Uncategorized

MAPISHI:BBQ YA NYUMBANI(NYAMA CHOMA)

By  | 
Mimi nyumbani kawaida hata kama kuna housegirl chakula napika mwenyewe.Hasa cha usiku na weekend pamoja na tumbo langu bado nimo.Sasa jumapili siku hizi siingii jikoni nina wanaume ndio wanahakikisha mchana tumekula na usiku tumekula kama kuna lolote ntasaidia ila kila kitu wanafanya wenyewe.Ndio tunafanya nyama choma at home.
Nyama ya mbuzi mbavu na inawekewa marination ya kawaida tu ili kuilainisha na kuipa ladha kabla ya kuichoma.
Tunatumia tangawizi,kitunguu saumu,ndimu au limao na chumvi.Nyama inapakwa hivyo vyote kisha inawekwa kwenye fridge kama lisaa hivi ndio inaanza kuchomwa.Inaweza kuwekwa hivyo vyote hata usiku ikalala kwenye fridge kesho yake ikachomwa.
Kuku nao huwekwa marination ila hii ni kitunguu saumu na limao na chumvi.Wakati mwingine tunaweza kufanya chicken tandoor kama tunataka ile ladha ya pilipili.Mikono ni ya my brother in law akishughulika.
Hii ni mbuzi ikiiva taratibu…mdogo wangu yupo vizuri kwenye kuchoma mbuzi na shemeji yangu yeye kwenye kuku.
 Mambo yako tayari kuliwa..
Mdogo wangu akitengeneza kachumbari.
LUNCH:Mbuzi choma,ugali,kachumbari na mboga ya majani ya maboga.
DINNER:Kuku choma,ndizi tamu za kukaaanga na kachumbari bila kusahau chachandu.
Jumapili ikawa imeishia hapo.Kama ipo ndani ya uwezo wako unaweza kujibajeti vizuri ukafanya nyumbani.Sio kwamba unanunua mbuzi mzima mbuzi kilo mbili hata moja inatosha kulingana na ukubwa wa familia yako.Kuku mmoja,wawili au watatu pia wanatosha.Sio mpaka tukale kuku au mbuzi bar hata nyumbani vinawezekana tu hasa baba akiwa ndio kashika usukani.

28 Comments

 1. Anonymous

  February 11, 2014 at 1:19 pm

  Hongera Dina kwa kutuletea pishi zuri itabidi niliandae weekend hii
  Big Up kwa wadogo zako wako poa ktk mapishi

 2. teressa simon

  February 11, 2014 at 2:57 pm

  Hongera sana Dina, Pishi ni zuri napenda mno nyama choma, jpili nitaanda kwa ajili ya familia

 3. Anonymous

  February 11, 2014 at 3:07 pm

  dina naomba unialike my dear..daah nakuonea raha

 4. Anonymous

  February 11, 2014 at 3:45 pm

  uwii Dina umenitamanishaje sasa hizo nyama jumamosi lazima niandae na mimi swali nyama unazichoma na foil paper au unaziweka kwenye foil baada ya kuiva ili ziendelee kuiva taratibu? nihabarishe mwenzako pleease mpenzi wangu

  • dinamariesblog

   February 11, 2014 at 6:32 pm

   ZIKISHAIVA NDIO UNAWEKA KWENYE FOIL ILI ZISIENDELEE KUKAUKA…NAKUTAKIA MAPISHI MEMA UNITUMIE PICHA.

  • Anonymous

   February 13, 2014 at 9:30 am

   Asante sana mpenzi nitakujuza zangu zimetokelezea vipi

 5. Anonymous

  February 11, 2014 at 3:59 pm

  safi sana Dina

 6. Anonymous

  February 12, 2014 at 7:18 am

  Nie

 7. Anonymous

  February 12, 2014 at 9:09 am

  Dina mi nakupendaga bure tu
  hivi mtu akitaka kuja kukutembelea home kwako anaruhusiwa?
  i wish to see your home

 8. Anonymous

  February 12, 2014 at 10:32 am

  Duuuuu! leo usiku lazima niote nakula uhu msosi, atariiiiiiiiiiiiiiii

 9. faraja sulli

  February 12, 2014 at 10:52 am

  yaan Dina nakupendaga sana na always napenda life style yako for sure. Mungu akujaalie afya tele ujifungue salama na urejee katika hali yako ya kawaida na mwanao akiwa na afya tele, nguvu, hekima na akili za kutosha

  nyama hyo nitaikula jmos hii, nitakukaribisha

 10. Anonymous

  February 12, 2014 at 2:05 pm

  Hadi nimemeza mate nikajihis kama nakula daaaaa

 11. Anonymous

  February 12, 2014 at 2:46 pm

  Uwii bora umesema mapema, maana nahisi ningeweka moja kwa moja kwenye foil ndo nikachoma.

 12. Zakia Mustafa

  February 13, 2014 at 8:06 am

  Ninachopendaga kwa mwanamke ni kupika Dina huwa naambiwa wewe ni mpishi mzuri sana big up.! Itabidi nimwambie shost wako Debora aje kuonja msosi yupo huko.! Yum yum

 13. Anonymous

  February 13, 2014 at 11:03 am

  Na mimi natamani sana nichome, ila Dina jiko langu ni la kawaida siyo special kwa nyama choma. Je litafaa kweli mi sina familia kubwa nipo na Hubby na house girl. Pliz nishauri.

 14. Anonymous

  February 13, 2014 at 2:58 pm

  uwiiii nimependa jamani..mbuzi napata wapi mbichi au ndio mpaka niende vingunguti??nijuze fasta nataka nichome jumamosi..

 15. sylvia

  February 16, 2014 at 6:23 pm

  Safi sana dina.umenihamasisha sana.nakumis jaman radion .nakuombea heri na salama.

 16. Husna

  February 17, 2014 at 8:42 am

  Habari da Dina samahani naweza choma kwa oven instead of mkaa maana cna jiko kama lako la kuchomea jiko langu la mkaa ni dogo sana

 17. Anonymous

  February 20, 2014 at 11:32 am

  nimetamanijeee da dina,na me ntajaribuuu

 18. Anonymous

  February 21, 2014 at 9:24 am

  hi dina,inapendeza sana sana hongera kwa hao wanaume pia kushughulika wapi nchakalih

 19. Anonymous

  February 21, 2014 at 5:13 pm

  Imetulia, safi sana

 20. Anonymous

  February 27, 2014 at 5:10 am

  Miss you DINA cjakusikia siku nyingi

 21. Amina k

  March 13, 2014 at 6:02 am

  mpaka raha kuwa na wataalam wa nyama.Asante mamii kwa kutujuza nasi tutajitahidi majumbani mwetu. Nakutakia kila la kheri ujifungue salama tena awe baby girl.

 22. Anonymous

  March 25, 2014 at 1:13 pm

  SAFI SANA NIMEIPENDA KWA KWELI, SASA HIYO STRAINER YA MAFUTA NIMEIPENDA SANA, NITAIPATA WAPI? IMECHUJIWA NDIZI.

 23. Anonymous

  April 1, 2014 at 11:27 am

  Hongera Dada Dina kwa kutuletea baby boy jamani, nakumissije humu ndani, ukija najua utakuja nakishindo kila siku naangalia kama umeweka kitu kipya. ila najua malezi ya mototo hasa wa kwanza lazima utulie vizuri. Nakutakia kila la kheri katika hayo malezi.

 24. Anonymous

  April 13, 2014 at 1:39 pm

  Ndoa lini ?

 25. Anonymous

  April 23, 2014 at 5:00 pm

  Nikupongeze kw mambo mazuri unarudi lini kazini tumemic kazi yako pia kweny blog hutupi Habar zipo za zaman tu

Leave a Reply