Uncategorized

MY HOBBIES…MAUA

By  | 
Wale mlioulizia stand za maua zinapouzwa piga simu namba hii hapa utawapata 0717004838
 Kwenye maisha haya kila mtu ana vitu anapenda na vinamfurahisha yeye mwenyewe.
Kuna watu wengine wanapenda magari na ni machizi magari kila leo ana jipya.Mie hapa sina intrest kabisa na magari nina forbia kabisa ni vile nifanyeje lazima nilipande linifikishe niendako.
Napenda maua na nacollect maua nikiliona mahali zuri nachanganyikiwa kabisa ninavyoyafurahia.Najua kuna watu wanapenda maua kama mimi na kama haupendi bahati mbaya lakini lazima na wewe kuna kitu chako kingine unapenda.

38 Comments

 1. Lily Z

  August 22, 2014 at 9:09 am

  wooou yanapendezaje mi pia nina hobi hiyo hiyo yaani nadatajae sasa ngoja ntakutumia maua kadhaa ambayo sijayaona nikuelekeze na pakuyapata. Usambara mountain hiyo ya pink na red yametanda vizuri kwenye hiyo stendi..

 2. Anonymous

  August 22, 2014 at 9:59 am

  safi sana maana maua ni mazuri sana

 3. Anonymous

  August 22, 2014 at 11:45 am

  wallah… huu ulimbukeni utakuisha lini dinna. duh!!!!

  • Anonymous

   August 22, 2014 at 5:12 pm

   Sasa ulimbukeni hapo kauonyesha wapi??? Watu mna stress zenu za maisha mnataka kuletea wenzenu shindwaaaa.

  • Anonymous

   August 23, 2014 at 5:55 am

   Unajitahidi kuponda sana lakini mwenzio kimyaa hujishtukii tu Kama inakukera fumba macho usione

   .

  • Anonymous

   August 23, 2014 at 5:58 am

   Mama Zion nimependa ntaiga

  • Anonymous

   August 25, 2014 at 9:31 am

   Kwani lazima uingie ktk hii blog? mbona watu wengine wachokozi hivyo? yaani yote hayo unataka Dina akujibu.

 4. teressa simon

  August 22, 2014 at 12:26 pm

  Mi kiukweli sina kabisaaaa hobbie ya maua ya kupanda kama hivyo wewe dina,ila napenda ku decorate ndani na hobbie yangu ni vyombo,napenda sana vyombo vya ndani na picha mbalimbali na kupika,hongera sana kwa kuitendea haki hobbie yako

  • dinamariesblog

   September 6, 2014 at 8:21 am

   hongera sana mie hilo la kudecorate napenda mno ila vyombo kiasi tu cha kawaida itabidi ni udopt maana naona kama sina vyombo vya kutosha.

 5. Anonymous

  August 22, 2014 at 12:36 pm

  Hi dina hongera sana….. wapi unapata flower pots zako please share. thanks

 6. Anonymous

  August 23, 2014 at 5:40 am

  I lav flowers ila vumbi la moro linanikatisha tamaa

 7. Anonymous

  August 23, 2014 at 11:23 am

  uyo baba zion awe muangalifu maana nyumba yake itageuka msitu muda si mrefu.

 8. Anonymous

  August 23, 2014 at 1:36 pm

  ANNOY 4:45 AM.utakufa na kijiba cha roho,ngoja nikushauri kitu usijepata Bp buree nyonyo USIINGIE HUMU,

 9. Anonymous

  August 24, 2014 at 12:31 pm

  mama zion kipindi lini cha tv lini?nimekumisi japo hata kasura kako tu

  • dinamariesblog

   September 6, 2014 at 8:23 am

   kipindi cha tv bado kidogo kikiwa tayari utakuwa wa kwanza kufahamu.

 10. Anonymous

  August 24, 2014 at 5:13 pm

  Binafsi napenda sana maua na hizo stendi zilinidatisha kabisaaa ngoja nipige namba fastaaaaa

 11. Anonymous

  August 25, 2014 at 3:59 am

  Dina hongera mama…mie nahisi hiyo nyumba ni yako kabisa unavyoipenda

 12. Anonymous

  August 25, 2014 at 5:57 am

  Kuna watu Wa ajabu jamani mtu kaweka hobby yake ulimbukeni uko wapi hapo?Kwani umeitwa humu kwendraaaa

 13. Anonymous

  August 25, 2014 at 6:12 am

  Annoy 4.45 AM , yaani Dina Hana jema sasa hapo kibaya kipi? Una Lako jambo Aisee sio bure.

 14. Anonymous

  August 25, 2014 at 9:43 am

  Tembelea bustani mpya iko pembeni na baraka plaza njia ya kuingia beach kama mita tano hivi toka beach. Ndiyo inaanza lakini inapendeza saana

 15. RUCKSHAZ

  August 25, 2014 at 12:14 pm

  ANONY 4:23 acha roho mbaya utakufa mdomo wazi,tangu ameanza kuyapanda hayo maua bb zion hakumuona?? Jamani si mfanye yenu ??yeye ameshafanya yake!! Nakupenda dada Dina

 16. Anonymous

  August 25, 2014 at 2:03 pm

  Halafu uchawi sio lazima upae na ungo,hata roho mbaya pia ni uchawi!Go go Dina…thx for sharing Dina!

 17. Anonymous

  August 25, 2014 at 2:05 pm

  Hongera Dina!Halafu kukaa kimya ndo jibu la mjinga!

 18. Anonymous

  August 26, 2014 at 9:30 am

  ulivyokuwa kijitonyama mauwa ulikuwa hupendi? mbona hukutuonyesha,usibanie coment

  • dinamariesblog

   September 6, 2014 at 8:16 am

   kwa sababu umeniuliza ngoja nikujibu.Kila siku kwenye maisha unaruhusiwa kuongeza hobbies na wakati mwingine ndani yetu kuna vitu tunavipenda labda kwa sababu ya mazingira unashindwa kuvifanya au kuwa navyo.Kwa hiyo kupenda maua lilikuwa ndani yangu nikiwa mdogo nyumbani tulikuwa na bustani ya maua na nilikuwa namwagilia na kutunza maua.Kijitonyama seems unapajua nilipokuwa naishi palikuwa na maua na yaliishia kunyauka maji yalikuwa ya kununua hamna maji sasa ninunue maji dumu 500 nimwagilie maua au ninunue maji ya kupikia,kufua na usafi nyumbani.Nilipo sasa vyote vipo ndani ya uwezo wangu maji yapo mengi tu na mazingira yanaruhusu kufanya hivyo.Ipo siku utaniona nachora utanishangaa ni kwamba mimi ni mchoraji mzuri tu ila mara ya mwisho kufanya hivyo mwaka 2004 ila ndani yangu napenda kuchora na ipo siku nitarudi huko.Ni sawa na mtu ambae leo anabajaji na anapenda siku moja awe vitz lakini sababu ya hali ya wakati huo hawezi kuwa nayo.Sasa siku ukimkuta na vitz utamuuliza mbona wakati ule ulipokuwa na bajaji hukusema kama unapenda vitz?am sure hata wewe ulipo wewe leo sipo ulipokuwa jana wala juzi.

  • Anonymous

   September 8, 2014 at 7:04 am

   Asante sana kwa kunielewesha. Naomba uanze kuutuwekea na mapishi yaani menu mbalimbali.

  • dinamariesblog

   September 8, 2014 at 7:22 am

   ntajaribu maana siku hizi sipiki piki sanaa nipo kwenye diet.

 19. upendo lema

  August 26, 2014 at 2:59 pm

  yani inapendeza sana,penye sifa tusifie,Dina anastahili sifa,ww mwenye roho ya kwanini una yako ndo mana hakuna anaekusupport

 20. Anonymous

  August 27, 2014 at 10:32 am

  Twasubiri ndoa sasa

 21. Anonymous

  August 28, 2014 at 8:39 am

  habari Dina,samahani mpenzi mi nilikuwa nahitaji unielekeze panapopatikana vyungu hivyo vya plastic,mi ni mgonjwa mwenzio kwenye maua.napenda hatari.plssss.

  • dinamariesblog

   September 6, 2014 at 8:18 am

   vyungu jaribu kuulizia popote unapoona wanauza maua sasa sijui wewe unaishi wapi.Au nenda kwa wale wauza vyombo vya plastic vya cello au cello kwenyewe.Huku mbezi ya chini kwa wauza maua mie ndio huchukua huko.

 22. Amina K

  August 28, 2014 at 8:39 am

  mie pia napenda sana maua toka nipo shule nilikuwa napanda home, tena wakati huo tupo nyumba ya kupanga, naokoteza huko majumba ya watu kwa marafiki nakuja napanda home, baadae tkahamia kwetu ndo kabisa, nikamfanya mama angu nae awe mpenzi wa maua akawa ananunua au tunanunua wote,tukampata mtunza bustan akatupandia kwa ujuz sasa. yaani nyumba ilikuwa kama jangwa now inapendeza. Wasiopenda maua wanashangaza mana maua ni kama bahar ukikaaa kwenye bustan mawazo yote yanaondoka unapata mawazo mapya na mazur kwa zile rang mbalimbali za maua. Dinna keep it up tupo nyuma yako siku nami nitakupostia bustan yangu

 23. Anonymous

  September 2, 2014 at 9:48 am

  ulimbukeni?sijaelewa?unahusiana nn na DINA kupenda maua?Mhhh watu wengine nini jamani?Apawomiiiiiiii!!!!!

 24. Anonymous

  September 2, 2014 at 11:19 am

  Hey ma Dina, mic u any thing new jaman!

 25. sina neno na enjoy

  September 7, 2014 at 9:04 am

  kuna mtu.umu.ana niacha oiii any way dina do wat u fel mwaya .

 26. Anonymous

  September 17, 2014 at 7:19 am

  mi hata sijuhi ni nini jamani maana kama ni kufanana na wewe basi this is too much jina langu ni Geraidina ila jina maarufu dinna wengi walishindwa kuliita jina langu kuwa ni refu hivo bibi yangu akaanza kuniita dina mpaka leo naitwa hivo ila watu wakiniita dina lazima wamalizie na Marious basi huwa nawambia mwenyewe akijua atanifunga. nimekua mfuatiliaji mzuri wa harakati zako tangia nipo chuo mpaka sa hivi nimemaliza nipo najishughulisha na ujasiria mali. Da dina ninapenda maua hatari zamani nilikua naishi na aunt yangu magomeni kwenye nyumba ya kupanga lakini nlikua na bustani ya maua uani watu wakawa wanakuja kupigia picha hapo hasa nyakati za siku kuu na mengine nilikua nayaweka ndani napamba wakati wa Christmass chumba kilikua kama Garden hivi kwa sasa naishi kinyerezi na huko nimepanda maua mengi sana . wakati nipo High school Mtwara technical chumba changu kilikua maarufu kwa kupambwa na natural flowers karibu kila siku walimu walikua wananishangaa wakipita kukagua vyumba na wakati mwingine wananiomba niwaelekeze jinsi ya kumpamba kitanda kwa kutumia maua na style tofauti za kukunja mashuka kiukweli ni kitu ambacho kipo ndani yangu. Kuhusu kuchora ndo husiseme napenda kuchora hatari chumba changu kimejaa picha nipo za kuchora pia wakati nipo form 3 nilitengeneza diary kwa manila cards na kuchora picha nyingi zilizokuwa zinaendana na vitu nilivoviandika niko nayo mpaka leo na nimeitunza ili nije kumpa mwanangu ntakapojaliwa kupata mtoto. mara nyingi nikiwa na hasira au mawazo huwa zinaishia kwenye kuchora au kutengeneza mapambo ya nyumbani kama frame za picha kwa kutumia vitu tofauti tofauti ila ndo hivo vipaji vingine ni kama kupika nina pika waliosomea mapishi wanakaa chini kuna siku dada angu alinambia ataachika ntaolewa mimi baada ya mumewe kunisifia kwa kupika chakula kizuri sijisfii sana ila namshukuru MUNGU kwa kunijalia hivo navifurahia vipaji vyangu na natamani nipate oppotunity ya kuvitumia kuwasaidia wengine…… mpe hi sana King Zion be blessed my dia kama utapata time naomba unitumie email my adress dinnakaiza@gmail.com

Leave a Reply