Uncategorized

HELLO WAPENZI KUTANA NA KING ZION

By  | 
Hello wapenzi wangu habari za toka mwezi january daaah nimeadimika mpaka basi.Leo nikasema hata wacha nije hapa kuwasalimu na niwaletee kijana wangu kwa wale ambao mnanifollow insta gram mshamuona.Kama bado hujanifollow natumia dinamarious.
Last time nimepita hapa nilikuwa sijajifungua bado ndio zilikuwa dk za mwisho mwisho.Nashukuru Mungu kwa uwezo wake nilijifungua salama mwanangu Zion.
Nilitamani sana kujifungua kawaida ila daktari akaniambia mtoto mkubwa nisijaribu kurisk maana sitapewa tuzo ya kuzaa kawada.Dk za mwisho ulta sound ilionyesha ana kg 4.9 nikalazimika kufanyiwa oparation jumapili ya tarehe 16 feb mida ya saa saba mchana ndio nikakutana rasmi na Zion toka hapo maisha yangu yamebadilika kabisa naitwa mama Zion.Hata kublog nilikuwa najionea shida tu nikasema muda ukifika nitapita huko tu.
 
Thanks to my mama mkwe mama yake na Reuben aliacha kazi zake zoote akaja kukaa na mimi toka mwezi wa kumi na moja mwaka jana na mpaka Zion alipotimiza miezi mitatu ndio akaondoka.Amenilea amenihudumia vyema as if mimi ni mwanae kabisa na tumekuwa marafiki sana tunapiga story na kugossip lol.Ni mwanamke wa pekee sana yaani nilikuwa najihisi nipo na shost wangu.Ni mama anayeishi katika misingi ya dini kila jumatatu lazima aende bible study akirudi kesho yake lazima aanze kunipa na mimi somo nimejifunza mengi kutoka kwake kiukweli.
Baba mtu yeye alichukua likizo kabisaaa ya partenity kuhakikisha anakuwepo kwa kila hatua kumbembeleza akilia kumchange akiokojoa au kujisaidia n.k
Japo ni mara ya kwanza hajataka kupitwa na chochote he is a good father kwa Zion na wanaelewana mno.
Namshukuru Mungu naendelea vizuri na maisha mapya ya umama.Naomba aniongoze zaidi kwa kunipa imani,hekima,maarifa,subira katika malezi.Nashukuru kwa sala zako na dua zako nilifanikiwa kujifungua salama maana kila hiyo siku ilivyokuwa ikikaribia nilikuwa napata mawazo itakuwaje.Ila kwa Uwezo wake na neema yake Mungu baba nikapita salama japo kwa kisu.
Haya wapenzi nitakuwa napita pita humu nimerejea kidogo kidogo sio saaaana.Kwa mambo mbali mbali kama kawaida yetu yagusayo maisha ya kila siku.

60 Comments

 1. Anonymous

  June 2, 2014 at 9:34 am

  mzuri jamani ni bonge la toto, u made ma dear

 2. Anonymous

  June 2, 2014 at 10:06 am

  Hongera Sana kwa mtoto nzuri… Hadi raha mwenyezi Mungu awabariki katika malezi ya mwanao jamani.

 3. Anonymous

  June 2, 2014 at 11:15 am

  Hello Dada Dina,

  Am so happy you are back……n baby wako ni mcute sanaaaaa. Congratulations
  me nilikua nikipita hapa kila mara kuchungulia kama umerudi……………….and finally you are here.
  Plz we will be grateful kama utakua una share maisha yako mapya ya umama na sisi ili tujifunze mengi kupitia kwako.

 4. Anonymous

  June 2, 2014 at 11:31 am

  Yesu ni mzuri dinna Marious, akubariki sana nakupenda na Mungu akupe familia nzuri yenye amani na furaha ubarikiwe sana

 5. BETTY SENIOR

  June 2, 2014 at 11:49 am

  Dear Dinah, hongera sana na karibu kwenye chama cha familia na mama wazazi. Hebu chukua dakika kadhaa, utafakari tofauti unayoihisi ulipokuwa huna mtoto na baada ya kuwa na mtoto, unajisikiaje na je unaweza kuielezea hiyo furaha kwa maneno machache walau?

 6. Anonymous

  June 2, 2014 at 12:27 pm

  HONGERA DINNA KWA KUKUZA HONGERA SANA

 7. Anonymous

  June 2, 2014 at 12:37 pm

  Mwanao mzuri mpenzi hongera sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa umeleta HB wa ukweli Mungu akukuzie mamiiii penda nyie wte….

 8. Anonymous

  June 2, 2014 at 12:56 pm

  Mashallah Dina mungu atukuzie mtoto so qute kanakuwa na kupendeza jamani hadi raha. Mdau wa Norway.

 9. Anonymous

  June 2, 2014 at 1:00 pm

  Hongera sana Dina..mtoto Zion ni mzuri mno..familia nzuri sana..Mungu azid kuwabariki.
  Mama Davina

 10. Anonymous

  June 2, 2014 at 1:06 pm

  Dina hongera mno mamy. Mwanao mzuri sana na afya tele. Mungu amkuze na kumlinda na kila baya

 11. Anonymous

  June 2, 2014 at 1:30 pm

  Dina mwanao ni mzuri mnoooo, too cute. Mungu akukuzie mwanao, awape na nyie wazazi wake hekima ili muweze kumlea mtoto wenu. God bless your family.

 12. Anonymous

  June 2, 2014 at 2:08 pm

  Hongera sana Dina kwa kupata mtoto mzuri wa kiume. MashaaAllah Mola akukuzie mtoto wako awe mwema na amuepushe na shari za dunia

 13. Anonymous

  June 2, 2014 at 2:23 pm

  Hongera! You have a very cute son. Mungu awalinde na kuwapa afya njema.

 14. Anonymous

  June 2, 2014 at 3:42 pm

  Ongera sana dada dina. Mungu akukuzie kijana wako

 15. Anonymous

  June 2, 2014 at 11:09 pm

  Hongera sana Mama Zion, Mungu ni mwema siku zite mtoto mzuri sana na usichoke kumuomba mungu azidi kukupa faraja, hekima na busara, wewe pamoja na Baba Zion.

 16. Anonymous

  June 3, 2014 at 7:02 am

  hongera sana dada Dina kwa kuwa mama jamani na hongera kwa Zion wako jamani, ana afya njema halafu kafanana ana dad wake ile mbaya, tunamuomba mwenyezi mungu akukuzie

  kila jema kwako na mumeo Ndege

 17. Anonymous

  June 3, 2014 at 7:05 am

  Maashallah Hongera sana kwa kumleta handsome boy. Inshallah Mungu akukuzie mwanao awe mtoto mwema na msikivu.

 18. Anonymous

  June 3, 2014 at 7:21 am

  HONGERA DINA MUNGU AKUTUNZIE MWANAO

 19. Anonymous

  June 3, 2014 at 8:22 am

  welcome back…missed u bt si sana coz tunakutanaga insta mwaego! kila la kheri dada lake mungu ambaliki zion inshallah akue salama

 20. Anonymous

  June 3, 2014 at 8:31 am

  Hongera sana dina mungu akukuzie

 21. mama manka

  June 3, 2014 at 8:55 am

  hongera dina mungu akukuzie mtoto wako mzuri kzion

 22. Jullie

  June 3, 2014 at 8:56 am

  Hongera sn sn Dina,Mungu akukuzie kijana wako!Amuepushie hatari za roho na mwili,amjaalie afya njema akue ktk maadili mema.

 23. Anonymous

  June 3, 2014 at 9:05 am

  Hongera Mungu akukuzie

 24. ney

  June 3, 2014 at 9:54 am

  hongera sana dada Dina… wewe wapekee kabisa Mungu akuzidishie mnoo nataman kuonana nawewe japo hua nakutext watsup kukusalimia am so happy hua unanijibu…

 25. Anonymous

  June 3, 2014 at 11:05 am

  HONGERA DINA

 26. Anonymous

  June 3, 2014 at 11:36 am

  Hongera sana,Mtoto mcuteeeee

 27. Anonymous

  June 3, 2014 at 12:05 pm

  he is handsome like daddy lol??ila kana smile ya mommy ake na kipua chake

 28. hawa

  June 3, 2014 at 12:35 pm

  hapana chezea mamii, Allah akukuzie mwanao In Shaa Allah

 29. Anonymous

  June 3, 2014 at 1:03 pm

  hongera mumy, Mungu akukuzie anafanana sana na baba yake

 30. Glady Maimu

  June 3, 2014 at 2:30 pm

  hongera Dina kwa kumpata baby Zion furaha yako imezidi kua kubwa……….hongera kwa kumpata mama mkwe anaejali na mume anajali pia

 31. teressa simon

  June 3, 2014 at 2:48 pm

  Mungu ni mwema sana nimefurahi kwa kila kinachotokea maishani mwako,Mungu aendelee kukupigania, I love you Dina . Mama isaac wa kiseke mwanza.

 32. Anonymous

  June 4, 2014 at 4:46 am

  Mungu ampe afya jaman hongera sana da dina

 33. Anonymous

  June 4, 2014 at 5:03 am

  Hongera sana dina

 34. Anonymous

  June 4, 2014 at 5:20 am

  Hongera sana dina Mwenyezi Mungu akukuzie Inshalah!…

 35. Anonymous

  June 4, 2014 at 5:34 am

  Dina hongera sana he is sooooo cute

 36. Anonymous

  June 4, 2014 at 7:09 am

  Hongera sana Dina, cute Zion MUNGU baba akukuzie katika maadili ya kumpendeza yeye na awe mtoto mwema siku zote, baraka nyingi sana kwako na familia nzima. Huyo mama ni mstaarabu kwa sababu ana hofu ya MUNGU hakuna kitu kizuri katika maisha kama kuwa karibu na MUNGU.

 37. Anonymous

  June 4, 2014 at 7:57 am

  waooo baby ZION jina zuri toto zuri Dina and Reuben hongereni

 38. Lily Z

  June 4, 2014 at 8:45 am

  Waooou nimefurahi kuona umerudi kwa blog..mi tupo pamoja kila sehemu bloguni,facebuk,whatsup,insta etc kwa jinsi gani navokupenda kokote ulipo name nakufata..

  Xox0

 39. decent lady

  June 4, 2014 at 9:12 am

  Dina am super happy,,hongera sana. Congrats for a super Zion, his dad and in law. God b wth u. Am happy u r back here,used to visit everyday

 40. LUCRESHA,DSM

  June 4, 2014 at 9:26 am

  so cutie! he is such a sweet baby! hongera Dinna. Mungu akukuzie! I want one of my own..lol! is high time…in JESUS AMEN!

 41. Anonymous

  June 4, 2014 at 11:19 am

  WOW…… CUTE BABY, JINA ZURI, KAFANANA NA MAMA, BABA, BIBI….. MUNGU AKUKUZIE INSHAALLAH. HE IS SO CUTE. HONGERA SANA DINA. KWELI TULIKUMISS. MUNGU AMJAALIE MWANAO AFYA NJEMA, IMANI NA BARAKA TELE. AMEEEN

 42. Anonymous

  June 4, 2014 at 11:39 am

  Hongera dada Dinah

 43. Eva Magali

  June 4, 2014 at 11:54 am

  Hongera Dina Mungu akukuzie mpz, na malezi mema mama Zion!

 44. Mbalu Mimi

  June 4, 2014 at 11:56 am

  Mungu ni mwema sifa na shukrani tumrudishie yeye.

  Mungu akujalie umlee king Zion katika misingi bora kama ww na baba yake mlivyolelewa na wazazi.

  Welcome to the motherhood.

 45. Anonymous

  June 4, 2014 at 12:07 pm

  hi dada dina, hongera sana na Mungu akulindie Baby Zion. Naomba kujua daktari wako ni nani na anapatikana wapi, natafuta daktari mzuri wa mambo ya uzazi ili nianze clinic nami.

  Nashukuru kwa msaada utakao utoa. mungu Akubaliki

 46. Anonymous

  June 4, 2014 at 12:14 pm

  Thanx kwa kushare nasi binafsi I wish u all da best wen de wedding comes plse share us some 4toz

 47. Anonymous

  June 4, 2014 at 12:52 pm

  Hongera sana Dinna, ZION Kafanana sana na Baba yake, pia nimependa Hair style ya Mama Mkwe, your very Lucky, ana maadili ya Mungu.

 48. Anonymous

  June 4, 2014 at 4:47 pm

  Hongera best. da boy is xo cute kuna wimbo wa krismas unaitwa zion"s daughter unaujua?

 49. Anonymous

  June 5, 2014 at 6:47 am

  hongera sana Dina mtoto ni mzuriii

 50. Anonymous

  June 5, 2014 at 10:20 am

  hongera mama zion, we misd u kwakweli,, wel cm back, na karibu pia bby zion,, twakuombea uwe super hero zaidi ya dad na mam

 51. Anonymous

  June 5, 2014 at 10:46 am

  Hongera sana Dina .Mtoto anafanana sana na Baba yake

 52. Anonymous

  June 5, 2014 at 11:10 am

  Mtoto n mzuri hadi rahaaa,congrats alot

 53. Anonymous

  June 5, 2014 at 12:57 pm

  hongera mwaya tulikumisi kwa kweli ila mtoto kafanana na daddy mpaka basi haahahaaa all the best my dear kulea mimba sio kazi kazi ni kulea mtoto mtangulize Mungu atakuongoza

 54. Amina K

  June 9, 2014 at 12:12 pm

  Hongera dina, tulikumiss sana.

 55. Anonymous

  June 12, 2014 at 2:18 pm

  Hongera sana dina. Mwanao mzuri sana na ana afya. Namfunika kwa damu ya yesu mtoto na wazazi pia ili shetani asije akawasogelea. Nakupenda dina na nitazidi kukupenda. Tm

 56. Anonymous

  June 13, 2014 at 5:50 am

  Hongera dina

 57. Anonymous

  June 14, 2014 at 8:54 am

  hongera sana mpenzi

 58. Anonymous

  June 18, 2014 at 2:56 pm

  Hongela

 59. Anonymous

  June 29, 2014 at 8:30 pm

  Cute boy! I am happy for you Dina…tulikumiso sana…yani mpaka niliacha kupitia hii blog nikijua huko busy na ukijacho…hongera sana mamito; hakuna furaha humu duniani kama kuwa na mwana

 60. Anonymous

  July 4, 2014 at 7:16 am

  Hongera dada dina

Leave a Reply