abt wew na Ruben then nikawa nawish iwe kweli…yan nimefurah had bac,mnaendana kwakweli Mungu awajalie mfike mbali with love till the end mana kuna wengine wanafika mbali kwa mazoea….me love you so muuucch.

 31. Anonymous

  January 28, 2014 at 3:18 pm

  Dina am so happy kukuta upost humu. Ucjali mamy utajifungua salama.am so proud kuwa mama da dina ni raha sana kuwa mama!

 32. Anonymous

  January 28, 2014 at 6:02 pm

  Am so happy for u Dina,God bless you and your lovely family.

 33. Anonymous

  January 28, 2014 at 6:27 pm

  Hongera sana dina siku ya harusi yako mkijaaliwa nialike nije nidue kihehe kidogo

 34. Anonymous

  January 28, 2014 at 6:33 pm

  Hongera dina siku ya harusi yako ukijaaliwa nialike nije nidue kihehe kidogo jamani yani nakupenda sana

 35. Anonymous

  January 28, 2014 at 8:02 pm

  m always proud of u DINA wish to meet u one day,big up n may God bless u,love u much sisy.

 36. Anonymous

  January 28, 2014 at 8:04 pm

  Dina Mungu mwema Wala usihofu kila kitu kitakuwa sawa. Nakupenda.

 37. Anonymous

  January 28, 2014 at 8:12 pm

  Dina mamy,unaona ni jinsi gani unaona watu wengi wanavyokupenda na kukutakia heri humu ndani,sioni sababu ya wewe kukatishwa tamaa na watu wachache wasiokutakia mema,ishi maisha yako mamy,wengi tunakupenda na kukutakia heri na baraka tele,wewe kwangu ni zaidi ya Mama,wewe ni mwanamke shupavu mnoo!Mungu akiwa upande wako,hakuna atakayekuwa juu yako,mapenzi telee Dina!

 38. kiparis

  January 28, 2014 at 8:21 pm

  Kila mtu amekufurahia jaman inaonyesha vile tunakupenda Mungu akuongeze akupe kila lenye kheri nawe…amen

 39. Adela Dally Kavishe

  January 28, 2014 at 9:40 pm

  Hongera sana sana Dina mwenyezi Mungu akulinde katika kila jambo,

 40. Mariam

  January 29, 2014 at 8:14 am

  hongera sasa Dina nakukubali sana dada angu hata wakuponde vipi mimi nakupenda ni wajibu wakila m2 hasa mwanamke kama mungu kajalia uitwe mama usiwasikilize hao wanafki maana hawakusaidi na wala hawatakuja kukusaidia kulea mtoto wako kikubwa mungu akutangulie ujifungue SALAM

 41. Anonymous

  January 29, 2014 at 9:31 am

  Hongera sana mdada, hadi nakutamani. Nimefurahi kwa kurudi tena maana nilikuwa nafungua blog hii kila siku ckuti jipya nkaacha.

 42. Anonymous

  January 29, 2014 at 10:51 am

  Hongera sana dina mungu awe pamoja nawe

 43. Anonymous

  January 29, 2014 at 12:42 pm

  Dina hongera sn kwa kuwa jasiri hata me nakupenda sn usiwasikilize maneno ya watu kbs keep it up na Mungu akulinde na ujifungue salma

 44. francisco

  January 29, 2014 at 8:19 pm

  Na iwe kwako pia Mungu awe nawe kwa kila jambo,uende mbali

 45. Anonymous

  January 30, 2014 at 1:49 am

  ongera sana dada dina,mungu akusimamie ktk sfr yko iyo

 46. Joe

  January 30, 2014 at 6:21 am

  Veeeeeeeeeeeeeeeery goooooooooooooooooooood news to kick start year 2014! ALWAYS REMEMBER Mti wenye matunda ndio unaorushiwa mawe. GOD Bless you abundantly……… Receive ma biiiiiiiiig HUG….! Mdau wa AR.

 47. Anonymous

  January 30, 2014 at 10:50 am

  nakupenda sana mami maidha yako yananibariki sana

 48. Anonymous

  January 30, 2014 at 10:52 am

  Dada dina .ongera kwa kuwa mama kijacho.nafurahi kuwaona na Ruben.ww km mm cjaolewa il a ninamchumba Wangu na ss mm no mjamzito sijui nitaanzaje kumwambia mzazi Wangu nishauri.ninaishi mwenyewe nafanya kazi serekalini n.

 49. Anonymous

  January 30, 2014 at 11:23 am

  Kila lakheri nakutakia Dina Mungu akuvushe salama.Watoto ni baraka na pia huleta furaha ya moyo.Ninapenda vile uko mstaarabu hata kwa kile unachokiandika.You are such a good woman to admire.LOVE YOU-Mama Luqman

 50. Anonymous

  January 30, 2014 at 1:24 pm

  SIS DINA I LOVE U VERY VERY MUCH and GOD BLESS YOU..REMEMBER THAT U DON`T GROW WHEN THING A EASY U GROW WHEN U FACE A CHALLENGES.

 51. Anonymous

  January 30, 2014 at 3:22 pm

  Honngera sana kaza buti! Sasa ushawajua wabaya na wazuri.nawengine wanataka umaarufu kuptia watu wengine.mbona wao hawakuanza leo wamekua makachero kulinda wasivyo vijua pole yao!

 52. RUKY

  January 30, 2014 at 5:14 pm

  WAWAAAAA KUMBE SHEMEJI LETU NI HUYU WAWAAAO NIMEFURAHI HADI SANA ALL THE BEST JM DINA NAKUOMBA UWE UNATUPIA VIPICHA ISTARAM JM NAKUMISS PICHA TU ZA KAWAIDA..LOVE U FOR REAL MDOGO WANGU

 53. Rose SK

  January 31, 2014 at 12:34 am

  Lambda nimechelewa Ku comment lkn my dina unajua how much nipo name ww na tangu siku nimesikia ni mama kijacho nilifurah mno Kama vile ningesikia kwa ndugu yangu wa damu kila la heri mpnz na mpnz mpya ajae. Nakupenda sana nakuombea heri kila siku.

 54. Anonymous

  January 31, 2014 at 4:23 am

  Kuna siku ulisema kua hutaweza kuzaa kabla ya kuolewa sasa imekuaje tena….

 55. Anonymous

  January 31, 2014 at 4:23 am

  Kuna siku ulisema kua hutaweza kuzaa kabla ya kuolewa sasa imekuaje tena….

 56. Anonymous

  January 31, 2014 at 9:43 am

  huu mwanamke wa nguvu

 57. Anonymous

  January 31, 2014 at 12:41 pm

  Yes Dina, Mimi nikati ya watu wanaokumpenda sana hasa jinsi ulivyo, intellengent, organized, humorous and kind hearted. Mimi nimekumiss sana kwenye blog only to find out kua mjamzito! Congratulations Dina and Reuben! huu ndiyo wakati wenu. Celebs lazima wakuseme tuu, ila ziba masikio usisikie za watu wee fanya lako. Mungu awabariki.

 58. Anonymous

  January 31, 2014 at 2:28 pm

  Hongera sana dd dina nakupenda na mungu akijaalia siku ya harusi yako usikose kunialika nije nidue kihehe tumrudishe mama mkwe kwao

 59. Anonymous

  January 31, 2014 at 2:47 pm

  Hongera dada dina, ila ukijaliwa harusi usisahau kunialika nije nidue kihehe tumkumbushe mama mkwe nyumbani

 60. Habiba Simba

  February 1, 2014 at 5:23 am

  hi dina hongera sana kwa hatua hiyo uliyofikia,i really love u so much though hatujuani always nakuombea kwa Mungu akupe wepesi wa kila jambo lako, and hope u will be back with so much happyness.Love u mingi sana and siku moja tutaonana DINA MARIOS

 61. Anonymous

  February 1, 2014 at 10:13 pm

  God bless dina,god is with u,lov u so much,live long life…with ur family..

 62. emma kahere

  February 2, 2014 at 1:16 pm

  am happy for you my DINA,na nahisio huyo atakuwa beib boy.,may GOD be with you na ujifungue salama

 63. Anonymous

  February 2, 2014 at 3:03 pm

  Wish u all the best my lovely sister nakupenda sana Dina nimefurahi pia kuziona picha zako….Mungu atakusaidia utajifungua salama dadangu….

 64. Anonymous

  February 2, 2014 at 4:49 pm

  Mapenzi hutufanya tukubaliane na lolote lijalo mbele yetu, hakuna mwanamke asiyependa kufunga ndoa na ampendaye , ila wakati mwingine kuna chaguo ufurahishe dunia au ufurahishe nafsi yako, kila mmojawetu anasababu ya kutofunga hiyo ndoa , kwake hiyo sababu niya msingi ila kwa mwingine sio, mimi sijafunga ndoa kanisani wala kwa mkuuwa wilaya, nimeifunga moyoni mwangu natamani kuibariki hii tuloapiana wenyewe wawili. Tuna miaka kumi tukiwanamapenzi zaidi ya tulipoanza, kikubwa ndugu heshimianeni na kuzidi kukumbushana kuwa niagizo la mungu tufungendoa na tumfurhishe mungu zaidi ya wanadamu. Naombea wanandoa wote mungu awawezeshe kulitimiza agizo lake. Be blessed . Liz

 65. Anonymous

  February 3, 2014 at 6:49 am

  wapuuze dina wangu hao ndio binadamu,nimependa zaid jinsi ulivyodeal nao kimya,silence is the best weapon my dada that was soo breliant of you hun,mola akuongoze na akulinde utuletee kababy boy ketu nimeshakaona ha ha am kiding. HONGERA SANA.

 66. Anonymous

  February 3, 2014 at 8:29 am

  Hi Dina, mara nyingi watu hawapendi kuona mtu anapiga hatua kwenda mbele wengi wanapenda wakupite sasa ukimpita ndo hapo shuhuli.. Kila jambo lina wakati. Kwa hilo ndo wakati wake. Mungu ni kila kitu endelea kupiga hatua.. Hongera!

 67. Mama Eunice

  February 3, 2014 at 9:20 am

  Jamani nimesoma hadi nimehisi huruma, binadamu ndivyo walivyo, ni kweli walikuwa wanajaribu kukuchokonoa kwa kila hali lakini ulikuwa kimya na very strong. Mungu akupe wepesi katika maisha yako, Mungu huwa anasikia kilio cha kila mtu Dinna, kutokana na moyo wako wa upendo na huruma ndio maana akakutafutia furaha, hizo ups and downs ni za kawaida tu katika maisha kwasababu hata ukiwa nyumbani kwenu still migogoro sometimes huwa inatokea. Nakuombea kwa Mungu akufanye uwe mama bora kama ambavyo unawapenda watoto na kuwasaidia kila siku na ninaamini katika hilo. Hongera kwa kupata familia nzuri na yenye upendo tena unaonekana wazi. Ubarikiwe Dinna.

 68. faraja sulli

  February 3, 2014 at 9:33 am

  Hongera sana Dina, nimefurah kusoma hii post na nimejifunza kitu kikubwa sana hapa, Mungu akuongoze na akutangulie katika hili na ujifungue salama mtoto mwenye afya tele na aman nyingi maishani mwako mamii

  just 1 word to you and all readers "YOU CAN'T BE AFRIEND TO EVERY 1"

  All the best, love yu

 69. Anonymous

  February 3, 2014 at 11:37 am

  Nimefurahi leo sana tena sanaaaaaaaaa!!! God will bless you all and your plans also, akutangulieni katika kila pumzi mtayovuta ndani na kuitoa nje. Amen

 70. Anonymous

  February 3, 2014 at 12:21 pm

  sijapita humu siku nyingi sana maana ilikuwa kila nikipita hamna post mpya nilivyokuta hii binafsi nimefurahi sana hasa hapo KWENYE JIBU LA MJINGA hiyo ni silaha kubwa sana.
  NAKUOMBEA SANA KWA MUNGU UMALIZE KIPINDI KILICHOBAKI CHA UJAUZITO SALAMA NA UMPATE MTOTO MWENYE AFYA NJEMA. MTOTO AJE KUWA FURAHA NA FARAJA KATIKA MAISHA YAKO MAANA MTOTO NDIO KILA KITU.
  sikujiuliza baba ya mtoto ni nani niliposikia habari ziizokuwa zinaenea kuwa Dina ni mjamzito ila nilifurahi maana meamua kuwa mama na zaidi kila nikiangalia shughuli zako na unavyozihandle kweli niliona wewe ni mama bora sana na najua mtoto ataenjoy to the most.MUNGU AKUPIGANIE KATIKA KILA HATUA MPENDWA WETU

 71. Anonymous

  February 3, 2014 at 12:35 pm

  Da maneno yoye wamemaliza wadau, in short nimefurahi sana for you Dina, barikiwaa….x1oooo….

 72. Jane

  February 3, 2014 at 12:52 pm

  Nikili tu kuwa hakuna siku nilikuwa sipiti humu tangu ufungue blog mimi mdau wako, nikili kuwa sikumbuki lini mara ya mwisho ku comment, wish u all the best katika mwaka huu mpya na karibu katika maisha ya umama maana ni maisha mazuri asikwambie mtu. Hongera sana na Mungu akubaliki

 73. Anonymous

  February 3, 2014 at 7:16 pm

  DINA YOU MADE MY DAY HONGERA SANAAAA MPENZI

 74. Anonymous

  February 3, 2014 at 8:46 pm

  Dina Mungu akupe wepesi my dear ……nimefurahi beyond ur expectations all the very best

 75. dinamariesblog

  February 3, 2014 at 9:01 pm

  Helllo wapenzi…natamani nimjibu kila mmoja ila sitaweza,napenda niwashukuru kwa upendo wa pekee,ushauri,sala na dua zetu.Nimebarikiwa sanaaaa na nimefurahi pia.Nipo pamoja nanyi…nawapenda pia na Mungu awabariki sana!

 76. Anonymous

  February 4, 2014 at 5:57 am

  Hongera sana Dina, nimefurahi sana kwa maendeleo yako, yani unastahili my dear, nimekuwa nikikusikiliza mara nyingi yani uko tofauti, napenda unavojiheshimu, zaidi nakuombea kila la heri, Mungu awe ndio kila kitu kwako, uwe na familia nzuri yenye amani na baraka za Mungu, nakupenda sana, mimi kama binti nimejifunza mengi kutoka kwako natamani tuwasialiane my dear. pole sana kwa kutokuwa na mama lakini yote ni kumshukuru Mungu kwni hiyo ni mipango yake. all the best, love you, keep it

 77. Anonymous

  February 4, 2014 at 7:31 am

  dina
  one word for you

  JESUS HAS PUT SOMETHING IN YOU,utilize it till the last breath..una upendo sana wewe mdada
  we love you
  God loves you…

 78. Anonymous

  February 4, 2014 at 11:52 am

  hongera sana, ile story ya maisha yako ilinihuzunisha sana, nimefurahi kuwa umepata amani upendo na furaha hivyo ni vitu muhimu ktk maisha, mungu akutangulie na akubariki ktk kila jambo unalolifanya

 79. Anonymous

  February 4, 2014 at 12:14 pm

  Namefurahi sana my dear DINA 'hongere sana Mungu akutangulie kwenye maisha yako ya umama

 80. Anonymous

  February 4, 2014 at 12:37 pm

  Dinna umeshajifungua?je kama tayari umepata motto gani?

 81. Anonymous

  February 4, 2014 at 6:17 pm

  DINA!!!!! CONGRATULATIONS MOMMY-TO-BE!!!!! HUWA NAKUPENDA SANA INGAWA HATUJUANI, NILIKUWA NATAMANI UWE WIFI YANGU, NINA KAKA YANGU MWENYE TABIA NJEMA KAMA YAKO. BUT ITS OKAY NAFURAHI KUSIKIA HABARI ZAKO NJEMA. NAJUA UTAKUWA THE BEST MOMMY KWA MTOTO WAKO, NAMPA HONGERA SHEMEJI YETU PIA. I LOVE YOU DINA! MUNGU AKUBARIKI SANA.

 82. Anonymous

  February 5, 2014 at 7:20 am

  oooh Dina..mimi huwa napita humu kwa blog yako mara kwa mara. huwa nasoma na sicomment kitu chochote. ila leo, imenibidi niseme kitu. Tangu nakusikiliza kwenye kipindi cha leo tena, ulipompokea tu marehemu Amina, na tangu niliposikia sauti yako kwa leo tena. na kadiri siku zilivyokuwa zinaenda, nikawa najisemea mwenyewe moyoni au nikiwa kwenye gari nawaambia watu walionizunguka.''huyu dada ni wa tofauti sana, ana malengo makubwa sana, ana uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo na pia ana kibali, hapa nikimaanisha una kibali kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwa wanadamu. kwa maneno mengine, una authority kwenye ulimi wako, mengi unayoyazungumza, yanakubalika na kutendeka'' Kwangu mimi naweza kusema, ni karama ambayo si kila mtu anayo.

  Ubarikiwe sana dada. endelea kumtegemea Mungu ndio furaha yetu na mlinzi wetu mkuu. Usimwache. Mungu mwenyewe ndie atakayetupa upendo na furaha ya kweli. Kuna upendo na furaha ambayo hutoka kwa wanadamu, baba yako, akina zamaradi, mpenzi wako, LAKINI kuna sehemu itabaki ambayo hata mume/mpenzi wako hataweza kukutimizia. Upendo huu na furaha unatoka kwa Mungu tu. Unajua ni kwanini? kwa sababu Mungu husema naye pia ana wivu na hupenda kuwa karibu yetu. Kwahiyo kuna sehemu ya upendo ambayo utaipata tu kutoka kwake. Na ni muhimu mno mno mno. Hivyo, endelea kumwomba Mungu akupe upendo wake and furaha yake.

  Mwisho: Nakutakia maisha mema. Kaa ukijua tuko pamoja sana. tunaingia humu na kukusikliza kwenye radio. na nina imani siku moja tutakutana kwenye mihangaiko ya haya maisha. Na ni matamanio yangu ufike mbali sana. You are yet to count your blessings. I really admire you. You are an inspiration to all human kind and I think that is among the purposes of your life. Way to go. Bless you.

 83. Anonymous

  February 5, 2014 at 3:15 pm

  hongera sana Dina am very happy for you natamani kulia sana .yaani sina la kusema.Inshaallah ntakuja nikuone nikja DAR,mie ni msikilizaji wako mkubwa wa leo tena nipo Arusha

 84. Anonymous

  February 5, 2014 at 3:50 pm

  Hongera sana dina. Nafikiri siku mkitangaza ndoa watu watagombania kukuchangia na wengine watatoa vifaa badala ya hela. Nikifumba macho naona kwenye maono yangu watu watakaokuchangia usafiri, MC/Music sidhani kama clouds watakutoza hela, kuna watakaojitolea mavazi ya harusi na hata wengine watawapeleka honeymoon baada ya harusi. Kwenye msafara wa mamba kenge pia wamo. hivyo ni vyema ukachukua tahadhari hasa kwenye kamati itakayohusika usiweke watu wenye njaa wenye kutafuta 10%. Projection zangu zinaonesha kuwa una mashabiki kibao ambao uwezo wao kifedha ni dhoofu. Sisemi kwamba uwabague bali uangalie namna ya kuwa -accomodate na pia wao wajue kwamba starehe ni gharama nao wachangie kitu kidogo. Kwa maana hiyo minimum contribution iwe 50,000/=. Halafu ukumbi chukua Diamond mkubwa maana naona utakuwa na wageni wasiopungua 1,000. Mkijipanga vizuri hii inaweza kuwa fursa kwenu ya kuanza maisha ya ndoa huku mkiwa na mtaji wa biashara. Kuna jamaa yangu alifunga ndoa akatumia nusu ya hela alizopewa kwenye michango baada ya kutoa gharama zote bila kubana na nusu iliyobaki akajikuta imeangukia mfukoni mwake. Huo ni utabiri wangu tu ila nawatakieni kila la kheri wewe na Mr. SN

  • Anonymous

   February 11, 2014 at 4:03 pm

   hahaa ha Anonymous feb 5 2014 unamaono balaaa…..ila hukumsikia mwenyewe Dina alivyotuaga kwenye leo tena alisema hataki shughuli yake ya harusi iweee kuuuubwa

 85. Anonymous

  February 5, 2014 at 9:42 pm

  jamani dina nilikumisje my darling kila nikiingia naonana na pilau am happy if u r happy nilikumis hadi nahisi kuumwa ningekuwa mwnaume ningefanya juu chini nikuibe kwa hubby to beee

  nakutakia afya njema wewe na u,pendaye na kiumbe chetu .muhimu usijali watu wanasema nini binaadamu wameumbwa kwa kusema na sio kumcha m mungu maneno ya watu wachache yasikupe shida asilimia 90 watu tunakupenda sana mung akupe afya tele

  jamani nipe namie no yako niwe nakujulia hali

  mrembo wa kizamani

 86. Amina K

  February 6, 2014 at 12:45 pm

  LUV U SANA DINA, NAKUOMBEA KWA MWENYEZI MUNGU AKUJAALIE AFYA NA UZIMA UJIFUNGUE SALAMA TENA AWE MTOTO WA KIKE INSHAALLAH. NILIKUWA NAKOSA RAHA HUPOST KITU ILA LEO NINA AMANI SANA. PUMZIKA MWAYA SOMETIMES MAMBO YA BLOG YANACHOSHA NA KWA HALI HIYO ULONAYO YAHITAJI MAPUMZIKO,, ACHANA NA BINADAMU KWANI MIDOMO MALI YAO. ALL THE BEST

 87. Anonymous

  February 7, 2014 at 6:15 am

  Hello Dina. Hongera sana dia tupo pamoja am praying for u Mungu akusaidie ujifungue salama n upate mtoto mwenye afya njema. Ur friend Jane koromo naye nmeona fb amepata bby gal. B blessed.

 88. Anonymous

  February 7, 2014 at 12:00 pm

  Dina mungu akubariki sana nakupenda sana tunakuombea kwa Mungu utajifungua salama kabisa.Mungu akutunze mama .

 89. Anonymous

  February 10, 2014 at 1:51 pm

  Dina my love I pray for your safe delivery may it be ''natural'' may you have a peaceful family LAV YOU

 90. Anonymous

  February 10, 2014 at 6:31 pm

  Hongera sana dinna mungu ni mwema naami utayaweza mambo yote ktk yeye akutiae nguvu love u and all the best ktk mipango yako yote.

 91. Anonymous

  February 11, 2014 at 8:32 am

  dah, unazid kuninspire nakupenda sn dada angu pia napinda kazi zako natamani cku moja niwe km ww ktk kufanya kazi. Mungu akubariki sn kwan ww ni kioo kwangu, pia nakuombea kwa mwnyz Mung uwe na afya njema.

 92. Anonymous

  February 13, 2014 at 9:47 am

  Hongera sana dina Mungu akujaalie kila al kheri ujifungue salama,..jamani hakuna raha kama kuwa mama

 93. Anonymous

  February 14, 2014 at 2:12 pm

  Mimi love this sana… I love you both, May the almighty GOD Bless you and uwe na happy family….. Love you da Dina and b blecd

  Lydia

 94. Anonymous

  February 16, 2014 at 3:16 pm

  HONGERA SANA MPENZI FOR YOUR BABY BOY MUNGU AKUKUZIE DIA

 95. Anonymous

  February 17, 2014 at 7:30 am

  Yeeeeiiiii Hongera sanaaaa Dina…….! Utadhani ni mimi kwa jinsi nilivyofurahi

 96. Anonymous

  February 18, 2014 at 2:05 pm

  dada Dina hongera kwa baby boy, Mungu n mwema na akubariki uwe mama mwema kama ulivyo we mwenyewe! hongera sana mamii!

 97. Anonymous

  February 18, 2014 at 4:40 pm

  AM sooooo happy for you Dina mwanao nimemuona kwa instagram he is the real SAYUNI ''ZION'' kama jina lake umebarikiwa my dia namshukuru Mungu kwa ajili yako

 98. Anonymous

  February 19, 2014 at 7:44 am

  Hongera nyingi Dina, Mungu mwema aendelee kukupigania na kukutimizia kila hitaji ktk maisha yako. Tunakuombea.

 99. Anonymous

  February 20, 2014 at 11:58 am

  hongeraaaa dina kwa kupata mtt(baby Zion)mungu akukuzieee lv u sanaaaa

Leave a Reply