Uncategorized

WATOTO NA VIPAJI:MTOTO WA MIAKA TISA ALOSHINDA SHINDANO LA UPIGAJI PICHA HUKO UINGEREZA

By  | 

Kila mwaka hufanyika shindano la upigaji picha la National History musium la London.Shindano hilo lilianza toka mwaka 1964 na huitwa Wildlife Photographer Of The Year.La upigaji picha mambo ya utalii na viumbe vya mwituni.N mwaka huu mshindi ni mtoto wa miaka 9 mwenye asili ya Hispania Carlos Perez.

Wazazi wa Carlos ni wasafiri wa mara kwa mara na hupenda kusafiri kuzunguka dunia kuangalia vivutio mbali mbali vya utalii.Katika safari zao wamekuwa wakiambatana nae toka ana miaka 4.Na alianza kupenda kupiga picha toka ana miaka hiyo 4.Shindano hilo ni lilihusisha vijana mpaka miaka 17 na Carlos kuibuka mshindi wa mwaka huu.Baadhi ya picha  ndio hizo nilizoweka.

Wazazi kama inawezekana kusimamia na kusuport vipaji vya watoto wetu toka wadogo basi tufanye hivyo. Hatuwezi kujua Mungu amewapangia nini kupitia vipaji hivyo.

2 Comments

  1. Nilam Mohamed

    December 2, 2014 at 11:02 am

    Dada Dina mie naona wazazi wengi na jamii ya watanzania hawana utamaduni huo wa kuendeleza kipaji cha mtoto.Nasema hivyo kwa mfano wangu mie mwenyewe,Nilikulia katika mazingira kupenda kutangaza tokea nikiwa mdogo enzi za Betty Mkwasa anatangaza habari ITV.Basi nikawa nachukua casset za mama za taarab naenda kujirekodi nasoma habari weee mama alikua akigundua ananitandikaa!!!Basi nikakua hivyo mpaka nilipoanza kusikiliza redio kuanzia Leo tena ya marehemu Amina(MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA)Alikua ni mtu ambaye aliendelea kuniinspire kupenda kutngaza.Ukaja wewe Dina,lakini bado wazazi wangu hawakuwahi kunipa support yoyote na walikuwa hawapendi kabisa kusikia hayo mambo!Nilipokuja kumaliza form 4nikaomba nikasomee Utangazaji lakini hakuna aliyenielewa,na mwaka mmoja mbele nikaolewa nikiwa na miaka 19.Huko nilikoenda ndoani nikawa namuomba mume anipe nafasi ya kutimiza ndoto na kipaji changu lakini nayeye ikawa na vilevile basi hua nakaa mwenyewe naumia rohho vile naona ndoto yangu inayeyuka japo wewe ulikuja kuirudisha siku moja ulitoa post ya mwanamke mmoja mchoraji jinsi alivyoweza kutimiza ndoto yake,ile post ilinitia sana moyo dada dina.Ilinifanya niende kwenye audition za choice fm ilikua mwaka juzi mume wangu alipogundua movement zangu hizo alikasirika sana na mwisho nikaacha!!Sasa leo nilikua namsikiliza Joseph kusaga asubuhi kwenye cloud360 aisee aliniliza yule baba aliposema USIKUBALI MTU YOYOTE AKAKUWEKEA KIKWAZO KATIKA NDOTO YAKO KWANI KILA BINADAMU ALIZALIWA NA NDOTO YAKE SIMAMA UTIMIZE YAKO LEO!!Alipongea mengi ya kutupa moyo vijana,mungu ampe maisha maisha marefu aweze kufungulia fursa vijana wengi zaidi.Nisikuchoshe dada na gazeti languNamuomba mungu nije kutimiza ndoto za watoto wangu ili wasije ishia kuwa kama mimi.Na wazazi wengine pia nawaasa ukiona mtoto wako ana kipaji flani usikikalie na usimvunje moyo,mfanye asimame katika kipaji na ndoto yake ili siku moja akisimama mahali kutoa shukrani akushukr mzazi wake kwa kufikisha alipo.Naq si kumfane aje akae anakualaumu mzazi wake kwa kumyeyushia ndoto yake.NIMEMALIZA

  2. Anonymous

    December 11, 2014 at 3:20 pm

    Hata mm ndoto zangu hazkutimia kabsa nlimaliza form4 niklazmishwa kuolewa nlikua najifungia ndan nalia sana mapaka sasa maisha yangu yamekua ni kujuta wals cfurahh maisha ya ndoa kabsa wee acha tu inaumiza sana.

Leave a Reply