Uncategorized

BYE BYE LEO TENA

By  | 

Wapenzi wangu najua kila kitu kilianzia kwenye leo tena hadi wewe kuamua kufatilia kazi zangu na kila kitu ninachofanya.Ila wanasema safari moja huanzisha nyingine ndivyo ilivyo kwangu.
Baada ya muda wa miaka nane kuongoza leo tena na mie kuilea kwa kila hali kuhakikisha inakuwepo.Leo tena ilikuwa maisha yangu nikilala,nikiamka,nikiwa barabarani ili mradi niwe na jambo kwa msikilizaji wangu kila siku.Iwe ni segment mpya,topic,wimbo,jingle,yaani chochote ambacho naona kitanogesha kipindi.
Nilichukua likizo ya martenity na niliporejea nikaambiwa dada tunakuhamishia sehemu nyingine,TV.Daah haikuwa kazi rahisi kukubali na kuipokea niliona daah itakuwaje jamani mbona leo tena ndio kila kitu kwangu.
Nikaelezwa vile ofisi ina malengo makubwa na kipindi kipya nitakachoanzisha ambayo siwezi kuyaanika hapa lol basi kidogo kidogo nikaanza kuelewa somo na sasa nipo tayari.Kuna wale ambao bado mnaendelea kuulizia kwa nini hamnisikii ukweli ndio huo kwa sasa sipo tena kwenye leo tena najiandaa na kipindi changu kipya cha tv kitakachoruka clouds tv hapo baadae.
Japo nina changamoto ya mwili mmenenepa mie ila kila kitu kitajiset mbele ya safati.Nikiwa najiandaa na kipindi kipya pia najiaandaa na ule utaratibu wangu wa kusaidia watoto yatima kupitia dada dina cares ambayo itakuwa ni mwezi ujao.

Najua tayari nina mawazo yangu ya nini nitafanya kwenye hicho kipindi lakini pia naomba nikuulize.Ungependa kuona nini kwenye kipindi changu cha tv?

24 Comments

 1. MWARUBADU

  June 4, 2014 at 1:30 pm

  NAKUKUBALI DADA DINA NA NAPENDA KAZI ZAKO MIMI KAMA MSHABIKI WAKO TUTAKUWA PAMOJA

 2. Anonymous

  June 4, 2014 at 1:59 pm

  hongera Dina kwa kila kitu.. kwenye kipindi chako uwe na mchanganyiko wa vitu ili kisiboe.. maisha kwa ujumla km:kipengele cha mapishi.kipengele cha mahojiano na watu maarufu based kwenye maisha yao ya kila siku.na kumshirikisha Gea kwenye hekaheka za mtaani Mara moja moja. na kutoa elimu kwa jamii kupitia mifano mbalmbal..!all the best I know you have better ideas already

 3. veronica chuwa

  June 4, 2014 at 2:57 pm

  kwanza nakupongeza sannna kwa hatua ambazo umepitia mpaka ulipo, kikazi na uzazi haya mambo si mchezo ni jambo la kumshukuru mungu sannna.
  pili katika kipindi chako cha tv nategemea sanaa kukuona ukijiamin na kutupa extra katika yale tuliyokuwa tukiyasikia kwenye radio mf. heka heka na nyumbani kwetu leo.
  nakupenda sanna my Dinah.

 4. Anonymous

  June 4, 2014 at 4:32 pm

  Dina nilibyoskia unahama leo tena roho iliniuma mnoo ila no way out sasa ss ambao tuko nje ya dar tunaomba vpind vyako viwekwe pia you tube tukuone mi nakuamini utaweza tu hop sku moja tutakuona BBC DW tv …ukihost huko coz wewe ni wa level hizo

 5. Anonymous

  June 4, 2014 at 5:02 pm

  Hello Dina,
  hongera sana kipenzi kwa mtoto pia kwa kuhitimisha salama safari ya Leo tena. Nakutakia kila lakheri kwenye kipindi kipya. Nakuamini na najua kitaneda vyema. Binafsi sikua msikizaji wa Leo tena so natumai kuwa hiki cha tv kitanigusa zaidi nikitazame. Good luck and all the best to you.nilikumiss sana humu bloguni aisee.

 6. Anonymous

  June 5, 2014 at 5:29 am

  sina mengi ila ningependa kuona unafanya vizuri kama ilivyokua LEO TENA Nakutakia kila la kheri ktk kipindi chako kipya GOD BLESS YOU

 7. Anonymous

  June 5, 2014 at 6:42 am

  kila la heri dada ila tunakukumbuka sana

 8. Anonymous

  June 5, 2014 at 9:54 am

  Kwanza hongera sana mungu akutangulie katika malezi ya mtoto na familia yako kwa ujumla.Pia ni vema ukaendelea na dada dina carees pia uongeze nguvu katita kupigania haki za watoto na wanawake katika kufichua maovu maana hiki kazazi hata kwa mungu ni mtihani

 9. Anonymous

  June 5, 2014 at 10:21 am

  Hongera yote kheli mama

 10. Josejully

  June 5, 2014 at 7:43 pm

  Kwanza hongera kwa kupata baby boy,mungu akubariki ww pamoja na baba mtoto Wako na mtoto nae.Mm ningependa kuona ukutetea haki za wanawake pamoja na haki za watoto,Vilevile usiache kutoa zile tuzo za mwanamakuka pamoja dada bora wa kazi za nyumbani.

 11. Anonymous

  June 5, 2014 at 10:02 pm

  Dada Dina hongera sana. Mm ningependa uzungumzie suala zima la unyonyeshaji wa watoto. Mm nipo martenity ss ila nimegundua kuna changamoto sn ktk hili hasa kwa wale wamama wanaohudhuria hospitali za private.

 12. Francisco

  June 6, 2014 at 10:23 am

  Napenda kuona ukiendelea kumleta aunt Sadaka kwenye kipindi chako cha TV ndio segment iliyokua inanifanya nikusikilize everyday

 13. Anonymous

  June 6, 2014 at 12:40 pm

  ujgjghhddddddg

 14. Anonymous

  June 6, 2014 at 12:48 pm

  Hongera sana napenda changes.nategemea utakuwa oprah watz

 15. Anonymous

  June 6, 2014 at 1:40 pm

  Nilisubir kwa hamu zote nikijua utarud tena baada ya likizo ya uzazi ila sio mbaya tutakufuata huko huko

 16. nas Haulliers

  June 6, 2014 at 2:06 pm

  mamy hongera kwa kuwa mama kila la kheir kwenye malezi mema ya familia ,siku hizi nimekuwa mvivu hata kusikiliza leo tena nilizoea sana kukusikiliza ila yote kwa yote mwisho wa siku lazima upige hatua mi naomba kwenye hicho kipindi kipya ingewekwa segment ya fichua maovu kwa jamii huku yule mfichuaji akilindwa maana dada dina jamii yetu imejaa maovu sana ,roho za watu zimebadilika ,unyama umekuwa mwingi kuliko ubinadamu .Eeeeee mungu tunyooshe kwenye mema .ameen.

 17. dabrat abdul

  June 6, 2014 at 2:09 pm

  mamy hongera kwa kuwa mama kila la kheir kwenye malezi mema ya familia ,siku hizi nimekuwa mvivu hata kusikiliza leo tena nilizoea sana kukusikiliza ila yote kwa yote mwisho wa siku lazima upige hatua mi naomba kwenye hicho kipindi kipya ingewekwa segment ya fichua maovu kwa jamii huku yule mfichuaji akilindwa maana dada dina jamii yetu imejaa maovu sana ,roho za watu zimebadilika ,unyama umekuwa mwingi kuliko ubinadamu .Eeeeee mungu tunyooshe kwenye mema .ameen.

 18. dabrat abdul

  June 6, 2014 at 2:16 pm

  Hongera mama kwa kuwa mama wa familia na kila la kheir kwenye malezi ,mamy mi naomba kwenye hicho kipindi kuwe na segment ya fichua maovu kwa jamii maana dada dina jamii yetu tunapoelekea sipo maovu yamezidi mi naomba mamy lkn tu mfichuaji wa maovu asiwekwe wazi kwa ajili ya usalama wake.mwisho Eeeeee mmunuu tuongoze kwenye mema na tuvue na roho za ushetwani.

 19. Rehema-Dodoma

  June 9, 2014 at 7:51 pm

  Mungu alishakuumba kwa ajili ya kutetea akina ma na watoto, wanyoge, wanaoonewa na watu anaofanana na hao, hata kma utafanya kipindi katika tv ustoke nje na hivyo vitu. nakuomba sana, umewasaidia sana wanyonge

 20. Anonymous

  June 12, 2014 at 9:05 am

  Hi Dinah, Kwanza hongera kwa kila kitu jamani, kuwa mama, kwenda kwenye TV shows n.k. Ila roho imeniuma kukukosa leo tena ile mbaya, but all in all yote maisha na lazima tusonge mbele.
  Kwenye vipindi vyako usikose kuwa na kipindi na Aunty Sadaka. Ki ukweli huyo mama mimi namkubali kazi zake na mimi ni mojawapo kati ya wale ambao wamesaidiwa kwa namna moja au nyingine na Aunty Sadaka ku move on na maisha baada ya kupata msiba wa aliyekuwa mchumba wangu. Dina, nakupenda sana na Mungu aendelee kukuongoza katika kila jambo.

  All the best Mama Zion.

 21. Anonymous

  June 12, 2014 at 11:58 am

  Hongera Dina Kwa mtoto wa kiume! DIna please jitahidi uwe na interesting things Usije chuja maana radio yenu ni tofauti na Tv yenu … vipindi vyenu vya TV Bado kidogo soo wewe ndo ujiweke sawa.. all the best my dear!

 22. Anonymous

  June 19, 2014 at 9:50 am

  Sijui hicho kipindi kitakuwa kinahusu nini ila nahisi ni Talk show, basi sijui utaiwekaji ila watoto kuanzia miaka 0 na kuendelea wamesahaulika sana ( unyoyeshaji, vyakula, mama ku-handle mtoto) pia ukuaji wa tabia za watoto wazazi wawalee vipi watoto wao ili kujenga taifa zuri lijalo. Vijana wanao kuwa haswa ktk huu ulimwengu wa fujo, hili jambo wanasaikolojia wasikose. Yaani kipindi kihusu uhalisia wa jamii yetu, mambo ya kuhoji wasanii sijui watu maarufu kuja kuongelea maisha yao ya uongo na kweli vipindi vilivyopo vya hayo vinatosha. Pia kawepo kasehemu ka mapishi ya ki kwetu kwetu. Napenda kuwasilisha hoja

 23. Anonymous

  June 19, 2014 at 7:34 pm

  Hongera sana mama Zion….maisha ni hatua na wewe unaoiga hatua nyingine sasa kutoka redioni mpaka kwenye kideo…ila my worry tv isije ikakupoteza maana sio wote wanaangalia tv na itategemea kipindi chako kinarushwa lini,,,,kisijerushwa jumatano mchana wengi wako kwenye mihangaiko ya maisha,,,,,redio mtu hata akiwa kwenye daladala anasikia sauti yako…hata akiwa ofisini anasikiliza hata kwa simu sasa tv daaaaah tutakumiss dada…….na hivi ving'amuzi wengine ndio hatutakaa tukuone. Well me nakutakia heri….mafanikio tele natumaini huo ni mwanzo wa mafanikio yako mengine makubwaaaaaa

 24. Christian Bwaya

  July 12, 2014 at 5:35 pm

  Hongera sana dada kwa kupanda ngazi. Tunatarajia makubwa kwenye kipindi chako kwenye TV!

Leave a Reply