Uncategorized

MAPISHI YA MABOGA NA VIAZI VITAMU,MBOGA MBOGA NA MINOFU YA KUKU.

By  | 
MABOGA NA VIAZI VITAMU
Nimechukua maboga nikaamenya nikaosha na kukata kata vipande vidogo vidogo.Na viazivitamu pia nikamenya na kuosha kisha nikakata vipande vidogo vidogo nikavichanganya na maboga kwenye sufuria moja.Nikaweka maji kiasi chumvi kidogo na 

Kisha nikavibandika jikoni vichemke na kuiva kwa muda wa nusu saa.Vilipoiva nikavitoa jikoni nikachuja maji yote nikaviponda ponda na kuwa laini kabisa kisha nikaviweka siagi itokanayo na maziwa.Nikakoroga vizuri ili iyeyuke na viwe bado vya moto na harufu nzuri baada ya hapo ikawa tayari kuliwa.

MBOGA MBOGA
Kwenye mboga mboga kuna kitunguu maji,kitunguu saumu,karoti,hoho nyekundu na njano,maharage machanga,brocol hii mboga sijui kiswahilo chake na kolimaua.
Niliweka mafuta kwenye kikaango natumia mafuta ya alizeti yalipopata moto nikaweka kitunguu nikakaanga pamoja na kitunguu saumu vilipokuwa brown nikaweka nyanya kidogo.Nyanya zilipoanza kuiva nikaweka chumvi na baadae nikaweka mboga mboga zote na kuzikoroga kuchanganya vizuri.Nikaongezea ndimu ili kuichangamsha.Baada ya dk 10 nikaipua maana haitakiwi kuiva sanaa kidogo tu.

KUKU MINOFU
Mnofu wa kuku ni eneo la kidari huwa lina mnofu wa kutosha.Nilichofanya niliosha kuku vizuri nikamkamulia ndimu na nikaweka tangawizi ilotwanga ikalainika vizuri na chumvi.Nikaweka kwenye frying pan kisha motoni nikaongeza maji kidogo.Nikamuacha aive mpaka maji yote niloweka yakauke kabisa na kuku akauke na kujikaanga na mafuta yakr kama yapo.Nikanyunyizia pili pili manga kwa juu akakauka kabisa kisha nikamtoa tayari kwa kuliwa.Hapa sijatumia mafuta kabisa.

Kama sahani inavyoonekana katika picha hapojuu inaliwa huo mchanganyiko wa viazi vitamu na boga,mboga mboga na kuku.Ni tamu mno na rahisi kupika.Hizo mboga mboga unaweza pia kuzila na wali hata chips hiyo kuku.

18 Comments

 1. Anonymous

  August 7, 2014 at 8:42 am

  Ahsante Dina kwa kutuelekeza pishi la viazi vitamu na maboga. Nitajihidi wikendi nijaribu kupika hili pishi kwa kufuata maelekezo yako lakini hili pishi la mboga mboga ulizo taja sijawahi kula ,brocol na kolimaua hivyo nitaenda supermarket kununua ama karikoo sina uhakika kama zinauzwa. Nimefurahi kuzijuria hapa kwa blog yako. Mungu akubariki nakupenda sana Dina Marios

 2. Anonymous

  August 7, 2014 at 11:35 am

  Ulikuwa unawabania wenzio kwenye LEO TENA lakini akaa kipindi kinasonga mbele tu. VIVA GEA NA DA HUUU.

  • Anonymous

   August 8, 2014 at 5:30 am

   Binadamu hamuna shukran alikua anawabaniaje sasa while kila mtu alikua anapata nafasi ya kuongea kwenye muda wake dina ndo alikua main pale. Watu wengine bana ovyoo ukikosa cha kusema kaa kimya ndo ustaatabu.

  • Sia

   August 8, 2014 at 3:38 pm

   I see wivu ni sheeeeeda!! Yani ndo keshamchukua Ncha kali baba Zion nna anajali family yake huyoòoo poyee ww km ulipigwa para ukaachwa utajiju! Mama Zion atabaki kuashine cjui ww usienajina utabaki kua Anonymous siku zotee!

  • Anonymous

   August 13, 2014 at 9:40 am

   umenenaaaaaaaaaaa

 3. Anonymous

  August 7, 2014 at 12:24 pm

  Brocoli na Kolimauwa utavipata soko la kisutu au mtaa wa jamhuri wanaviuza vibarazani mwa maduka ya wahindi huko utapata kila kitu.

  • Anonymous

   August 11, 2014 at 7:05 am

   Ahsante ndugu nilipita kisutu nilipata. Barikiwa

 4. Anonymous

  August 7, 2014 at 3:31 pm

  Asante kwa pishi zuri dada dina ila usipende kitunguu maji kukiunguza kiafya si kizuri ni ushauri tu..

 5. Anonymous

  August 8, 2014 at 12:17 pm

  Dina ni Dina ataendelea kuwa Dina, tupo kwenye mapishi unatuletea habari nyingine tofauti, watu wengine bwana! !!!!!!asante mwaya Dina wetu,Uzuri watu kama hawa Ulishajua namna ya Kudeal nao

 6. Anonymous

  August 8, 2014 at 5:37 pm

  asante kwa mapishi nakupendajeee

 7. Anonymous

  August 8, 2014 at 5:38 pm

  asante kwa mapishi nakupendajeee

 8. Anonymous

  August 8, 2014 at 8:32 pm

  lazima inoge!

 9. Anonymous

  August 9, 2014 at 4:37 pm

  AAAhhh, nicheke mkuki kwa nguruwe

  • Anonymous

   August 14, 2014 at 10:06 am

   kwa binadamu mchungu

 10. Anonymous

  August 13, 2014 at 9:39 am

  kweli wewe dinna una sifa mpaka basi badala ya kuelimisha watu mambo ya maana kuna matukio mengi tuu yanayojiri huku duniani ukakaa kufanya show off hapa sii bure uliambiwa bado kidogo utaonesha unavyofanya mapenzi duh!!!!! too much. mbululaaaaaaaaaaaaaa

 11. esther nyalusi

  August 13, 2014 at 1:42 pm

  Hivi Kuna watu mmetumwa au ni wendawazimu habari iliopo ni mapishi we unaleta habaro zisizo husuuuu,mbona hujaweka picha na jina kama unajiamini msyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu kafie mbele huko

 12. esther nyalusi

  August 13, 2014 at 1:42 pm

  Yaaaaaani niko ku copy nakupaste kila kitu hapa

 13. Anonymous

  August 18, 2014 at 11:38 am

  wewe anon 2:39, hapo juu tafuta hayo mengine kwenye blog nyingine tuachie dina wetu, dina endelea tuletee pishi jingine, siye tupike achana na wajingajinga

Leave a Reply