Uncategorized

Mkate wa Beef Mlo Kamili – Tengeneza Kinyumbani

By  | 
Leo naonyesha mapishi ambayo mara nyingi tunakula tuendapo katika restaurant kama Subway; Sasa hapa naonyesha namna ambayo unaweka pata taste tamu zaidi hata ya kule restaurant. Pishi hili lahusisha mkate ( French bread) na beef.

Mkate ni wa kununua ila ipo siku nitawaonyesha namna ya wewe mwenyewe kuweza kuupika. 

MAHITAJI 
  •  Nyama steak nusu kilo 
  • Vitunguu maji viwili 
  • Pilipili Manga 
  • Mixed Hearbs 
  • Pilipili ya unga 
  • Cheese kwa wale wanaotumia 
  • Chumvi 
  • Unga wa ngano vijiko viwili 
  • Butter kijiko kimoja 
JINSI YA KUANDAA 
Hatua ya kwanza kabisa ni kuchemsha nyama. Nyama usiikate kate chemsha ikiwa nzima nzima – weka maji, weka mixed hearbs kijiko cha chai kimoja, weka pilipili manga kijiko kimoja cha chai, weka pilipili ya unga nusu kijiko cha chai. Sasa iache nyama hii ichemke kwa muda wa kutosha kabisa hadi itakapokuwa imelaininka kabisa. 
Nyama ikiwa tayari icharange kwa style ya slices – ikate kwa ulalo hivi yaani mapande makubwa ila membamba.

Sasa chukua chombo zaidi iwe flampeni weka kwa moja kisha weka kijiko kimoja cha butter na unga wa ngano ikaange hadi ngano iwe kama inakuwa na brown hivi – kama ukiona inashika sana chini unaweza ongeza ile supu uliochemshia nyama. 

Kisha weka vitunguu na pilipili hoho , kisha weka ile nyama – vikiwa vinachemka ongeza pilipili manga na pilipili ya unga kidogo pia chumvi kama ile ya supu haitoshi. 

Kumbuka hii souse sio iwe maji maji so ikuwa ni nzito tu kama ambavyo nimeonyesha katika video ( tafadhali angalia video kwa kuelewa zaidi)

Ikiwa tayari chukua mkate wako upasue katikati weka nyama , pamoja na vitunguu maji, vibicho au roasted , weka cheese , na majani ya giligilani kwa aroma zaidi.

Tayari endelea kuenjoy mkate wako na beef. 

Kwa maelezo zaidi ingia: 

Leave a Reply