Uncategorized

JUMAMOSI ILOPITA DADA DINA CARES ILIPOTEMBELEA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA MWANDALIWA.

By  | 

Tunashukuru Mungu anaendelea kutupigania na yale tunayojadhamiria kuyafanya kwa dhati  yanatimia.Ni mwezi sasa nilipoanza kuchanga hela za kununua vitu hasa chakula na kupeleka kwenye vituo vya watoto yatima.Na jumamosi ilopita tuliwasilisha vitu katika kituo cha kulea watoto yatima cha Mwandaliwa kipo mbweni.
Tulipeleka unga kg 150,mchele kg 100,maharage kg 100,sukari kg 50,unga wa ngano kg 50.Pia tulipeleka ndoo 4 za mafuta ya kupikia,box 4 za sabuni za miche za kufulia ambazo kila box inakaa miche 10.Mafuta ya kujipaka dozen 4,dawa za meno box zima,miswaki,malapa n.k
Kama ujuavyo chakula lazima watoto wale kila siku hivyo tunashukuru tumefanikisha hilo.Nawashukuru wote waliojitolea kufanya kazi na mimi hasa Halima Temu,Gloria Shayo,Ummy Kitwana na kijana anaitwa Richard Chambai.Hizi ni kazi za kujitolea hazina malipo yoyote lakini wao walijitoa na tukafanikisha.Nitakuwekea na picha tulipoenda kituo cha Zaidia kilichopo Sinza madukani.

14 Comments

 1. Anonymous

  August 4, 2014 at 1:15 am

  Mpendwa Dina hongera sana kuguswa kwa dhati na pia Mwenyezi Mungu kukujalia kutimiza azima yako kwa kuwaweka sawa hawa wanetu yatima.Hakika wewe ni mama wa nguvu.Ubarikiwe pamoja na timu nzima ulioshirikiana nao.Maandiko ya dini yanatuasa tuwajali sana yatima na mjane.

 2. Anonymous

  August 4, 2014 at 7:59 am

  dinna tuongee ukweli unapenda sifa sana.

  • dinamariesblog

   August 4, 2014 at 9:43 am

   Eti eeh?basi sawa.

  • Anonymous

   August 4, 2014 at 8:25 pm

   Kwahiyo cha sifa hapo ni nini? Jaribu wewe kuchangisha fedha za watu kisha usionyeshe hata matumizi yalikuaje! Hivi mtu akifanya vyema ni ngumu sana kumkubali eeh?

   Dina hongera mwaya. Hongera kwa moyo wa utoaji…wengi wenye nafasi kama yako hawaguswi kuhudumia hili kundi la yatima. Ubarikiwe mpaka ushangae.
   Christine

 3. esther nyalusi

  August 4, 2014 at 11:31 am

  Mungu anajua nini haja ya moyo wako mumy na uzidi kubarikiwa sana na sana.no matter vikwazo we songa mbele tu

 4. Anonymous

  August 5, 2014 at 1:20 am

  duniani kuna watu na viatu,we tia pamba masikioni Dina.Mungu ndiye hakimu wa yote.Endelea kutupa vya maendeleo,wasioyataka wabaki na wivu wao mbele, na Mungu atakubariki tu.

 5. Anonymous

  August 5, 2014 at 11:18 am

  Umenenepa vibaya mwili umekuwa mkubwaaaaaaaa

  • Anonymous

   August 6, 2014 at 5:27 pm

   kipi kinachokurea na wewe Dina muda ukifika utapungua tu

 6. Anonymous

  August 6, 2014 at 11:15 am

  Alokwambia kunenepa dhambi nani? Laanakum wahedi..! Nimekugundua ni mtu mmoja unaeweka comment shombo! Acha mara moja, sijawahi comment ila nimeumia sana kwanini mtu usipite kimya? Huyo Dina humjui hakujui..kama huna kazi kashii ulale…

 7. Anonymous

  August 6, 2014 at 5:24 pm

  we kinachokukera kipi na mwili Dina my dear go go go usisikileze ya watu muda utakapo fika utapungua tu

 8. Anonymous

  August 6, 2014 at 5:26 pm

  We kinachokukera kipi na mwili wake Dina mpz fanya yako muda ukifika utapungua tu

 9. Anonymous

  August 11, 2014 at 10:16 am

  Hellow dina,MIC u ma dia,kama hutojali plz whatsap me,my no 0713 913840

 10. Anonymous

  August 17, 2014 at 3:57 pm

  hongera mungu akubariki

Leave a Reply