Uncategorized

WEWE UNGEFANYA NINI??

By  | 

House girl alitandika kitanda cha bosi wake Kama Sehemu ya jukumu lake la kila siku. Alipomaliza akakitazama sana kile kitanda cha bosi wake akasema naweza kufa bure bila ya kulalia kitanda kama hiki. Akasema ngoja nijaribu kulala angalau kidogo.
 Akavua nguo zote akaziweka chini, akabaki na gagulo tu akawasha AC akajifunika brangeti gubigubi akalala. Kwa bahati mbaya usingizi ukampitia kweli akalala fofofo.
Ghafla Mume wa bosi akarudi na haikuwa kawaida yake kurudi Muda huo. Alipoingia chumbani, akajua hakika huyu ni mke wangu na kwa kuwa jana tulikwaruzana atakuwa amekasirika tu. Akaogopa kumwamsha. Mwanamme akasaula, akabaki na msuli naye akajifunika hilo hilo blanketi kwa taratibu sana kwa hofu ya kumwamsha mke wake. Kwa bahati mbaya naye usingizi ukampitia, akalala fofofo .
Bosi aliporudi, akaingia chumbani, akakuta watu wawili wamelala fofofo. Akafunua blanketi kwa nguvu, akawakuta wote wawili; yaani yule mfanyakazi na mume wake wamelala pamoja. Walipoulizwa kila mtu akaeleza ukweli wake.

1. Je, kama wewe ungekuwa ndiyo yule mke wa bosi ungewaelewa?

2. Je, kama wewe ungekuwa ndiyo yule mfanyakazi ungejitetea vipi?

3. Je, Wewe ungekuwa ndiyo yule bosi ungejitetea vipi?

4. Je hapo ugomvi utakuwa umesababishwa nani? Mke, mume au mfanyakazi?

3. Story inawafunza nini mabosi, wake za mabosi na ma hausigeli?

11 Comments

 1. Melwyn

  November 16, 2014 at 4:42 am

  Imekaa vibaya

 2. Anonymous

  November 16, 2014 at 9:33 am

  Lol hii kali asee. ha ha ha! hapa hata kama utakuwa mkweli kiasi gani hakuna mwanadamu atayeamini hata ufanyaje. Kwa kipindi hichi kwa kweli ni wale tu ambao wanashikilia dini ndo wanaweza kuaminiana.

 3. Anonymous

  November 16, 2014 at 9:40 am

  heheee….1. Nisingewaelewa kwakweli….kwasababu huyo mume alivoingia kujifunika hakusikia kama harufu ni tofauti as kila binadamu anaharufu yake…tena mkeo mnaelala pamoja kila siku lazima ujue hilo.
  2. Ningekuwa mfanyakazi ningesema ukweli kwa kumbembeleza kwa hali ya juu na ningekuwa radhi kuchunguzwa kama nimefanya mapenzi masaaa machache…
  3. Ningekuwa mume pia ningetumia utetezi sawa na wa dada wa kazi
  4. Hapo ugomvi utakuwa umesababishwa na mke…chumba ni cha baba na mama tu,y umruhusu msichana kuingia? Yote haya yasingetokea kama mama asingemruhusu msichana kuwa anaingia chumbani kwao
  5. Kwa mabosi…wapange pamoja na wake zao jinsi watakavokuwa wanaiendesha nyumba na si kumwachia mama pekee…..yawezekana bosi alikuwa hajui kama mfanyakazi ndo huwa anasafisha rum ya
  Kwa wake….mfanyakazi awe na mipaka ya kazi zake..vitu kama usafi wa chumba chenu,usafi wa nguo,upishi,kupiga pasi…inafaa mwanamke mwenyewe uvifanye…coz hiv vitu huwa vina love ndani yake…
  Kwa wafanyakazi…..y playing with your boss`s stuffs?….fanya yako…kwanini ukalale chumbani tena unavua nguo kabisa na unajua kunakupitiwa usingizi….kama hivyo sasa….kakutwa

 4. Anonymous

  November 16, 2014 at 8:37 pm

  1.NINGEJUA WALIKUWA KTK PENZI MOTO WAKAPITIWA NA USINGIZ
  2.SIDHANI KAMA NINGEJITETEA KWANI UKWELI WANGU HAUNA NAFASI PALE
  3.LABDA NINGEHADITHIA ILA UTETEZI HAUNA NAFASI
  4.UMESABAMISWA NA MKE

  5. INATUFUNZA SIO MAJUKUMU YOTE UWAPE WAFANYA KAZI WA NDANI KWANI WANAWAKE TUNAOLEWA KAA PICHA WAFANYACHAZI NDO WENYE NYUMBA ZETU,
  NA TUNAONA SIFA KUWAPA MAJUKUMU TUNAJISIFU NINA DADA ANAFANYA KAZI ZOTE.
  DADA NDO ANAJUA KIPI HAKUNA NA KIPI KIONGEZEWE NDANI SIO MAMA,
  UKIANZA KUGOMBA KAMA MCHELE HAMNA KWA NINI HUKUSEMA WEWE NDO UNAJUA KILA KITU.
  JE SISI WAOLEWAJI TUJUE NINI.

  WADADA HATA WAKILALA NA WAUME ZA MABOSI ZAO HAWANA MAKOSA WANAPEWA MAJUKUMU MENGI MNO.
  MIE SHEMEJI YANGU ALITEMBEA NA DADA WA KAZI MIAKA NA MKE HAKUGUNDUA ,NILITAMANI KUSEMA NAOGOPA NIKASEMA ATAJIJUA MWENYEWE .NA MPAKA LEO SIJUI KAA ANAJUA HILO

 5. Anonymous

  November 17, 2014 at 1:04 pm

  Hapo kwa mawazo ya haraka haraka, ningejua tayari wameshazini, pia inategemea na wewe au mimi mama nilivyo, huwa nachukuliaje tatizo linapotokea? ikiwa ni mama wa kukurupuka hapo tayari ni kesi, ikiwa utaziuliza kwanza mbingu, utachukua muda kidogo na kutafakari, na kwa maombi mengi kumuuliza Mungu ili akupe jibu la kufanya, akina mama tunatakiwa tusibweteke kuruhusu msichana mpaka aingie chumbani akufanyie usafi, wewe umeolewa ili iweje, hata kama kuna ugomvi tandika mwenyewe, na jua lisichwe hujasamehe. kumbuka hasira hukaa vifuani mwa wapumbavu, na mwanamke mpumbavu huvunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. mahousigirl wawe na mipaka, sio chumbani, chamba chako ni mahali maalum sana, hairuhusiwi mtu kuingia ingia ovyo.

 6. Anonymous

  November 17, 2014 at 3:03 pm

  Yaani hapo mwenye makosa ni aliyeruhusu hausigeli aingie kutandika kitanda, kwa uvivu gani au starehe gani mtu usiweze kutandika kitanda chako!! alaa! hamna kesi hapo

 7. Anonymous

  November 18, 2014 at 7:21 am

  Dina hata km niko busy kiasi gani housegirl hawezi kunitandikia kitanda…kwanza ndani kwangu anafuata nn house girl?ujinga wa mwanamke ……tusijisahau

 8. MOJAONE

  November 25, 2014 at 1:35 pm

  Mfanyakazi wetu wa ndani mpaka hivi sasa baada ya miaka miwili hajui chumba cha boss wake kimekaaje.

 9. Anonymous

  December 2, 2014 at 10:30 am

  Ningekuwa mie ni housegairl na mume ningeongea ukweli wote ulivokuwa then haro ya mke kuamini ama kutoamini namwachia yeye mwenyewe na mungu wake.

 10. Anonymous

  December 3, 2014 at 9:52 am

  aise hapo ni uzembe wa mke ww utamwachache msichana wa kazi aingie chumbani mwake?haifai wamama kupweteka

 11. Anonymous

  December 3, 2014 at 10:59 am

  kwakweli na mimi ningefikiria wameshafanya ni ngumu kuamini katika hali ya kawaida, ila tujifunze wamama msichana wa kazi ataingiaje chumba unachalala na mme wako? kwanza hatakiwi hata kukijua kikoje, mimi nikisahau kufunga chumba changu lazima nirudi. hata nikiwa naumwa simruhusu dada wa kazi aje anifanyie usafi nitasubiri mpaka nipone nifanye mwenyewe, sasa mpaka kidanda utandikiwe! jamani mambo mengine wamama tunajitakia.

Leave a Reply