Uncategorized

NAOMBA MSOME HAPA NA TUMPE USHAURI MAMA HAPA YUPO NJIA PANDA.

By  | 

dina naomba uniombee ushauri wangu kwa wanawake wote na wanaume wanaopita ndani ya hii blog yako.mimi ni mfanyakazi mama wa watoto watatu wakike mmoja nilimzaa kabla ya kuolewa na hawa wawili ni mapacha wa kike jumla watatu. Mume wangu nilimkuta na mtoto mmoja wa kiume tatizo lililopo mtoto wangu mkubwa juzi kaniambia mama kaka ananivua chupi ananifanya mchezo mchafu tena sio mara moja kama mara mbili nikasema sawa subiri baba arudi. Baba alivyorudi tukakaa tukaongea akasema atafanyia uchunguzi swala hilo atatoa jibu. kwa kweli niliumia nikasema sawa saa ya kulala akaniambia wewe kama mama ulikuwa wapi mpaka mtoto anafanya hicho kitendo na umeshindwaje kumgundua kama ameanza mahusiano na kwanini asiseme toka siku ya kwanza anafanyiwa hicho kitendo nikawa nimechoka nilichofanya nikakaa kimya nafikiria kuachana na huyu bwana kwa ajili ya mwanangu nateseka moyoni jamani nipo kazini akili inawaza mwanangu alivyotendwa nifanyaje mimi na baba hanipi ushirikiano zaidi ananituhumu kweli hii??

  USHAURI WAKO PLS??

33 Comments

 1. Anonymous

  November 11, 2014 at 1:24 am

  Pole sana nimeumia roho sana binti yako ana umri gani ?mungu akulindie

  • Anonymous

   November 12, 2014 at 12:47 pm

   mtoto wa kike miaka 12 wakiume 16

  • Anonymous

   November 26, 2015 at 10:18 am

   uwiiii jamani mkaka kabisa,si keshambikiri kabinti hako?nahisi hasira

 2. Anonymous

  November 11, 2014 at 3:49 am

  huyu anayeomba ushauri hembu kwanza kabla sijaanza kumshauri andike umri wa huye mtoto wake wa kike na huyo wa kiume ndipo nijue pakuanzia kumpa ushauri

 3. Anonymous

  November 11, 2014 at 7:24 am

  kwanza mama huna haja,ya kumuona baba mbaya,,,yy anakisa gani,,km unaona bb anakosa na ww unakosa sawasawa na hilo,,,sababu wewe hukujua knachoendelea mpaka bint yako alipokwambia,,au baba alikua anajua..?? hvyo basi km mlikosea kwenye malezi huu c wakat wa,kulaumiana wala kukimbiana,, mnatakiwa,mkae chn mlijadil muwaite na watoto,,then mtafte jins ya kuwatenganisha ikiwezekana mmoja aondoshwe coz wanaweza kuendeleza hyo tabia wakiwa pamoja. Usipende kukimbilia kuondoka,,unakoenda akifanya tena hyo tabia utakimbia tena? Sababu huyo mwanao nae cdahan km alibakwa walishawishiana akafanya,,angebakwa angekwambia cku ileile,, so kaen chn na wanenu semeni nao,,bdae kaa na bint yako sema nae,,umweleze madhara ya hayo mambo,,. Mambo yataenda sawa ila usikae kumlaumu mumeo yeye hakumtuma kijana wake,,asante

  • MOJAONE

   November 15, 2014 at 12:39 pm

   Mama anamlaum mmewe kwa kutotoa ushirikiano baada ya kujua.

 4. Anonymous

  November 11, 2014 at 7:48 am

  Pole mama japo hujatuambia umri wa mtoto wako. Kwakuanzia nenda hospital ili ijulikane mtoto kadhurika kiasi gani kisha waweza kuchukua hatua aidha za kisheria au kuwaona wataalam wa saikolojia

 5. Anonymous

  November 11, 2014 at 7:50 am

  Pole sana tena sana . Hata mie ningepebda kujua umri wa watoto hao wawili wahusika.
  Ila ndugu yangu mwanamke mwenzangu nakushaur tena kwa mapenzi.
  Ongea na mumeo kwa mara nyingine akitoa jibu lile la kwanza . Waite watoto wate wawili wakalishe ukiwa kama mzazi tena nindependa uwe na ndugu wa mumeo ikiwa ni wakwe au shemeji yule mwenye sauti katika familia. Kisha ongeeni na watoto na kuwajulisha lipi baya na lipi zuri . Na wajue wao ni ndugu hakuna anayechangia mapenzi na ndugu hata kama hawakuzaliwa tumbo moja.'
  Kisha mtaftie mwanao shule ya boarding na ukiendelea kumjulisha Hatari ya mapenzi utotoni . KWANI MUONJA ASALI HAONJI MARA MOJA:

  Usipotoa sauti niamni usiniamini kuyo kaka mtu atakuja kuanza mchezo na hao mapacha. Mie nasomea mambo ya watoto wa vitu wanavyoanza utoto. ,Huyo mtoto wa mumeo sio mtoto wa kawaida kwani watoto wengi huanza huo mchezo ila hawaanzii ndani .Inaonesha ni jinsi gani atakavyoendelea kuwafanya watoto wa ndani .

  KINGINE WAZAZI TUJITAHID TUWE NA DARASA LA KUHUSU DUNIA NA WATOTO WETU ,HAKUNA ATAKAYE WAEKLEKEZA BAYA NA ZURI ILA NI SISI.
  ANGALIA MAMBOMMENGI YANATOKEA NA KUENDELEA KUTOKEA KWA KUWA HATUWI WAWAZI , NA NAGAZETI, MITANDAO YA TANZANIA IKO WAZI KULIKO MINGINE. MIMI NAISHI ULAYA NIKIINGIA KATIKA COMP KAMA KITU KIBAYA LAZMA NIANDIKE UMRI NA COD NO . HATA KAMA KIKO YOUTUBE,
  TANZANIA BLOGS NYINGI UNAKUTA PICHA HATA HUELEWI NA NI KAWEKA NA ANAAKILI AU?

  DARASA KWA WATOTO MUHIMU ,UNASEMA MCEZO HUU HUTAKIWI ,TIGO NI MARFUKU MPE NA SABABU KWA NINI VIBAYA,
  MWANAUME WAKO NI SAWA NA PICHA ULOIWEKA KTK FREM .SITAKI KUMUHUKUMU NAKUACHIA WEWE MWENYE MAUMIVU UAMUE KUHARIBU MAISHA YA WATOTO AU AUCHANE NAE.

 6. Anonymous

  November 11, 2014 at 8:22 am

  Kabla hayafikiria kuachana na huyo Mume wake, amuangalie mtoto kama hajaharibika zaidi, amsaidie na mtoto wa yule baba ajue kuwa huyu ni mdogo wake hakustahili kumfanyia hayo aliyoyafanya na pia asikimbie nyumba, dawa ya tatizo ni kulitatua sio kukimbia tatizo.

 7. Anonymous

  November 11, 2014 at 8:31 am

  Pole sana dada ndio mitihani ya ndoa hiyo,nahisi mtoto wako ni mdogo but weka umri wa huyo mtoto wa kiume.

 8. Anonymous

  November 11, 2014 at 9:27 am

  Mbaya saan

 9. Anonymous

  November 11, 2014 at 11:44 am

  Pole sana, wanaume wengi huwa upande wa watoto wako, tena ushukuru mungu mtoto amekwambia mapema, tafakari kwa kina wala usichukulie masihara katika jambo hilo, mwanaume utapata mwingine, je mtoto?

 10. Anonymous

  November 11, 2014 at 12:10 pm

  kweli dada tunaomba uandike umri wa watoto ili tuweze kutiririka maana huwenda wanafikiria wanacheza au kaka yupo serious anajua achokifanya.funguka dada na punguza munkari

 11. Anonymous

  November 11, 2014 at 1:13 pm

  Mtoto wangu wa kike ana miaka 12 na wa kiume 16

  • Anonymous

   November 12, 2014 at 12:45 pm

   WANAWAK WENZANGU TUJITAHIDI MTOTO ANAPOKUSHITAKIA USIJIBU TUSUBIRI BABA ARUDI . TUWE NA MAAMUZI NA SAUTI NDANI YA NYUMBA ZETU . JE JIONI BABA AKIRUDI MKAKOSANA AU ASIPORUD UTAFANYAJE ?
   MIE MTOTO AKINISHTAKI HUWA SISUBIR NAMWITA NA MUULIZA .
   UMEKAA NA MWANAUME INA MAANA MTOTO WAKE NI WAKO USISUBIRI MAAMUZI SASA JIBU ALOKUPA LINAKUUMIZA ,BORA UNGEYAMALIZA KAMA MZAZI.
   TUNAFICHA MENGI NA NDO YANATUUMIZA .MUHIMU MUHAMISHE MWANAO BILA HIVYO WATAENDELEA KISIRI NA UTAENDELEA KUUMIA
   JINSI NIJUAVYO HUYO MTOTO WA KIUME KAONJA NDANI ATAENDELEA KWANI ITAKUWA NGUMU KWAKE KUTOFAUTISHA NDUGU ..USHAURI HUYO WA KWAKO MPELEKE SHULE YA KULALA ILA MWELEZEE BAYA NA ZURI NI LIPI KATIKA UMRI WAKE ,
   KWA SABABU ENZI ZANGU HATAA STAREHE YA PENZI SIKUIJU NDO MAANA NILICHELEWA KUANZA WATOTO WA SASA WADOGO WANAANZA,

 12. Anonymous

  November 12, 2014 at 6:11 am

  kwa umri wa watoto nadhani niwakubwa sana…kwa nini msiwaite wote wakajieleza kwa pamoja.halafu mkawaonya kabisa na kujua mazingira yanayompelekea kumfanyia hivyo ni saa ngapi na wanakuwaga wapi ili umuepushe??kikubwa ni kumwambia asikubali kufanyiwa hivyo kabisa kabisa kwa bahati mbaya ikitokea akapenda hicho kitendo kwa kuwa ni wana ka undugu hawataa waache mapema na itakuwa aibu kwa familia yako..

 13. Anonymous

  November 12, 2014 at 6:26 am

  pole ndugu, wote hao wako kwenye umri wa kukua na wanahisia kali sana nijukumu la wazazi kuwapa elimu ya mabadiliko ya miili na hisiza za miili yao. kuondoka sio tatizo wapeleke hospitali ukacheck afya zao alafu muongee nao na muwapeleke kwa wataalamu wa maswala ya saikolojia waongee nao na watumishi wa mungu wenye busara na sisitiza wenye busara waongee nao pia. alafu mama zidi kuwa karibu na mtoto wako wa kike kwanzia sasa awe rafiki mwanao kwako, nasisitiza awe rafiki mwanoa kwako( usijemfanya shosti yako, hapana).
  hizi changamoto ziko kila sehemu so hakuna haja yz kuzikimbia ni kupambana nazo tu.

 14. Anonymous

  November 12, 2014 at 6:39 am

  Yaliwahi kunitokea ila mtoto wangucalikuwa wakiume na step brother wake ndio alikuwa akimfanyia uchafu huo, nilipo mwambia mme wangu akamtetea mtoto wake jiyo nje ya ndoa basi nilichofanya niliwafata rafiki zake wote nikawaambia mkasa mzima naona waliongea nae vizuri, alirudi nyumbani amechukia eti nimetangaza mambo ya siri ya aibu ya familia nime mdhalilisha kwa rafiki zake, ingawa alimuadhibu mtoto na akampeleka kijijini kwa bibi uake kwa mda sijui atarudi lini ila mwanangu anaendelea vizuri ingawa na wasiwasi bado tuombeane jamani wazazi tuna kazi sana, nilifikiria kuchukua awamuzi wa kisheria hasa kipindi nilichokuwa namwambia mme wangu upuuzi wa mwanangu wa kambo halafu yeye ananijibu mbovu…..angalia na aiana ya marafiki wa mme wako kabla ya kuongea nao wengine hawatakusaidia kabisa utabaki kuchekwa ni vizuri pia ukaona wazazi pia mwanangu alikuwa ana miaka 14na yule wa kambo 17

 15. Anonymous

  November 12, 2014 at 10:50 am

  yaani mie nadhani ningekimbia ndoa kabisa
  Miaka 16 linajua kabisa mema na mabaya pumbaff zake

  • Anonymous

   November 14, 2014 at 11:54 pm

   kwakweli mie ningeachana kabisa na hiyo ndoa,sasa akianza kulala na hao mapacha?utamsubiri tena baba yao umwambie nae akujibu ovyowanawake sie tunaendekeza upumbavu kwakweli.

  • Anonymous

   November 18, 2014 at 2:09 pm

   nyie hamko criaz ww km mama huwez kimbia tatizo isitoshe c baba aliyefanya hayo ni mtoto ambae unamlea ww japo c wako ww ndo unaeweza kukemea hiyo tabia tena bado mapema je ukikimbia ndoa ukaenda huko unakotaka kukimbialia akafanyiwa hayo2 pia utakimbbia hutakiwi mkukimbia tatzo unatakiwa kulikabili na kutafuta suluhisho mama pole sana kwa yaliyokukuta pia usiongee nao kwa hasira koz haitosaidia

 16. Anonymous

  November 12, 2014 at 12:13 pm

  Mtoto wa miaka 12 ni mkubwa kujua jema na baya kwasababu hata mimi nilikua darasa la saba nilivokua 12 na nilikua najua kila kitu coz shule tunafundishwa reproduction na ukimwi darasa la sita , kwahiyo ukae na wanao uongee nao ,uyo ni mkubwa hawezi kuvuliwa chupi akabaki anakodoa macho tu,….atakua anapenda ila kuna kitu wamepishana..cha kufanya ongea nao wote kwasababu hao wameshapevuka akili zao na kuelewa mambo

  • Anonymous

   November 14, 2014 at 12:36 pm

   UMEONGEA LA MAANA HATA MIE UMRI HUO NILIKUWA NAJUA LIPI BAYA AU ZURI.
   NA MIAKA 13 ILOPITA TENA ENZI HIZO VITU VILIKUWA VINAFICHWA .SIJAWAHI KUSIKIA MM YANGU AU BB WAKITUKANA . DUDIA YA LEO IMEJAA BALAA MPK MWISHO.WATOTO WANAANZA MAPEMA .
   USHAURI WANGU KAA NAO UONGEE NAO LA SIVYO WATABEBEBSHANA MIMBA NA KINGINE AKIUME ATAKUJA WAFANYIA HATA HAO PACHA .
   MASAIKOLOGI WANASEMA TABIA YA MTU
   1. ILIANZA TOKA UTOTO
   2. AMERITHI AU
   3.MAZINGIRA NA MAISHA YANAWEZA MFANYA AWE HIYO.

   UKIONA MTU MLEVI TAFUTA CHANZO UTAGUNGUA VITU VITATU NILOVITAJA.

   KWA HAO WATOTO YAWEZEKANA UKARIBU WAO WALONAO , KUTOKUAMBIWA BAYA LIPI ZURI LIPI NA KUWA PEKE YAO MUDA MREFU .

   DAR WATOT WENGI WANAHARIBIKA MAZINGIRA YA MAHALI.
   WAZAZI TUNAONA AIBU KUONGGEA NA WANETU KWA KUFATA MILA.
   MTOTO WA NCHI ZILIZOENDELEA HAFANYI SEX MPAKA AFIKISHE MIAKA 18,ANAJUA MADHARA YAKE .
   SIE TANZANIA UKIINGIA BLOG UTAKUTA ICHA ZAUCHI MPAKA UNAJIULIZA WAPI TUNAELEKA???
   NILIINGIA TUANGAZE BONGO BLOG UNAKUTA ETI MTU KAWEKA PICHA MTU ANALIWA TIGO .NAUMIA SANA NIMEANDIKA MPK BARUA KWA WAZIR WA HAKI ZA WANAWAKE JIBU SINA .
   WATOTO TUWAPE SIMU ILA TUSIWAWEKEE INTERNET.
   MIE NAISH ULAYA NA WANIITE MSHAMBA SIMPI MWANANGU SIMU YENYE INTERNET,
   WAZAZI NA DINA PLS ANZISHENI DARASA LA WAZAZI JUU YA WATOTO. KUNA WENG HAWAJUI WAFANYE NINI.
   WATOTO WENYE BIKIRA NI WACHACHE KWA SASA

  • Anonymous

   November 14, 2014 at 11:57 pm

   miaka 12 bado jamani kwenye nchi za watu hiyo ni rape,kwetu tunachukulia swala la kawaida tu pia wazazi wengi hawaongei na watoto kuhusu maswala haya utakuta limjomba linabaka humo ndani,house boy anabaka humo wazazi kimya.

 17. Anonymous

  November 12, 2014 at 1:31 pm

  mmmhhh kama nakosea mtanisamehe, lakini mimi sioni kwanini huyo mama aumie kwa jibu alilopewa na mumewe. je alitegemea mume akurupuke kuchukua hatua kabla ya kufanya uchunguzi na kupata jibu sahihi? na kingine katika utanzania wetu mama ndio hua karibu na watoto zaidi kuliko baba, kuulizwa kwanini hakugundua hilo jambo mapema ndio iwe sababu ya kutaka kuachana na huyo mumewe? ninachokiona mimi hapo ni mama anashindwa kua muelewa anaona kwasababu mvulana ni yule aliemkuta nae mumewe na msichana ni yule aliekuja nae basi bintie hatendewi haki, je ingekua wote ni watoto waliowazaa pamoja angekua na mtizamo alioko nao sasa hivi?, mimi naona hilo ni tatizo limejitokeza inatakiwa kufanya uchunguzi na kupata jibu sahihi halafu hatua zichukuliwe za kuhakikisha hilo tatizo halijitokezi tena. na pia kuwaelelimisha hao watoto wajuae nini wanapaswa kufanya

  • Anonymous

   November 14, 2014 at 12:45 pm

   Omba yasikukute mama maisha ushauri , unapomwambiab mwenzio mtoto wafulani anolewa lazma aje na reaction ya kuonesha kafurahi au kachukizwa, swali lina kuja na nani?
   Wewe ni ni mwanamke unapomweleza wemzio anatakiwa ajibu jibu lenye kuonesha kaumia.
   angeonesha msisimko swali la kwanini hugundua halina jibu sahihi. Ss hata kama ningegundua si ndo Tendo lisha tendwa .

   kama baba alitakiwa aoneshe uanaume wake sio ule wa kuvaa suruali ni ule unamfanya aitwe baba. Je ingekuwa wakwake ni wa kike angeukiza hivyo.

   HAKUNA MWANAUME MALAYA au BIKIRA;
   Kisaikologi kamwaribia mtoto wa kike ndoto zake ,

   SIKILIZA OPRAH WINFREY story tya maisha yake utajua wanawake wanamaumivu walotoka nayo utotoni .

  • Anonymous

   November 15, 2014 at 12:00 am

   sasa hapo kuna uchunguzi gani ufanyike?binti wa miaka 12 hawezi kutunga anafanyiwa mchezo mmbaya,seriously kuna mda tutumie akili,hapo wote waitwe wapewe adhabu kali especialy huyo mvulana maana anaweza kuja kuwa pedophile bure maana ndio wanavyoanzaga then atupwe boarding kabla hajalala na watoto wengine humo ndani.

  • Anonymous

   November 18, 2014 at 2:21 pm

   anony 4:45 am unaumia kwa kitu ambacho hakina maana hapo ungejiweka kwenye hiyo nafac ya huyo mwanaume alafu ndo umjudge kiukweli lazima aulize swali km hilo koz ww ndo upo karibu na watoto na umesema c mara ya kwanza mwanao kufanyiwa mchezo mchafu je km mm kwa nn hukugundua mapema na km kaumia alitakiwa alie ndo ujue kaumia yawezekana kaumia lakini anashindwa kukupa support koz of maswali mengi alonayo kichwa ikiwa ni pamoja na hilo ulikuwa wapi ucgundue mapema alafu kingine mtoto wa miaka 12 kwa dunia ya ss anaelewa anachofanya ni nn kwann hakusema hiyo mara ya kwanza kwamba alifurahia sahv kaumizwa au ni vp. hapo solution c kumchukia au kumlaumu mumeo na kukimbia ndoa koz of watoto tena unaowalea ingekuwa ni mumeo ndo anamtendee mwanao hayo ungekuwa sahihi kukimbia kaa na wanao ongea nao tena wape adhabu maana wanajua walichokuwa wanafanya mwisho kabisa watenganishe all the best mama

 18. Anonymous

  November 13, 2014 at 7:18 am

  Ok,asante kwa kufunguka kuhusu umri,dada kwa mtazamo wangu hapo WOTE WANA MAKOSA,kwanza kwa umri wa mwanao nadhani kama anasoma atakuwa darasa la sita kama sikosei na kwa umri huo kwa shule zetu siku hizi elimu ya jinsia na uzazi inaanza kutolewa darasa la tano na sidhani kwa umri wa mwanao kama atakuwa hana idea yeyote na mambo hayo hata kama wewe hujawai kuongea nae alafu pia ni ngumu kuelewa anaposema kaka ananivua chupi ananifanya mchezo mchafu zaidi ya mara mbili tena akanyamaza na kitendo cha kusema hivyo huyo anaonyesha anauelewa fulani kama ni kosa, na huyo mtoto wa KIUME,kwa umri wake pia anaonyesha anafaham vizuri kama ni kosa na yupo katika kile kipindi cha kutaka kujaribu na kujifunza vitu vingi vya ukubwani na hasa hayo mambo ya mapenzi kwa kifupi ni umri unamsumbua,Lingine nyinyi WAZAZI WOTE MNAMAKOSA NA MSILAUMIANE kwa sababu inaonyesha ni jinsi gani hamuongei na watoto wenu kuhusu makuzi yao na kujitambua ,Lingine nikushauri tu dada wala usikimbie ndoa wewe valia njuga tatizo na mlimalize waiteni watoto na waite wanafamilia wawili watatu kutoka upande wako na mumeo mkae kikao kuwaonya baada ya hapo wapeleke kwa mwanasaikolojia awape elimu zaidi na kuwaweka sawa kisha mfanye utaratibu wa kuwatenganisha hata boading kwa upande wa shule.Pole kama nitakuwa nimekukwaza ni USHAURI TU.

 19. Anonymous

  November 14, 2014 at 12:01 pm

  nimejaribu kusoma kwa umakini sana comments zenu wapendwa na hiyo stori ya huyo mama nilichogundua mimi mama anashindwa kumlea mtoto wa mumewe na ninahisi anamchukia. ukiangalia umri wa hao watoto wala sio wa mtoto wa kike kwenda kushtaki sbb wote karibu wanalingana na wote wanajifunza kufanya hayo mambo na yeye hajiulizi kwa nini hakuambiwa binti alivyofanyiwa kwa mara ya kwanza! ukiwa mama unatakiwa kuadhibu watoto kama mama alafu baba akirudi unamweleza na yeye atawaadhibu kama baba. sioni sababu ya huyo mama kutaka kuondoka mwanaume hana kosa lolote.NAMSHAURI MWANAMKE MWENZANGU ONGEA NA WANAO TARATIBU KWANI WOTE WANAMAKOSA SAWA.

 20. Anonymous

  November 15, 2014 at 7:06 am

  inaskitisha aisee,pole dada

 21. Anonymous

  November 19, 2014 at 7:18 am

  Ningekuwa mimi kwanza kabisa ningewaita wote wawili wanieleze wakoje kIsha wakanijibu.Nikawauuliza kwa nini wameyafanya hayo waliyoyafanya? Wakinijibu nawalisha bakora wote wawili kisha namsubiri huyo baba yao nimueleze waliyoyafanya watoto baada ya hapo nasubiri atasemaje kama jibu halikuridhisha ndio nawaitwa wanafamilia watusaidie kutatua jambo hili kisha kuwapelewa watoto wote Hospital wacheckiwe na ushauri zaidi wakirudi hapo wote bording kama hatutakuwa na uwezo mtoto wa kiume aondolewe hapo pia na wakike aondolewe hapo kwishiney maana nikimuacha motto wangu nitakuwa napendelea.KINA MAMA MNAOFANYA KAZI KILA SIKU NASEMA HAYA MANENO ONGEENI NA WATOTO WENU IWE WA KIUME AU WAKIKE DUNIA IMEISHA SANA USIMUAMINI MJOMBA,KAKA,BINAMU, WAKINABABA WADOGO CJUI NA PIA MUWE MNAWAKAGUA WANENU UNAWEZA KUMKUTA MAMA MTOTO WA KIUMME NA WAKIKE MDOGO WAKUOGESHWA LAKINI HANA HABARI NAE MTASTUKA WATOTO WAMESHAOZA VIUNGO VYAO SHAURI YENU.

 22. Anonymous

  November 24, 2014 at 5:21 am

  Pole dear dada, Hakukuwa na subira pale eti baba arudi. kumbuka yule ni wa kwako na wa kiume ni wa baba. unaanza na mkwara mzito, adhabu, unamalizia kwa mumeo. Acha mawazo ikiwezekana fanya kila mbinu aondoke huyo mtoto hapo. au muondoe wako aende kokote.
  Punguza upole.

Leave a Reply