Uncategorized

VIPINDI VYA TV NINAVYOTAZAMA WAKATI NIPO NYUMBANI.

By  | 
Wakati huu ambao nipo nyumbani nautumia vizuri kuangalia vipindi vingi vya tv ikiwemo hivi hapa.
Kwa wale waliounganishwa na DSTV mtaweza kuona vipindi hivi.Body Mind and soul cha mchungaji TD Jakes ni kati ya vipindi ninavyovifatilia sana najifunza na pia napata ideas mpya.Hapo huzungumzwa mambo mengi yahusuyo maisha yetu ya kila siku kiroho,kimwili na kiakili.
Oprah Winfrey ni mwanamke ambae ameweza kuinspire millions of people especialy women hapa duniani nikiwemo mimi.
Nimekuwa namfatilia kwa miaka mingi sana na alinisukuma kitambo kuanzisha talk show lakini naona muda bado haujafika ukifika nitafanya hivyo.
Jumapili huwa naangalia vipindi vyake vingi tu super soul sunday,oprah next chapter na oprah behind the scene.
Kupitia Oprah behind the scene unaona ni jinsi gani ana team kubwa ya production nyuma yake.Ana maproducer ambao kwa miaka yote wamehakikisha akirusha kipindi lazima kiache historia.
Hii imenifanya niumize kichwa sana.Hatuwezi kuwa kama Oprah ila tunaweza kujifunza kupitia yeye.Vipindi vyetu tunavyofanya ukiwa wewe ndio mtangazaji basi vitu vingi utakuta unaviwaza wewe na wakati huohuo unazalisha wewe mwenyewe hakuna team ya producers nyuma yako.Hata vijana wanaosomea journalism wengi wanataka kuwa watangazaji hakuna mtu anataka kuwa behind the scenes kama mzalishaji.Lakini hii nayo ni ajira ila inataka uwe mbunifu na mwenye upeo wa hali ya juu wa kugundua madini yanayoweza kupelekwa hewani.Ujitume na uwe na upeo kumzidi hata mtangazaji husika,je wangapi wanataka kuwa wazalishaji?una vigezo?
Steve Harvey Show…Steve ananifurahisha sana na wageni wake,ucheshi wake na topics anazozileta kwenye show.Steve talk show yake amewalenga wanawake nimependa idea ya yeye kuwa mwanaume lakini anafanya show target yake ikiwa ni wanawake.Akiwa ni mwandishi wa kitabu kilichouzwa sana mwaka juzi THINK LIKE A MAN ACT LIKE A LADY.
Napenda kipindi hiki maana mie mwenyewe nafanya kipindi kinachomlenga mwanamke kwa hiyo najifunza zaidi japo mie nipo radio.Talk show inataka uwe live na wale waliopo kwenye show,wageni unaowahoji na bila kusahau anaekuangalia nyumbani kupitia luninga yake very challenging Steve yuko sawa kwa ucheshi wake lazima niangalie kipindi chake.
 
Haya kama nilivyosema nipo tu home nitakuwa naandika yale ninayoyaona katika mazingira yangu.

14 Comments

 1. Anonymous

  February 4, 2014 at 8:43 am

  Poa mamy,but nakumiss sanaaaa…

 2. Anonymous

  February 5, 2014 at 6:45 am

  dah….Dina unaniispire…that is all I can say…Mungu akujalie ujifungue salama,mm nalea kichanga change now…this jmoc anatimiza two months Mungu akipenda…..Mdau Jane K

 3. Anonymous

  February 5, 2014 at 6:50 am

  halaf uliwah andika kipindi cha nyuma kuwa papai bichi linaivisha nyama ya ng`ombe ndani ya dakika 5,mbona mm haikubal?….dau Jane K

 4. Anonymous

  February 5, 2014 at 7:12 am

  nampenda sana oprah, she chaming, kindly, smart and strong beautiful and amazing, ki ukweli namuadimire ile mbaya ni mwanamke shupavu ni mfano wa kugwa, tazama anamiaka 60 utafikiri ana 40

 5. Mama 2 (Mrs M)

  February 5, 2014 at 12:05 pm

  Natumaini unaendelea vizuri Dinna! kweli kabisa hiyo ni ajira tosha, kama inawezekana wajitokeze vijana wa aina hiyo, ni kweli watawasaidia watangazaji.

 6. Anonymous

  February 5, 2014 at 8:37 pm

  Yan Dina me Steve Harvey show ndo inanibamba na kila cku nina kitu najifunza kwa hii show .Nikii kosa hua nackia vibaya kabisa. He is an inspiration na ni one of my male role model vile nmelelewa na mama tu.

 7. Anonymous

  February 5, 2014 at 9:01 pm

  Dada dina naomba uniandikie hivyo vipindi vinapatikana namba ngapi dstv pliiiiiiiiz kwani na mm npo tu hom nasubiri km ww nimeboleka sana

 8. Anonymous

  February 6, 2014 at 9:20 am

  Dina vipindi hivyo vyote naangalia wala hujakosea, ila umeshau na Queen Latifah Show ni kizuri sna pia, bila kusahau kutune Telemundo pia kwa tamthiliya za kujifurahisha. Nakutakia kila la Kheri

 9. Anonymous

  February 6, 2014 at 12:36 pm

  Mic u mbaya Tayari. Hata ya home yanavutia pia.. kuliko kua kimya kabisa

 10. Anonymous

  February 6, 2014 at 7:10 pm

  Tv ni nzuri ikiwa unajua nini cha kuangalia kama hivyo umeselect good channel. Mi pia nipo home nasubiria any day nitaingia labour, ila muda wangu mwingi naitumia kusoma vitabu hasa vya leadership,motherhood, marriage and christian books. Nakushauri pia jaribu kusoma books vitakusaidia sana katika career yako na personal growth.

 11. Anonymous

  February 7, 2014 at 10:09 am

  Jamani angalia na channel ya food ili uwe unaongezea recepies mpya za mapishi.

 12. MOJAONE

  February 7, 2014 at 1:13 pm

  Mie sina zaidi ya mechis tu.

 13. Anonymous

  February 9, 2014 at 8:40 pm

  mamii uko juu. Weka picha yako ulvo na mimba nikuone wangu. I adore u.

 14. Anonymous

  February 27, 2014 at 8:32 am

  I adore you sis Dina, ninauhakika ukianzisha talk show itakua nzuri sana na itapata wapenzi wengi kuliko unavyodhani,sababu naamini unakipaji chako cha pekee.

Leave a Reply