Uncategorized

MSAADA WA MAWAZO KWA CHAKULA CHA MTOTO KUANZIA MIEZI SITA

By  | 

Nimekuwa nikipata mwaswali kutoka kwa wazazi wenye watoto wadogo ambao ndio uzao wa kwanza.Kuhusu chakula cha mtoto kianzia miezi sita mpaka nane,tisa.

Ndio nikaona niweke hapa ili tuweze kupata mawazo wote kwa pamoja maana hata mie nahitaji.Mwanangu sasa hivi ana miezi saba anaenda wa nane.Ukiacha maziwa ambayo anakunywa na kunyonya hivi ndio vyakula ambavyo nimekuwa nikimpa.

1.Uji wa mahindi ulochanganywa na maziwa na sukari kidogo.
2.kiazi kitamu nakichanganya na karoti nakichemsha pamoja kikiiva nakiweka maziwa kisa nakiblend kwenye blander.
3.Wali bokoboko naukatia humo karoti kisha naublend na maziwa.
4.ugali laini na mchuzi wa maharage yaliyopikwa na kitunguu tu bila nyanya.
5.ugali laini na mchuzi wa samaki
6.cerelac hasa usiku
7.Matunda kama papai
8.juice ya tikiti ilokamuliwa juice ya chungwa
9.juice ya chungwa
10.maji ya kunywa huwa nampa mara kwa mara kuna saa hataki kuna saa anayanywa.Maana ni ngumu kujua wakati gani ana kiu.
Hii ni list tu sio ratiba sasa tunaomba mawazo ya vyakule vingine.Ndizi sijaanza kumpa nilisikia huwa zinaleta gas kwa watoto.Na je ni muda gani aanze kunywa uji wa lishe?

68 Comments

 1. Anonymous

  October 8, 2014 at 6:12 am

  Uji wa lishe haushauriwi na wataalam sababu karanga huvunda na kuwa na sumu, bora dona uongezee maziwa. Mwanangu nampa na ndizi sija observe ishu ya gesi. All the best ktk kulea

  • dinamariesblog

   October 8, 2014 at 9:22 am

   asante sana hata mie hili la karanga nimelisikia

  • Anonymous

   October 9, 2014 at 1:13 pm

   Nakubalia na mtoa jibu hapo juu. karanga huwa zina vunda, not unless unasaga nakuitumia hapo hapo.

 2. Anonymous

  October 8, 2014 at 6:15 am

  hi Dina, ndizi mpe za bukoba zile laini hazina gas unamchemshia kwenye soup ya kuku wa kienyeji ila nyama humpi uazisaga ndizi tu kwenye blender

 3. anna

  October 8, 2014 at 7:18 am

  kuanzi miezi sita anaruhusiwa kuanza kula chakula ikiwa na uji wa lishe ila kikubwa ni kuwa makini wakati wa kuandaa na uhivaji kawake pia kama utaweza naomba mtengenezee lishe ya dona ambaya mchanganyiko wake unakuwa na vitu hivi mahindi yasio kobolewa,soya iliyo chemshwa na kukaushwe vizuri,karanga zikaange vizuri,na mchele kidogo kisha unasaga pamoja na unaanika ule unga vizuri kisha chekecha na unakuwa tayari kutumia kwenye uji unaweza weka maziwa na vitu vingine utakavyo penda kuweka

  • dinamariesblog

   October 8, 2014 at 9:25 am

   nashukuru sana lakini nilisikia hata kuna mtu amecomment pia humu.Kuwa karanga si nzuri inavunda na kuwa sumu unless usage na uji unywewe siku hiyo hiyo sio unga wa kukaa muda mrefu.

 4. Anonymous

  October 8, 2014 at 7:49 am

  hongera sana Dina mtoto amekua na ana afya nzuri.

 5. Anonymous

  October 8, 2014 at 8:12 am

  supu zaina zote samaki nyama, maharage mpe. mtori pia sawa, mbogamboga pia anahitajika kula unaweza kupiga mtori wako then karibu unaiva dumbukiza mbogamboga blend pamoja. la chemsha mbogamboga mpe supu yake.akikisha anakula nyama samaki, maini hata kama utablend pamoja na chakula chake pia sawa maana wakati huo yeye hawezi kutafuna

 6. Anonymous

  October 8, 2014 at 8:12 am

  Boga la kuchemsha nachanganya na maziwa,mimi mtoto wangu ana miezi nane na wiki tatu,nampa maziwa ya ng'ombe ila yanatakiwa kuchemka vizuri,ndizi bukoba nachanganya na viazi mbatata na karoti na kitunguu,pia naweka broccoli au cauliflower alafu nasaga kwenye blander.
  Pia kwa upande wa tunda parachichi ni zuri unaweza kuchanganya na chungwa linamletea ladha nzuri.
  kwa upande wa uji nimeshaanza kumpa lishe ambayo ina mchanganyiko wa mahindi,mchele,ngano na ufuta.nikiwa naupika naweka maziwa,butter na peanut butter.
  Vyakula vingine ninavyompa ni kama alivyovitaja Dina.

 7. lisa

  October 8, 2014 at 8:18 am

  kwa kuongezea unaweza kumpa boga unachanganya na gimbi kidogo unavichemsha then unblend pia ni chakula kizuri sana kwa mtt,ndizi za bukoba unachanganya na smaki sato au kuku wa kienyeji unablend pia supu ya samaki sato ni nzuri na inampa calcium nyingi mtt

 8. Anonymous

  October 8, 2014 at 8:59 am

  parachichi wachanganya na ndizi mbivu na maziwa una blander maji unatia kidongo inakuwa nzito kama uji

 9. Anonymous

  October 8, 2014 at 8:59 am

  dada dina hii mada imenigusa kuchangia mi mwanangu nampaga hivi kwa kuongezea
  Asubuhi;uji ambao huo uji ndani yake unakuwa na ufuta wataalamu wanasema ufuta unasaidia mtoto IQ simuwekeagi karanga so nikiupika namchanganyia na maziwa na blueband kidogo maana ukiweka nyingi so nzuri kwa mtoto mafuta.
  saa nne;anakula cerelack.
  mchana;anakula viazi ambavyo vimechemshwa siweki mafuta naweka carrot hoho kitunguu namiwekea na uyoga wataalamu pia wanasema inasaidia IQ
  saa tisa:juice machugwa au papai au parachichi na passion any matunda namtengenezeaga.
  saa kumi na moja;anakunywa maziwa ya lactojen
  usiku;ndizi zilizochanganywa na samaki samaki ni nzuri sana kwa mtoto inasaidia afya nzuri na IQ.
  alafu ka akichelewa kulala ikifika saa nne nampa celelack den kulala.

  huo ndo mlo ninaompaga mwanangu mtoto anashauriwa kila baada ya masaa manne ale.asante dada dina tuna share ideas inabidi u add samaki na uyoga kwa zion ni nzuri sana naweza kukutumia pic ya mwanangu he'z health and I believe h'z genius haaaaaaaa lol.

  • dinamariesblog

   October 8, 2014 at 9:21 am

   nashukuru sana my dear nitumie picha kwa email dina_marios@yahoo.com

  • Lamyaseif

   October 15, 2014 at 10:20 am

   Mambo nimependa huo mpangilio yani kama wangu kabisa sasa mie nikawa naogopa kwamba namnyima maziwa muda mwingi na ana miezi saba sasa kwani wako anamiezi mingapi au nakosea plz nijuze

 10. Anonymous

  October 8, 2014 at 9:08 am

  me nashauri mtori wa ndizi bukoba, butternut, gimbi, boga pia mzuri kwa mtoto pia unaweza kumpa na supu ya kichwa cha samaki ni nzuri mno, kwnye juice unaweza kumpa juice ya carrot, parachichi na nanasi ni nzuri pia
  pia kwenye mtori unaweza kumuwekea zukin,conrflower,etc

  • dinamariesblog

   October 8, 2014 at 9:29 am

   shukrani sana kweli mwanangu alikuwa ana miss vitu vingi

 11. Herieth

  October 8, 2014 at 9:56 am

  1. Kiazi mviringo kikubwa kimoja na kipande cha samaki hasa sato au sangara…unachemsha pamoja…chumvi kwa mbali sana yaani kidogo then vikiiva unachambua hakikisha hakuna mfupa kisha unablend…hakikisha huongezi maji ule mchuzi ndiyo inachanganyiwa kwenye rojo

  2. Asubuhi hakikisha anakunywa uji wa dona…uchemke sana uji usipochemka husababisha madhara kwa mtoto tuwakanye na house girls kuhusu hili wasiripue

  3. Hakikisha chakula chochote unachompikia usiweke sukari kwa wingi, chumvi au mafuta

  4.Akifikisha mwaka wengi huwa wavivu kula hakikisha unamtayarishia mboga mboga kwa wingi wangu nilikuwa nampa majani ya maboga na bamia yaani unakuwa mlenda wanapenda sana watoto ila mara mbili au moja kwa wiki….pia mboga zake ziive vizuri ila zisipoteze ukijani

  Mengine Dinah kamaliza

  • Anonymous

   October 8, 2014 at 10:27 am

   basi sawa

 12. Anonymous

  October 8, 2014 at 10:09 am

  mimi nilishamaliza kulea mwanangu wa mwisho ana miaka 5!! Nimependa kushare nanyi kuhusu samaki ukichemsha supu tumia kichwa cha samaki ndo umtengenezee supu, kichwa cha samaki ni kizuri sana kwa mtoto anayekua,vingine vingi mlivyoshare viko poa.

 13. Anonymous

  October 8, 2014 at 10:54 am

  JE UNATAKIWA KUMPA MTOTO CHAKULA KILA BAADA YA MUDA GANI KWA MTOTO ANAYEANZA KULA

 14. Mama Malkia

  October 8, 2014 at 10:57 am

  Asanteni na mimi nimejifunza hapa .
  Mtoto wangu anafikisha miezi 9 mwisho wa mwezi ; vyakula vyake ni
  Mtori wa ndizi uganda nablend na kipande cha nyama ya kuku, au samaki , au beef
  Wali boko boko nablend na karoti
  Mtori na njegere na karoti
  Brocoli, zuchini , kiazi na karoti
  Butternut , karoti na kipande cha nyama
  Nyama ya kusaga nablend na mboga mboga
  Viazi vitamu na karoti nablend na maziwa
  Samaki nachemsha na mboga mboga nablend
  Juice ya parachichi na chungwa
  Ndizi mbivu nablend na embe na maziwa
  Papai na embe
  Juice ya tikiti
  Uji nampa dona ..namuwekea na maziwa na siagi kwa mbali
  Uji mwingine nimetengeneza leo naanza kumpa nimechanganya ufuta, ulezi, mahindi ya bisi ,ngano isiyokobolewa, na brown rice.
  Sijatumia karanga kwa sababu wanasema sio nzuri kwa mtoto badala yake ndo ufuta.
  NB : ukitengeneza huo uji zidisha mchele na mahindi.
  Mama malkia

 15. Anonymous

  October 8, 2014 at 12:13 pm

  note:celac sio nzuri kwa watoto inapoteza hamu ya kula, celac ni tamu ukija kumpa uji wa dona hatakuelewa,pia unga wa lishe sio mzuri kwani huo mchangako kila kitu kina boiling point tofauti,yani mchele utawahi kuiva zaidi ya unga wa maindi,au mtama utaungua wakati mahindi bado hayajaiva,ni bora umpe mahindi tu na maziwa,mchele tu na maziwa,.

 16. Anonymous

  October 8, 2014 at 12:55 pm

  Mtoto inatakiwa ale kila baada ya masaa mawili tafadhali.Asubuhi saa mbili uji,saa nne supu/maziwa,saa sita juisi,saa saba chakula,saa tisa tunda la kuponda/maziwa,kumi na moja cerelac, ikifika kumi na mbili na nusu supu/maziwa, saa mbili kamili chakula, kabla ya kulala akichelewa mpe cerelac. ukitaka cerelac unaweza korogea na maziwa.Juisi ya chungwa si nzuri kwa watoto chini ya mwaka,inaleta gas sana,mtoto anawezashindwa kula vizuri vyakula vingine sababu hiyo.

  • Anonymous

   October 10, 2014 at 9:10 pm

   Mdau kwa mtoto wa miezi sita hapo ni kum-overfeed. Ndio maana wamama tunalalamika watoto hawali kumbe tunawazidishia kipimo cha chakula. Kumbuka kuwa bado hawako active kwahiyo wakila chakula kinakaa tumboni muda mrefu. Kifupi mtoto wa miezi sita chakula chake kikuu ni maziwa ya mama/kopo. Juice labda mara moja kwa siku, na vi-mbogamboga kidogo vilivyosagwa mfano: karoti, njegere, mchivha, kiazi kitamu. Nia ni kuanza kumzoesha ladha mbalimbali lakini isiwe ndio chakula kikuu.

 17. Anonymous

  October 8, 2014 at 6:22 pm

  Boga ni nzuri sana..ila jamani karanga hapana dona is the best kwa kweli..pia papai waweza changanya na ndizi au parachichi..juice ya carot pia nzuri usafi uwe 100% ni bora mama kutengeneza peke yako na sio msichana wa kazi hizi juice

 18. Anonymous

  October 8, 2014 at 6:23 pm

  Mtoto anakula naada ya masaa 3

 19. Anonymous

  October 8, 2014 at 6:37 pm

  Dina nashukuru sana kwa mada hii nintoto anamiezi 11 hataki kula naombeni msaada wa mawazo.

 20. Anonymous

  October 8, 2014 at 6:54 pm

  Dina maziwa weka kwenye uji na umpe anywe tu pendelea kuweka supu kwenye chakula,pia lishe mpa ila weka maind ngano ulez na ufuta inatosha kabisa,pia tambi changanya carot hoho na main af saga inakua nzur sana

 21. Anonymous

  October 8, 2014 at 6:59 pm

  Af nilisahau dina achana na macerelac mavyakula ya kopo sio mazur pia kwa umri alionao zion kama unaweza pata mtu mwenye ngombe ambae unamwamin mpe ya ngombe achana na makopo sio mazur basi tu tunatumia but now anaweza kunywa na kama hayamzuru poa kabisa,pia jitaid sambil awe amekula il usiku apate kunyonya vzr maana wamama weng mchana hatupo hom watoto hawapat kunyonya vzr so uck ndo wanapata kunyonya

  • Anonymous

   October 10, 2014 at 9:04 pm

   Maziwa ya ng'ombe mpaka mtoto afikishe mwaka mmoja. Maziwa ya mama ndio the best, ila pia kuongezea na ya kopo sio mbaya kama nyonyo pekee haitoshi. Chakula kikuu cha mtoto chini ya mwaka mmoja ni maziwa, hivyo vingine vinatakiwa viwe kiasi kidogo sana.

 22. Anonymous

  October 8, 2014 at 7:10 pm

  Pia mtoto anatakiwa ale akiwa amekaa mwenyewe chini au kwenye kiti cha kulia cha watoto(high chair) au unampakata ila usimbane na mikono, ukimbana ndio mana watoto wanalia na kukataa kula coz wanaona kubanwa. Ila ni vizuri kuanza na chakula kimoja kimoja ili kuona kama kitamdhuru mana ukimchanganyia moja kwa moja na kimpa tatizo hutojua ni chakula gani. Pia usimpe chakula kingi mtoto chini ya mwaka mmoja mpe mara mbili tu, kama asubuhi uji jioni msosi sana maziwa ya mama kwa sie tunaonyonyesha na maji.

 23. Anonymous

  October 8, 2014 at 7:18 pm

  Ila mmetaja vyakula vingi sana mtoto anatakiwa apate wanga protin mbogamboga matunda vyakula vingine mnakuwa mnawaova doz watoto badala ya kuwa na IQ kubwa anashuka hata mim sipendekezi macerelac na maziwa mtoto chini ya miaka miwili mkazanie maziwa yako mama mimi ni hodari wa kunyonyesha kuliko lishe kwa mtoto mchanga na mwanangu wa kwanza darasani ni wakwanza tu nahis na wapili atafuata nyayo maziwa ya mama ni bora zaidi ila mama inabidi ule sana madocta wanashauri hivyo vyakula ni ziada tu maziwa ya mama ndo mpango mzima ndo maana wamasai watoto wao wananyonyaga tu miaka mitatu bila kupewa chochote

 24. Anonymous

  October 9, 2014 at 3:27 am

  ongeza mboga za majani. chemsha tu then mpe ile supu yake esp mchicha, majani ya maboga, mnafu..weka kachumvi kwa mbaali kuongeza ladha. you can also blend with cucumber…..very good for cell development.

 25. NURU RAMSI

  October 9, 2014 at 9:39 am

  ahsanten wamama,mnatusaidia wamama wa mtoto wa kwanza,mbarikiwe sana barikiwa dada Dina

 26. Anonymous

  October 9, 2014 at 11:22 am

  Nimeipenda sana mim mtoto wangu ndo anaanza kula kweli nimepata pakuanzia mana nlikuwa cjuh chochote

 27. ESTHER

  October 10, 2014 at 4:58 am

  Dina kweli wewe una maono na mungu akuzidishie maisha.mimi sina mtt mdogo ila mdogo wangu ana mtt wa mwakammoja na miezi miwili suddenly amekataa kula kila kitu , nilipoona hii topic nikamwambia alog kwenye blog hii halafu asome comments za watu. akafanya hivyo .jana nimeongea naye nikamuuliza kambadilishia mtt chakula ? akasema yes jana alimpikia kiazi akachanganya na ndizi akaweka carrot na maziwa hajawahi kupikia hivyo , yaani nasikia mtt alikula mpka wakahisi atavimbiwa. walimpa na juice ya tikiti hajawahi kupewa hiyo alikunywa ila kidogo. mama mtu alifurahi sana maana alikuwa analalamika mtt anapungua hataki kula.amenunua note book na comments za diet zote walizotoa watu humu ndani ameandika .nashukuru sana kwa msaada.

 28. Anonymous

  October 10, 2014 at 7:41 am

  Dunia ya sasa kila kitu ni sumu!!! Karanga ni sumu….mbona hata maziwa ya ng'ombe hayaruhusiwi kumpa mtoto wa binadamu kuyatumia? Mana wanasema kuwa ni magumu kuwa digested…so which is which?
  Wazazi wetu ndo walitulea kwa hizo karanga na ndo tumekua na akili za kumwaga lols. Any ways maisha ni kujifunza mana kila siku research zinatuletea ufahamu mpya.

  But kwa ishu ya sumu wallah unaeza ukaacha kula maana hata hao samaki wamesha kula mercury wakiwa majini nazo zina sumu, mboga mboga ndo usiseme mana sinamwagiliwa dawa bila kufuata ushauri wa wataalamu saa ingine zinamwaigiliwa dawa leo kesho zipo sokoni sasa hizo si ni sumu pia?
  AKILI ZA KUAMBIWA…….CHANGANYA NA ZA KWAKO lols

 29. Irene

  October 10, 2014 at 11:24 am

  Dada Dina asante kwa hii topic kwa wanaolea kama nimi nimefaidi sana. Mimi mwanangu amekataa kunyonya akiwa na miezi 7 sasa yuko mwezi wa 8 ila ni majanga make hata kula anasumbua mpaka ameloose weight. Mbarikiwe wamama.

 30. Anonymous

  October 13, 2014 at 5:26 am

  Msiwape watoto wadogo nyama nyekundu, inahitaji nguvu nyingi kusagika. Imagine watu wazima wanakatazwa nyama nyekundu nyie mmekazana humu nyama ya kusaga, nyama ya kusaga ya nini jamani?

  Wapeni jamii ya kunde na maharage zaidi, kama vile choroko, hizi unaweza kuziloweka kisha ukaziotesha kama unaona kazi nunua zilizooteshwa supermarket. Choroko zina protein na iron ya kutosha.

  Weka dengu, au dal, ina protein ya kutosha na ziko dal za aina nyingi tu, moon dal etc, nenda Shoppers section ya hivyo vitu utapata kila kitu mpaka unga wa uwele ambao nao una protein ya kutosha.

  Usiweke blueband kwenye chakula cha mtoto marufuku, weka natural fat kama parachichi ina faida kubwa na haina additives.

  Kama mtoto uzito wake unapungua, kuna nazi weka tui la kwanza la nazi kwenye chakula chake badala ya maziwa. Kwa sababu nazu ni chakula bora sana na dawa pia, ina anti fungal, anti viral and anti bacteria.

  Mpake mtoto mafuta ya nazi badala ya kuhangaika na mafuta fake yasio na benefit yoyote.

  Pendelea kummassage mtoto ukishamuogesha, hii inamfanya arelax na akuwe vizuri.

  Ni mimi bibi wa watoto wote.

  • Anonymous

   October 17, 2014 at 10:06 am

   Asante bibi kwa ushauri wako nimeupenda sana.

  • Vivian

   January 2, 2016 at 10:11 pm

   Bibi nimependa mawazo yako. Ahsante sana. Dina una akili wewe miaka 1090

  • shanice laiser

   May 28, 2016 at 10:43 am

   Nimeipenda hii bibi asante sana

 31. Anonymous

  October 13, 2014 at 8:03 am

  Mdau 10:26 nazi pia si nzuri sana kwa chakula zina kiwango kikubwa cha chorestrol wataalamu wanashauri isitumiwe kila mara. Hapa duniani vitu vingi vina madhara jamani ukivifuatilia basi hutakula ahahahahaha

  • Anonymous

   October 14, 2014 at 9:59 am

   Aliyekwambia nazi ina cholestrol ni nani? Macelebrity wanakunywa mafuta ya nazi kila siku for healthy and good skin. Hebu nenda kagoogle benefits of coconut, au tafuta nature cures not medicines. Huwa nawatibu watoto wenye utapiamlo kwa kutumia smoothie ya tui la nazi na ndizi mbivu. Mafuta ya nazi yana anti bacteria, antifungal na antivirul.

   Wenzenu huko duniani wanatumia maziwa ya nazi kwa chai kama healthy option umecrem wapi nazi inaleta cholestrol?

  • Anonymous

   October 16, 2014 at 10:55 am

   Ndio nazi inachoresrol kwani macelebrity ndo wanaguide tule nini ebo!!
   Cha msingi kila kitu kina mdhara hata kama ni kizuri.

 32. Mama oj-Kilindi

  October 15, 2014 at 4:38 am

  Mimi mtoto wangu ana mwaka sasa hivi na miezi miwili, uji nnaompa una KARANGA nakaanga vzuri tu, soya, mahindi yale ya njano ya bisi, ngano, ulezi na mchele vyote navitayarisha vizuri tu, hata kama wanasema ss hv karanga zina sumu, jamani sie tumekua na hizo lishe za makaranga, na mwanangu sitaacha kumpa karanga ndivyo nilivyoelekezwa na walionilea mm
  Kingine nimeona wengi hamjaongelea KIINI CHA YAI namchanganyia na uji mara 3 kwa wiki ndo nampa.
  Na sio kila siku mtoto anakula uji jamani anachoka asbh uji asbh uji…mbadilishie badilishie.
  Vingine anavyokula mwanangu
  -Mtori wa samaki au kuku wa kienyeji
  -wali bokoboko na apple na maziwa
  nasaga kwa pamoja
  -ugali wa dona laini na mchuzii
  -dengu
  -veggies namuwekeaga kwenye vyakula
  njegere
  -machungwa ndo anayapenda sana naona
  -samaki kua makini na ambao hawana
  mercury nyingi
  -oat meal
  -makaroni ukipata mazuri unamchanganyia na njegere carrots kitunguu
  -boga la maziwa
  Anakua vizuri tu nashukuru Mungu kwa lishe nnaompa alhamdullilah hata akiumwaga hapungui kg nyingi na hajawahi shuka graph ya kwenye kadi alhamdullilah.
  NB; simpi hivyo kwa siku moja hapana, na zingatia mafuta na chumvi havifai kwa under 1yr, ukitaka kilainishi cha uji atleast TANBOND.

 33. Mama oj-Kilindi

  October 15, 2014 at 4:40 am

  Nilisahau…Ili kupata mboga zisizo na madawa nimepanda mchicha kwaaajili ya mtoto na pia ndo anaoupenda sana, na majani ya maboga…asanteni

 34. Mama oj-Kilindi

  October 15, 2014 at 4:46 am

  Jamani nnavyoandika kila baada ya masaa mawili mtoto ale sio kweli jamani…kha hapumziki kulala huyo mtoto, atleast matatu au manne maana watoto wanalala sana wengine kama wangu kwakua anakula vzr anashiba hakataagi chakula alhamdullilah na siri kubwa yangu ni kumchezeshea ratiba tu hazoei chakula kimoja…yes pia i second mdau aliesema samaki kichwa bwana upate jibichwa la sato utapenda, muwekee na ndizi, kiazi, kabichi, kitunguu, hoho na carrot akitoka hapo huo usingizi wake balaaaa….malezi mema jamani.

 35. aisha kayumba

  October 15, 2014 at 4:27 pm

  DINa ubarikiwe sana na mwenyexi mungu hakuna mambo yanayotusumbie sisi wageni first mothrI kama hay a nakuona ni mkomboxi wetu kwa kweli

 36. Anonymous

  October 16, 2014 at 6:49 am

  Hi Dina. Mimi mwanangu huwa najitahidi kwa wiki ale samaki mara tano. samaki ni wazuri sana. unaweza ikampa n'a ugali, wali au ndizi. mimi huwa simpi viazi sababu huwa vinamsababishia gesi. Pia jitahidi kila siku iwe unampa matunda ya aina tofauti.

 37. Anonymous

  October 16, 2014 at 8:35 am

  Wapendwa nauza product za forever living kwa wagonjwa na watu smart wanaopenda afya zao,pia nna multi vitamin kwa ajili ya watoto wasiopenda kula inaongeza hamu ya kula.Kwa atakayehitaji anifollow instagram lattycarson au whatsapp no.0717 773397.Asanteni

 38. Anonymous

  October 17, 2014 at 8:03 am

  hi dina, mmetaja vyote mmesahau green beans mnamuwekea kwenye mitori na milo yote

 39. Zamkwise

  December 3, 2014 at 9:32 pm

  Aisee,mmetusaidia sana,asante mtoa mada

 40. Anonymous

  December 7, 2014 at 4:44 pm

  Hi dina nimefurahi kuona jinsi gain wamam tunapenda name kupeana ushauri. Mimi pia ni mama mwenye motto wa kwanza nimeona comment kuhusu samaki mwanangu nikimpa supu ya samaki Leo kesho anaamka anavipele mwilini. Nifanyeje maana samaki ni nzuri kwa mtoo

  • Vivian

   January 2, 2016 at 10:18 pm

   Umempa samaki aina tofautitofauti au aina moja mi naona kama vp badilisha aina ya samaki uende taratibu kwa interval ndefu ujue ipi ina shida. Lakini kama shida ni serious muone paediatrician kwa ushauri mzuri zaidi

  • Vivian

   January 2, 2016 at 10:22 pm

   Mimi nimependa hii maada ila my dears kila mtoto ni tofauti jamani jitahisi kumjua vizuri wa kwako jamani au mnasemaje? Ukiiga mambo ya wengine utachanganyikiwa. Na pia mother's instincts juu ya mtoto wake ni muhimu sanaaaa hvo kama kuna kitu unadoubt then do not apply hasa kama si lazima sanaa. Ahsante

  • Anonymous

   February 22, 2016 at 12:55 pm

   Ulezi kazi ila Mungu ni mwema

 41. Anonymous

  June 2, 2016 at 4:26 am

  Mwanangu amekataa kunyonya tangu ana miezi miwili ,sasa hivi ana miezi mitatu anatumia maziwa ya kopo tu(lactogen 1) nifanyeje aendelee kunyonya?

 42. Anonymous

  October 12, 2016 at 7:10 pm

  Enter your comment…jamani nataka kujua mtoto wa miezi mitano anatumia vyakula gani

 43. HETHAL JULIUS

  October 14, 2016 at 1:29 pm

  Imekaa vizuri hiyo nimeipenda, ngoja nianze kufanyia kazi sasa

 44. HETHAL JULIUS

  October 14, 2016 at 1:31 pm

  Nimeipenda hii kitu ngoja nikaanze kufanyia kazi mawazo ya wamama wazuri!! Mbarikiwe saaana wapendwa wangu!!

 45. HETHAL JULIUS

  October 14, 2016 at 1:32 pm

  Nimeipenda hii kitu ngoja nikaanze kufanyia kazi mawazo ya wamama wazuri!! Mbarikiwe saaana wapendwa wangu!!

 46. farida khamis

  January 29, 2017 at 6:18 am

  Hay dada dina mwanangu anazidi kupungua uzito na ana miaka miwili alikua anharisha sana meno hadi amefikisha kilo 10 naomba ushauri wa vyakula ambavyo vitarudisha uzito wake wa mwanzo

Leave a Reply