Uncategorized

ZAMANI NILISUMBULIWA SANA NA HILI TATIZO.

By  | 

Siku hizi huku kwenye mitandao watu wana maneno na misemo ambayo wakati mwingine ukifatilia ni kweli tupu.Haya maneno ni kweli kabisa kuna wakati nilikuwa hivyo.Unaweza kuwa una marafiki wewe kichwani kwako unadhani ni watu wako kumbe walaaa.Sasa kwasababu una nia safi nao unajikuta kila siku wewe ndio uwasabahi,uwatafuta na bado wasipatikane yaani watakuwa karibu na wewe kwa sababu ya situation flani inayomuhusu yeye akipita hiyo hali humuoni ng’oo.
Au anakuwa karibu na wewe aliakamilishe kitu flani akikamilisha humuoni unabaki wewe kumtafuta atakupa sababu laki 8 za kwa nini siku hizi humuoni.Kuna watu watakuwa karibu na wewe ili akufanye ngazi ya kupanda mahali flani akishapanda anakutupa kule.Mifano ni mingi sana ambayo hata wewe mdau unaweza kuongezea.Nilipokutana na huo msemo nikasema ngoja niuweke hapa inawezekana kuna mtu mwingine nae haya yanamfika.
i

22 Comments

 1. Anonymous

  August 8, 2014 at 7:11 am

  Lol Dina very true, but these days its easy to tell who is a friend and who isnt

 2. Anonymous

  August 8, 2014 at 11:18 am

  Maneno kuntu,na mie zamani ilikuwa hivyo ila tangu nimekuwa na familia rafiki yangu mkubwa ni mume wangu,sitaki urafiki wa kila siku mie ndio wa kumtafuta mtu,bora nikae najua sina rafiki maana sipungukiwi na kitu chochote

 3. Anonymous

  August 8, 2014 at 12:09 pm

  Sina rafiki zaid ya mume wangu watoto wangu na wadogo zangu,hawa wengine uzushi tu,

 4. mary

  August 8, 2014 at 1:10 pm

  ni kweli kabisa maana kuna watu hadi uwatafute na wao pind wanashida ndo utawaona loh too boring

 5. Anonymous

  August 8, 2014 at 8:43 pm

  Yaani mi mwenyewe muhanga wa hilo lkn tangu nimempata Junior wangu ndo best friend wangu of course na babake hao wengine tutafutane muda uhitaji. afu imehamia had kwa ndugu pia.

 6. Anonymous

  August 9, 2014 at 9:40 am

  Yaani ni kama umeniandikia mimi dina, yashanitokea nikiwa sekondari, na chuo pia mpka sasa nafanya kazi najikuta sina marafiki washafanikiwa wamenitupa kule wako na marafiki wengine..

 7. rukshaz

  August 9, 2014 at 11:22 am

  Dada dina mbona huweki mapishi??? Nasubiri kwahamu

 8. Anonymous

  August 9, 2014 at 4:38 pm

  Muosha huoshwa

 9. Anonymous

  August 11, 2014 at 7:21 am

  yaani binadamu wako hivyo jamani nilikuwa nawatu wanalala kwangu kula kwangu walivyoanza kupanga na wao kila nikiwatafuta busy sababu nyingi nimewasahau maisha yanasonga mbele ila wakiwa na shida hawaishi kukupigia simu sijui hawana aibu jamani

 10. Anonymous

  August 11, 2014 at 9:37 am

  hilo umenena mamy ninao wengi sana yaan mtu anakunyamazia hatu mwaka uku
  imtafuta ndoa ansema mbona kimya hivo.

 11. Anonymous

  August 11, 2014 at 9:58 am

  Asante Dina kwa hili. Mie hadi mwaka huu bado linanisumbua japo taratibu nimeanza kuelewa. Wengine wanasumbuliwa na wivu na kidonda hiki hadi kwa ndugu. Unashangaa out of nowhere mtu kakukasirikia hataki kukusemesha. Walio majasiri hadi uzushi watakuzushia. Nimekuwa wa kulia muda mrefu lakini naanza kupona polepole hadi wengine hawaamini kuwa nimeanza kutojali.
  Nakushukuru sana kwa kuliweka hapa na hata kwa machangizo ya wadau wengine! Loh, hadi tukafe, tutakuwa tumeona na kujifunza mengi saaana sayarini hapa

 12. naike lema

  August 11, 2014 at 2:02 pm

  dada dinakwakweli unachosema ni kweli kabsaa…lakini watu kama hawa dawa yao nikidogo sanaaaa, mtu ukipata matatizo ndo unajua marafiki wako wa kweli, yaani we chukulia matatizo ndo chujio la marafiki watakao kufaa…fainali ukipata pesa na mambo yakakunyookea ndo unawapandishia vioo #SHENZ TYPE, jeuri yoote…ukishika pesa adabu inajaa……AND IM WRITING ALL THIS FROM A FULL EXPIRIENCE

 13. Anonymous

  August 12, 2014 at 8:15 am

  habari za leo wapenzi, Tunatakikwa tuelewe kuwa kuna wakati mtu unahitaji msaada fulani kupitia mtu fulani na wakati huo kweli mtu anakuwa anakunyenyekea sana kwa kuwa tu anahitaji msaada lakini pindi anapofanikiwa huwa kimya kwa sababu mara nyingine anaona kukusumbua tena si jambo jema au anakutana na watu wa aina yake ambao sasa wewe huwezi kuendana nao ndio maana anakuwa kimya kwako uelewe kuwa kila binadamu kuna hatua lazima upitie hata wewe ambaye unasema hivyo kuna mtu anakulalamikia kama unavyomlalamikia mwenzio lazima tutambue hayo ndio maisha yetu na hatuwezi kuyakwepa wapenzi. HAKUNA MKAMILIFU DUNIANI.

 14. esther nyalusi

  August 13, 2014 at 1:23 pm

  Maneno umeyatupa kweli mumy wapo watu.tunao usipomkumbuka wewe basi uju ndio imepita.

 15. Anonymous

  August 16, 2014 at 7:00 pm

  Dah umenigusa

 16. Anonymous

  August 17, 2014 at 7:38 pm

  yani umu mna ni touch coment zenu .mnanitia machung nilio.nayo.but napata faraja sana kutoka umu dina nakupenda sana

 17. Frida

  August 18, 2014 at 9:40 am

  Kweli kabisa Dinna. Watu kama hao wapo wengi sana. Wanatabia za ajabu. Hawakutafuti wanajifanya wako busy ila ukiwapigia cha kwanza ni kuanza kukueleza shida za na kukupiga mizinga. Na wakikaa pembeni wanakuongelea vibaya. Hao sio marafiki. wanatakiwa kuwekwa pembeni kabisa.

 18. Mwananyamala

  August 18, 2014 at 9:46 am

  Dinna kuna dada mmoja anaitwa Kemmy ndio tabia yake. Mwambieni aache. Na kazi yake ni kuchonganisaha watu. Kuzushia watu maneno ya ajabu akiomba msaada akanyimwa. Kamzushia dada wa watu maneno ya ajabu wakatu huyo dada alikuwa anampa hela ya kula na kila kitu sababu yeye ni mzururaji hovyo.

 19. Anonymous

  August 25, 2014 at 12:26 pm

  dah!yaani kama unanisema mimi mungu wangu!tatizo langu mie nilikuwa nawapenda sana marafiki zangu ila wao walikuwa hawana muda namie.dada yangu alishanishauri sana kuacha nao kwani kila siku wewe unaenda kwao mbona wao hatuwaoni huku?kuna tukio walinifanyia liliniumiza wik nzima nawafikiria wao ndo walinifanya kuamua maamuzi yangu,na nilipoamua kuwadelete sasa wanaanza kunitafuta mie,namie nshakuwa sugu na sitaki shoga,nawafanyiaje makusudi?kama wananienjoy nawaenjoy pia na tunaenda sawa mpaka wataelewa.

 20. Anonymous

  August 30, 2014 at 8:07 am

  mi nshakutana nayo sana but i thank GOD sasa hivi tupa kule na nimepata amani coz i know for sure hakuna anaetake advantage of me now

 21. anitha

  August 31, 2014 at 2:55 pm

  Thanx alot dina, iyo msg imenifanya Nipige hatua kubwa kimawazo niliyonayo kuhusu marafik,,,,,god bles u

 22. Anonymous

  September 11, 2014 at 12:07 pm

  yani msg hii imenigusa sana… mimi kwasasa sina mda na rafiki asiye na mda na mimi.. tena nimeichukua na kuiweka katika profile yangu ya whatsapp woteee waisome… wanaonihusu

Leave a Reply