Uncategorized

HADITHI YA CHIRIKU MDOGO.

By  | 

HAPO ZAMANI ZA KALE PALIKUWEPO NA NDEGE MDOGO ALIYEITWA CHIRIKU.HUYU ALIKUWA AKIISHI KASKAZINI MWA DUNIA YETU NA ALIKUWA AKIHAMA MARA KWA MARA TU BARAFU NA BARIDI INAPOANZA.

WAKATI YA BARAFU KUYEYUKA CHIRIKU NAE AKAANZA SAFARI YA KUHAMA LAKINI KABLA HAJAFIKA MBALI BARAFU IKAMWANGUKIA NA KUMFUNIKA KABISA.CHIRIKU AKAJUA NDIO MWISHO WAKE UMEFIKA.

GHAFLA KUNDI LA NG’OMBE WALIOKUWA WANATOKA MACHUNGANI WALIPITA SEHEMU ILE NA KUACHA KINYESI JUU YA BARAFU.SABABU YA JOTO LA KINYESI BARAFU IKAANZA KUYEYUKA.CHIRIKU YULE AKAANZA KUHISI UNAFUU FUKUTO NA JOTO VILIMFANYA AWE NA MATUMAINI NA KUJIHISI SALAMA.ALIANZA KUIMBA NYIMBO NYINGI KWA MATUMAINI AKISUBIRI AKAUKE APATE KUENDELEA NA SAFARI YAKE.

NDIPO ALIPOTOKEA PAKA MWITU ALIYEKUWA AKIWINDA AKASIKIA SAUTI YA CHIRIKU IKITOKEA KWENYE KINYESI.PAKA MWITU HAKUPATA TAABU AKAONDOA VINYESI NA AKAMKAMATA CHIRIKU NA KUMLA.NA IKAWA NDIO MWISHO WA CHIRIKU.

FUNZO
1.YOYOTE ANAEKUNYEA SI LAZIMA AWE ADUI YAKO.
2.NA YOYOTE ANAEKUTOA KATIKA LUNDO LA KINYESI SIO LAZIMA AWE RAFIKI YAKO.
3.KWA HIYO KAMA UPO SALAMA NA MWENYE FURAHA KWENYE LUNDO LA KINYESI FUNGA MDOMO WAKO.

13 Comments

 1. Anonymous

  October 6, 2014 at 11:12 am

  Nice!!!

 2. Anonymous

  October 6, 2014 at 4:11 pm

  Good story

 3. Anonymous

  October 7, 2014 at 5:37 am

  Asante mama maneno ya ukweee! nyc!

 4. Anonymous

  October 7, 2014 at 6:45 am

  fantastic

 5. Anonymous

  October 7, 2014 at 9:16 am

  kweli bana

 6. Anonymous

  October 7, 2014 at 9:22 am

  Funzo tosha

 7. Anonymous

  October 7, 2014 at 9:32 am

  Noted a good msg Dina.

 8. salha Said

  October 7, 2014 at 1:37 pm

  so touchfull

 9. Anonymous

  October 7, 2014 at 6:18 pm

  Dina,i just cant define u sometimes!U are so brilliant,to me, u are more than a woman!i have been visiting ur blog and learning a lot,Zion is luck to have a mother like u,always praying for u,even though u dont know me,be blessed,much love!!!

 10. LILY

  October 8, 2014 at 5:55 am

  nimeipendaaa mwee

 11. Anonymous

  October 8, 2014 at 7:27 am

  Nice ujumbe jamn be blessed Dina

 12. Anonymous

  October 9, 2014 at 1:12 pm

  Dah! Dina Umetisha Xana Na Hii Stor

 13. Anonymous

  October 15, 2014 at 7:09 pm

  Nice story. Dinna nimekumiss sana. redion sikusikii kwenye tv sikuon!!!!!

Leave a Reply