Uncategorized

KAZI NA KIPAJI

By  | 
Hivi majuzi nilienda ofisi moja jengo la biashara complex lililopo mwananyamala.Pale kuna mama nilienda kukutana nae mmoja kati ya akina mama wanaounda network ya wanawake ya Mama Graca Machel tena alikuwepo wiki mbili zilizopita hapa Tz kuzindua nertwork hiyo.
Sasa nikiwa nimepotea maana kuna ofisi nyingi nyingi nikaibukia ofisi ya hawa mabinti.Wasichana hawa ni ndugu mtoto wa mama mkubwa na mama mdogo.Ni mabinti wadogo tu mmoja anamiaka 24 mwingine 21 Yvonne na Ritha.Basi nilipoingia nikakuta wanashona nguo wapo wawili tu humo nikajikuta navutiwa nao.
Nilivutiwa nao kwa sababu kwa namna walivyo ni nadra sana kukuta mabinti wa umri huo wamekaa chini kwenye cherehani wanashona nguo.Wao wanasema nikitu wamekuwa wanapenda toka wapo shule hivyo baada ya kumaliza masomo wakaamua moja kwa moja kujiajiri kufanya kitu wanachokipenda.Wamekodi hiyo ofisi kwa mwaka sasa na wanalipa kodi kila mwezi tsh 200,000.
Pia wanapata suport kutoka kwa wazazi wao wanawateja ndio kiasi chake na gharama zao ni nafuu.Kwa sababu ya uharaka sikuweza kukaa nao kwa muda mrefu.
Kubwa zaidi kilichonivutia  madisigner wengi wa nguo hawashoni nguo wenyewe.Wengi wanajiri mafundi hata kuweka uzi kwenye cherehani hajui.Hawa wanafanya vyote najua muda unavyoenda wakiwa wakubwa kibiashara hawatamudu kufanya kila kitu wenyewe wataajiri mafundi wengine.Hata hapo kuna fundi mmoja wamemuajiri ila sikumkuta.
Wajameni kijana unaepita kusoma hapa changamka fanya kazi,jitume.Mafanikio yako yapo kwenye kipaji chako angalia una kipaji gani kifanyie kazi ili kujikwamua kutoka kwenye umasikini.
“Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini.Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha”.Mithali 10:4

8 Comments

 1. Anonymous

  September 17, 2014 at 8:48 am

  Nimeipenda hiyo dina. Ila mie sijajitambua kipaji Changu nisaidie nikitambue

 2. Anonymous

  September 18, 2014 at 8:29 am

  Na mie nimeipenda Mungu awe nao kwani umri wao mdogo na wamesimama nahakika hao ndo watakao kwa matajiri mbele
  Anonmy hapo juu kipaji chako utakigundua mwenyewe sio mtu mwingine na ukitaka mwingine akigundue ni lazima ukaae kwake . nakushauri tafuta shule ya wanaogundua vipaji vya watu. Ila navyo jua kipaji chako ni hobby yako .na unaweza ukawa huna kipaji ukaamua kukitengeneza mwenywew na kikawa . Na unaweza zaliwa nacho ukashindwa kukitumia kwa kuibeba starehe ya dunia au kuamka kuupara kukaa kibarazani ukisubiri jion ifike.
  Nakupenda sana Dida Mungu akuongoze utafika mbali kwa utabiri wangu kwani unafumbua macho unaiangalia Dunia inazungukaje

 3. Unknown

  September 18, 2014 at 10:02 am

  Hongera zao jamani. Ninavyotamani kujua kushona mimi! Napenda sana ila kila siku nasema kabla sijafa, naomba Mungu anisaidie kufanya vitu vitatu nje ya fani yangu ya sasa. (Chartered Acountant).
  Nataka nijue kushona mwenyewe , nataka nijue kupiga piano na nataka niweze kuendesha ndege.
  Naamini inawezekana.

  Nawapa hongera wadada hao kwanza kuwa ndugu na kufanya kazi pamoja na wasichana that young, ni kitu cha kupigiwa pande.

 4. dina kaiza

  September 18, 2014 at 1:28 pm

  very nice girls this is how we are supposed to be to use our own talents and make life possible rather than depending on men. mi nawatia moyo sana watafika mbali and GOD will bless the work of their hands.

 5. Anonymous

  September 19, 2014 at 8:44 pm

  Napenda anaejituma.. mabint weng wanawaza kuchuna mibuz

  • Anonymous

   September 23, 2014 at 12:02 pm

   Mungu barik kaz yao

 6. Anonymous

  September 26, 2014 at 9:58 am

  mamii naipenda blog yako but huwa nakosa raha napoingia nakukuta huja up date napenda niwe nakuta vitu vitu hivi sawa mamiiiiii

 7. Anonymous

  October 6, 2014 at 2:50 pm

  Good

Leave a Reply