Uncategorized

DADA DINA CARES NA WATOTO WA KITUO CHA ZAIDIA SINZA

By  | 

Kwa uwezo wa Mungu tulifanikiwa kutembelea kituo cha watoto yatima cha Zaidia kilichopo sinza madukani.Kwa michango tulopokea tumefanikiwa kuwapelekea nguo kidogo,unga kg 150,maharage kg 100,mchele kg 100,unga wa ngano kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia ndoo 3,sabuni za miche box 4,mafuta ya kujipaka dozen 4,miswaki na dawa za meno.
Tulikaa na watoto tukacheza kidogo na kuwapa vichangamsha mdomo baadae kurejea makwetu.Shukrani kwa mliochanga chochote ulichobarikiwa maana kutoa ni moyo si utajiri.Kuna matajiri lakini hata sh 10 yake hatoi kwa haya mambo.Kuna mtu unaona kajinyima kweli mpaka kachangia na bado kwa watoto anaenda kuwatembelea.Asante kwa team nilokuwa nayo Easter Nyalusi,Halima Temu,GLoria Shayo,Vivian Mchome,Blandina Mvungi,Ummy Kitwana,Tuntufye Abraham,Kaka Richard Chambai na mwanamuziki Mwasiti alikuja pia kujumuika nasi.Bado tunavituo vitatu Sifa bunju,house of hope mabibo na vetenari temeke ambavyo tutavifikia weekend hii.

8 Comments

 1. esther nyalusi

  August 4, 2014 at 11:39 am

  Mungu azidi kukuweka ili uweze kutimiza haja za moyo wako,barikiwa sana

 2. Anonymous

  August 4, 2014 at 3:34 pm

  Dada dina kiroho safi tu naona umejisahau sana najua ni ulezi ila chonde chonde usijisahau sana maana kipindi cha mimba mpaka uzazi wanawake wengi wanajiachia sana hapo ndiyo kipindi cha kina baba kubadilisha mawazo sasa dada dina naona umejisahau shemeji asije akabadili mawazo uzazi wa kizamani ndiyo ulikuwa hivyo lakini sikuhizi wanawake wameshajitambua wanajikumbuka angalau kidogo kipindi cha uzazi nafikiri umenielewa.

  • dinamariesblog

   August 4, 2014 at 5:20 pm

   Usijali naelewa na wala sijajisahau.Mwili wangu naufanyia kazi utarespond muda ukifika.Hata mimba mpaka kuzaliwa ilichukua miezi 9.Na mwili pia kirudi kwenye hali ya zamani unachukua muda.Nashukuru kwa mawazo yako ni mazuri sana na ni mema kwangu.

 3. Anonymous

  August 5, 2014 at 11:21 am

  mmh umenenepa sana jamani hupendezi kama zamani.

 4. Anonymous

  August 7, 2014 at 5:45 am

  Watu wengine bwana sijui wivu au upeo mdogo wa kuelewa, Dina kasha ambiwa kuwa kanenepa, kalikubali na kasema analifanyia kazi wewe kisebusebu na kiroho papa, kurudia maneno aliyosema mwenzio ndio jini? Dina miaka 100 mamii raha jipe nwenyewe upendeze usi pendeze ina huu?

 5. Anonymous

  August 7, 2014 at 12:25 pm

  Kipindi chako cha TV kitaanza lini naona umekaa sana, Tupo anxious kukitazama.

 6. Anonymous

  August 11, 2014 at 8:35 pm

  Samahani Dada dina nilikua na swali kule kwenye mapendo mema ila sijui wapi pa kuuliza.

Leave a Reply