Uncategorized

FUATA DONDOO HII ILI KUJIJENGEA TABIA YA KUNYWA MAJI INAVYOTAKIWA KIAFYA

By  | 

Wengi wetu tunapata shida sana kunywa maji vile inavyotakiwa.Tunakunywa maji pale tunapokuwa na kiu tu basi usiposikia kiu siku inaweza kupita bila kunywa maji.Mimi sasa hivi nafanya mazoezi trainer wangu huwa ananisimamia ile asubuhi kuhakikisha nimemaliza lita moja na nusu.Kwa siku natakiwa kunywa lita tatu za maji.

Wataalam wa mambo wanasema kwa siku tunapaswa kunywa maji glass nane.Ila kama unatatizo la kutopenda kunywa maji hii tip inaweza kukusaidia.
*Kunywa glass moja ya maji kila baada ya lisaa limoja.Masaa nane yakifika tayari utakuwa umekunywa glass nane.Fanya hivi kwa mwezi mmoja baada ya hapo utajikuta imeshakuwa tabia yako.

1 Comment

  1. Anonymous

    August 1, 2014 at 6:02 pm

    Boost your water drinking ability….then Kula tende 2 na glass 1 ya maji.

Leave a Reply